Mita inayofanana na hiyo unayoongelea niliiona uwanja wa nanenane Mbeya mwaka 2017. Nilivutiwa sana aisee. Yaani yenyewe unaifix kwenye nyumba ya wakazi wengi. Kila mtu ananunua umeme wake mwenyewe ingawa mita ya TANESCO ni moja. Na kila mtu anaangalia salio la units ambazo amebakiwa nazo. Umeme unaweza kuisha chumba kimoja vyumba vingine wanaendelea kuenjoy. Ukisafiri umeme wako unabaki vile vile hadi urudi unaukuta vile vile.
Halafu ile mita inaingizwa namba kulingana na idadi ya vyumba. Kama vipo 8, kwa mfano, inaingizwa namba 1 mpaka 8. Chochote unachofanya kama kuingiza umeme unaingiza kwanza namba ya chumba mfano 3 kisha unaingiza token. Kuangalia salio ni hivyo hivyo unaingiza kwanza namba ya chumba ndio uone salio la units.
Yaani ni safi sana. Wao walisema watawasiliana na TANESCO ili kuangalia uwezekano wa kujumuisha teknolojia hiyo kwenye mfumo wa umeme ila ndio nasubiri hadi leo sijui waliishia wapi.