Kuunguruma kwa kongamano la Wanataaluma Dar: Moto wayaka!

Mimi nina matumaini sana na hawa jamaa. Lakini, tutapima ni maazimio na utekelezaji wake. Wasije wakajikuta wanaitwa majina na kina Makamba!

Mzee Mwanakijiji,

Wakati wa maazimio kwa Tanzania umepita; kuna maazimio mengi sana ila hakuna utekelezaji.

Hawa wana taaluma wetu ni bora waazimie kutekeleza mambo machache kuliko kuja na maazimio kibao ambayo yataishia kapuni.

Kuna watu nawaamini kwenye hicho chama chao ila Watanzania tumesalitiwa mara nyingi sana na hawa wasomi wenzetu. Mimi kwasasa siamini tena blah blah! Nionyeshe umefanya nini kwenye haya mapambano, kisha nitaamini kama kweli uko serious.

Vinginevyo nawatakia mafanikio mema!
 
Hatma ya watanzania imo ktk mikono ya watanzania wakielimishwa.

Nadhani hawa wanataaluma wangekuja na mkakati wa kuwakomboa watanzania kifikra hasa hasa kuchechemiza mapinduzi katika elimu ili ndani ya miaka 20 ijayo tusiongozwe na watu style ya mzee mapesa yaani wasomi wasio na maadili.

nina hisia kwamba wanaweza kuja na hoja kinzani dhidi ya yaliyojiri ktk kongamano la MNF. Kama watafanya hivyo basi maneno ya mwalimu yatatimia kwamba kusoma kwingi ni kuelekea ujingani kama hautachukua tahadhari
 
Tusubiri tuone watakayoyazungumza tusihukumu kabla hatujaona waliyayaazimia na njia watakazotoa jinsi ya kuyakwamua
 
"Pay no attention to what the critics say. A statue has never been erected in honor of a critic." Jean Siberius

Tumekaa kitako kukosoa tu kama kawaida!, kwa nini tusiwe mstari wa mbele kuleta mabadiliko tunayoyataka ndani ya TPN..!!? Si iko wazi kwa wanataaluma wote!
 
Huu siyo wakati wa maazimio japokuwa wazo la TPN ni zuri. Mimi nafikiri watanzania tunahitaji kujikita zaidi ktk utekelezaji wa maazimio lukuki yaliyo kwisha tolewa miaka ya nyuma na yamewekwa kapuni.

Kwa mfano, suala la ku-review mikataba ya madini ambayo imesainiwa wakati wa mwinyi na mkapa linahitaji utekelezaji lakini shangaa kwamba kila mtu yuko kimya.

Kuwa na tume huru ya uchaguzi inayo shirikisha vyama vyote vya siasa, hili nalo linahitaji utekelezaji tu, je wasomi tumefanya nini ktk hili?? au tunaona ni sawa??
 
Nadhani wakicheza karata zao vizuri wanaweza kujiwekea miongoni mwa makundi ya mabadiliko. Hata hivyo ni lazima waoneshe kuwa wako tayari kulipa gharama ya mabadiliko wanayoyataka.
 
Mh, hii ngumu kweli kwetu watanzania, ni nani tanzania anaweza kuandaa kitu kikapokewa na positive mazee?

Yaani inavunja moyo kweli

Sasa wewe angalia mada zenyewe tu, kitu kimoja kimenyumbulishwa seven ways kujaza empty space, inaonyesha hawa watu hata hawana cha kuchangia above abstraction layer.

Halafu maswala muhimu kabisa wanaogopa kuyagusa.

Mbona katika abstraction layer tuna makabrasha kibao yamejaa policies nzuri tu, tatizo utendaji.

Ndiyo maana Julius anakupa hood philosophy ya "show me better than you can tell me"
 

Vipi kama wengine hatuna taaluma na wengine taaluma zetu ni criticism?

Na huyo mshamba aliyesema hakuna statue iliyokuwa erected for a critic aliona a statue ndiyo highest honor, mbona ni superficialities za antiquated roman era? The entire enterprise of science is based on criticism.

Without criticism Galileo asinge expose makosa ya Aristotle, Copernicus asinge expose makosa ya Ptolemy, Einstein asinge expose limitation za Newton, na sisi tusingekuwa na GPS na internet.

Hata a pure critic ana a role in society, the more literate and scientific a society gets, the more critics are needed.

Do not belittle the value of the enterpise of criticism, go toe to toe with the contents of criticism, if you can.
 
I cross my fingers for the sucess of this meeting.Who knows what will come out of it! Kila kitu lazima kiwe na mwanzo
 
I cross my fingers for the sucess of this meeting.Who knows what will come out of it! Kila kitu lazima kiwe na mwanzo

Tatizo letu ndilo hili, we "cross our fingers", we "pray", we "hope" etc etc

We do everything except some critical thinking.

No wonder we are where we are.
 
Nadhani wakicheza karata zao vizuri wanaweza kujiwekea miongoni mwa makundi ya mabadiliko. Hata hivyo ni lazima waoneshe kuwa wako tayari kulipa gharama ya mabadiliko wanayoyataka.


Hapo kwenye bold ndipo penye mtihani kwa hawa Wasomi/ Wanataaluma.

Kama Keil alivyosema hapa tatizo letu lipo kwenye siasa...hatuna siasa safi yenye kutoa viongozi wasafi. Turekebishe hilo...haya mengine yote itakuwa mteremko kuyarekebisha.
 
Hakuna lolote la maana litakalotokana na hilo kongamano. Natoa miezi miwili tu na watu watakuwa washasahau hata kama kulikuwepo kitu kama hiki.
 
.

critique is the 3rd eye. Exellence can only come where there is a challenge, rising against chalenges is what brings success, no challenge without criticism, therefore criticisim is the key to success.

Man is an animal by nature, ili kufurahia mafanikio yako, you have to earn that respect by being a conquarer. Ndio maana hata kwenye mambo fulani ukigusa tuu, ukapata bila kutokea jasho, hutauthamini ushindi wako, hivyo inaishia kuwa 'easy come easy go'. Ili kupata morali ya unachokipiginia, lazima uset targets na how to hit the bull, bila chalenge, you'll never hit and end up being the failure kama Tanzania tulipo.

Ndio maana nawaona waimbaji wa nyimbo za sifa, shangwe na mapambio kwa mkulu, eti kafanya hiki, kafanya kile, hawamsaidii na wala hawaisadii chochote nchi hii, msaada wa kweli utatoka kwa macritic wataompa challenge of doing better na sio kuridhika na alichokifanya huku nchi ikizidi kuzama kwenye umasikini uliotopea na kibwagizo cha 'maisha bora kwa kila Mtanzania' kikikosa mashiko.

long live critique.
 
kuna 'constructive criticism' because you have a better perspective in comparable, na kuna just 'negative criticism' unapaenda kubisha tuu.

Mfano how do we know in two month nothing would come out of this so called Kongamano. Sasa hizi ndio fikra za Miafrika, huwa inakuja na pessimistic perspectives in the name of criticisms.
 


kuna msemo unsema to be successfull u need friends,but
to be very successfull u nedd enemies.....
 
Wengine wanatafuta channel za kutokea hapo

Wengine wanatafuta kuonekana nao wamo

Hamna aliye na kipya, ukiangalia maswali yao tu utaona kama wanataaluma ndio hawa bora labda hao wabeba boksi.

No more comments - You have said it all

Labda 2010 in mind? "Nitoke Vipi"?
 

Huyo niliyemnuu ameongea kwa kutumia lugha ya picha naona hilo hukuliona

Without criticism Galileo asinge expose makosa ya Aristotle, Copernicus asinge expose makosa ya Ptolemy, Einstein asinge expose limitation za Newton, na sisi tusingekuwa na GPS na internet.

Ukosoaji unaenda sambamba na uwajibikaji hao unaowatolea mfano walifanya tafiti ili kuweza kuja na ukosoaji walioutoa huwezi kamwe kulinganisha ukosoaji huo(wa kisayansi) na ukosoaji wa JF ambao watu wanakosoa hata kabla kongamano halijafanyika! Watu wamefanya nini ili kuweza kukosoa kongamano la TPN? Ukosoaji wa namna hii tunauita umende. hiyo ndio hoja yangu

Hata a pure critic ana a role in society, the more literate and scientific a society gets, the more critics are needed.

Do not belittle the value of the enterpise of criticism, go toe to toe with the contents of criticism, if you can.

Hilo nalikubali lakini liendane na uwajibikaji, sio ukosoaji mtupu bila hoja
mfano mtu anasema "hao hamna kitu ni waganga njaa!" hiyo ni nini??
 
Jamani basi tuanze kuyafanyia kazi mambo tunayozungumza. Haya mambo sio mapya.
 
Haya basi ni kipi kilichoongeleka huko? mlio karibu mtuelezee kwani ni jioni tayari.
 

Constructive criticism ni nini? Umesema constructive criticism inambidi critic "awe na better perspective in comparable" hii sentensi haijasimama, inaelea elea tu.

In comparable what? Do you mean in comparison? How exactly do you determine what is better?

Kama unamaanisha kwamba in order to claim to have "constructive criticism" ni lazima uje na solution kamili, nakataa.Nimesema hapa kabla, hata kuzuia kwenda kubaya bila kujua kuzuri ni wapi ni criticism nzuri tu.

Lets say tunatafuta solution ya swali la kihesabu, square root ya 64. Lakini sote hatujui square root ya 64, halafu mtu anakuja anakuambia square root ya 64 ni 128, hata kama hujui exactly square root ya 64 ni nini, lakini unajua kwamba square root ya 64 ni factor ya 64, basi utajua kwamba square root ya 64 ni lazima iwe ndogo zaidi ya 64.

Hiki ndicho tunachofanya JF hapa.Hardly kuna mtu anaweza kujidai anayo majibu ya maswali yanayoikabili nchi nyetu. Lakini tukiona mtu anatuambia square root ya 64 ni 128, ni lazima tuanze kusema kwamba square root ya 64 haiwezi kuwa twice the value ya 64, hata kama hatuna jibu kamili la kusema kwamba square root ya 64 ni nini.

Ndicho tunachofanya, nimesema kama kweli wako serious na the bigger picture Tanzania hawaonyeshi hivyo kwa mujibu wa maada zao, maada zao zinatuambia square root ya 64 ni 128, wakati tunajua square root ya 64 ni ndogo kuliko 64, hata kama hatuna jibu sahihi, tushaanza kupata the right direction, kwamba ili kuipata square root ya 64 itabidi tuangalie kuanzia 64 kwenda chini, sio juu.Hii ni step nzuri tu. Sasa utasemaje hatuna constructive criticism kwa sababu hatuna majibu?

Angalau mtu anaweza kuwa creative na kuanza 64/2 akapata 32, akafanya 32 square, akaona kubwa kuliko 64, akafanya 32/2 akapata 16, akafanya 16 square akapata kubwa kuliko 64, akafanya 16/2 akapata 8, akafanya 8 square, voila, amepata jackpot, 64, kazi imekwisha.

Kwa hiyo si sawa kusema kama critics hawana jibu wasi criticise wakati criticism hata kama haina jibu kamili inaweza ku improve method ya kupata jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…