Kuunguruma kwa kongamano la Wanataaluma Dar: Moto wayaka!

Kuunguruma kwa kongamano la Wanataaluma Dar: Moto wayaka!

Huyo niliyemnuu ameongea kwa kutumia lugha ya picha naona hilo hukuliona



Ukosoaji unaenda sambamba na uwajibikaji hao unaowatolea mfano walifanya tafiti ili kuweza kuja na ukosoaji walioutoa huwezi kamwe kulinganisha ukosoaji huo(wa kisayansi) na ukosoaji wa JF ambao watu wanakosoa hata kabla kongamano halijafanyika! Watu wamefanya nini ili kuweza kukosoa kongamano la TPN? Ukosoaji wa namna hii tunauita umende. hiyo ndio hoja yangu



Hilo nalikubali lakini liendane na uwajibikaji, sio ukosoaji mtupu bila hoja
mfano mtu anasema "hao hamna kitu ni waganga njaa!" hiyo ni nini??

Sijui kwa wengine, mimi nimekosoa kutokana na maada zao walivyozitoa, hazi reflect professionals walio serious, zinaonekana ni kama majibu ya mtoto aliyepewa homework aifanye weekend, akacheza weekend nzima, akawa anataka kujibu maswali Monday morning akijiandaa kwenda shule simultaneouly huku akinywa chai na kuchana nywele.

Kama tunaweza kujadili hilo, criticism yako ya criticism itakuwa constructive.
 
Wengine wanatafuta channel za kutokea hapo

Wengine wanatafuta kuonekana nao wamo
Hizi ndizo criticism za mtindo wa akina Galileo,Einstein na Copernicus..????

Hamna aliye na kipya, ukiangalia maswali yao tu utaona kama wanataaluma ndio hawa bora labda hao wabeba boksi.

Kuna tatizo gani kujadili haya..
Baadhi ya Mada zitakazojadiliwa, kuwekewa mikakati ya kiutendaji na ufuatiliaji ni pamoja na:
1. Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara
2. Ni Vipi Wanataaluma Wanaweza Kusaidia Watanzania wa Kawaida Waweze Kushiriki Katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa na Kuboresha Maisha Yao
3. Jinsi Wanataaluma Wanavyoweza Kukabiliana na Changamoto katika Kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa, Kielimu, Kijamii, nk.
4. Namna Gani Wanataaluma Waliopo Nje ya Nchi Wanaweza Kushiriki Kuleta Maendeleo Nchini
5. Wanataaluma na Dira ya Maendeleo ya Taifa Letu: Tukotoka; Tulipo, Tunakokwenda: Changamoto na Ufumbuzi
6. Je, Ni Wakati Gani Mwafaka Wanataaluma Walazimike Kuchukuka Hatua za Kuleta Mabadiliko Na kwa Vipi?
7. Ni Mikakati Gani Watumie Wanataaluma Kupeana Habari na Taarifa Za Uhakika na kwa Muda Muafaka
 
Bluray,
I am pretty sure you know there is a difference between constructive criticism and denunciatory diatribe that almost borders on downright rudeness. What you are vehemently defending as constructive criticism is neither that nor helpful engagement. To all intents and purposes this is a Bluray display of intellectual snobbery and foppishness masquerading as objective insight or analysis. I was especially put off (I must admit) by the grandiloquence of your arguments which made me wonder if you are capable of seeing the forest for the trees!

You seem to be focusing on the small details (the trees) and fail to grasp the larger plans or principles of the TPN organization. Amazingly, (and this underscores my point) you had the audacity to turn this into an academic debate on “the philosophy or politics of criticism” when you wrote:

“Without criticism Galileo asinge expose makosa ya Aristotle, Copernicus asinge expose makosa ya Ptolemy, Einstein asinge expose limitation za Newton, na sisi tusingekuwa na GPS na internet”.

The point you are making is unassailable but also irrelevant in the grand scheme of things especially when you take into account that the TPN is a fledgling organization that is trying to find its footing and establish its brand, therefore it needs encouragement not condemnation.

Let’s examine one example that I personally find quite relevant. I have a friend who is a professor in some of the leading US universities who want to establish a kind of research partnership with some of the institutions in Tanzania and wanted to use this TPN gathering to make that announcement. These types of relationships can be a game-changer for the small underfunded researcher in any of the research institutions in Tanzania that has been selected for this type of partnership. When you get right down to it, he who pays the piper gets to select the tune, in this case the US pays for the research and therefore they get to select the partner with whom to work.

What I don’t understand is, why in your infinite wisdom do you think this it is such a terrible idea for my friend (the US based professor) to attend this type gathering for the purpose of exchanging views and exploring ways in which such cooperation in research can be achieved with like-minded individuals in the academic, scientific and professional spheres? The TPN could serve as an organization to initiate these types of discussions. Why did you find it necessary to dismiss and brush aside that possibility right from the get go?

Your comment: “Hamna aliye na kipya, ukiangalia maswali yao tu utaona kama wanataaluma ndio hawa bora labda hao wabeba boksi”, which, on closer examination seems based on little more than a cursory understanding of what the TPN is really attempting to accomplish, is as entertaining as it is amusing, and it says it all. You don’t believe for one minute that these types of exploratory engagements can be productive or can serve any useful purpose!

I can bring up other scenarios, but I don’t wish to belabor the point. It would be ill-advised and pointless since the thrust of the message has been propagated. Criticism has its place in the world of philosophy (and politics) but in this case it merely serves as a destructive force not a constructive one with the potential for far more damage. Some of us from Sukumaland would find this as a demonstration of grandiose sense for self-worth if not downright narcissistic. By the way, I’ve noticed that most (not all) of you postings share the same underlying theme but I am new here so don’t read too much into that.

Saidhorizons
 
Tatizo letu ndilo hili, we "cross our fingers", we "pray", we "hope" etc etc

We do everything except some critical thinking.

No wonder we are where we are.
And that is what I crossed my fingers for.My anticipation was to have you leading with others in the open about the importance of critical thinking. I know the issue of prayers is not with you, as you have declared about not believing in God, but prayers work my budd!!!
 
Napenda falsafa ya robert nesta marley:kwamba the greatest man you did ever see was just a baby!hawa wanataaluma wapongezwe walau kwa kukutana kama hatua muhimu.huhitaji cheti cha logistics kujua kuwa kukutanisha watu wengi wenye taaluma na mitazamo tofauti ni jambo kubwa. Kwa sababu hiyo anayefikiri hawana lolote amekosea kidogo lugha na apewe msamaha maana hawana lolote ni falsafa ya kuridhia na yaliyopo na kukata tamaa!wanataaluma wakutane, wanywa bia ama soda wakutane na wasio na ajira wakutane iwezekanavyo! Mwisho wa siku mikutano hii italeta changamoto na zingine zitatatuliwa na wale wenye kudhani wana jipya basi!
 
After all these years I have lived, I have come to realize that "kuazimia na kutekeleza ni vitu viwili tofauti kabisa". So, the bottom line is, haya makongamano huwa yanaishia kutoa maazimio. Lakini utekelezaji wa hayo maazimio ni zero. Its time we change this.
 
hata kilichojadiliwa sijakielewa/SIJAKIONA!
MUNGU WANGU!hizi siasa hizi?!DAH
 
Wazalendo na Wanataaluma wa JF; nashukuru mambo yameisha salama inagawa uchovu ni mwingi sana. Kongamano limefanikiwa zaidi ya tulivyorarajia.

Washiriki waliofika walkitoka Nje ya Nchi; Ndani ya Nchi DSM na Mikoani. Na wengine wametuma maoni yao kwa maandishi na barua pepe. Idadi ianfika 100. Hakika pia walikuwapo wanataaluma maarufu na baadhi ya wanasiasa amabo wote walikuja na kofia zao kama wanataaluma.

Majadiliano yaliendeshwa kwa namna ya Elezea Issue; Toa Problem au Challenge; Propose Solution, Kisha Utekelezaji wake. Then Wengine Wanachangia na Makubaliano yanafikiwa. Ilikuwa ni issues tu, hakuna lawama wala personalities. Ilikuwa kama tunatafuta Plan B ya kufanya mambo yafanyike na tulitambua weakness zetu kama Wanataaluma na nini tufanye.

Mimi sikujua kuwa kumbe tunaweza kuleta mabadiliko makubwa sana na hata kuwawajibisha wanaofanya makosa au wasiotenda kwa kuwa katiba na sheria zinatupa uwezo huo ila ama tulikuwa hatujui ama tulikuwa hatutaki kuchukua hatua.

Maazimio na Mikakati ya Utekelezaji ni Mizuri sana na nina imani. Nitafanya jitihada ikiwa tayari niipost hapa JF na Kutoa Press Release. Tulimaliza Usiku.

Tusaidiane kuanza kubadili mindset za watu, hii pia ni sehemu ya tatizo kubwa.

Wasalaam.

SM
 
Huu siyo wakati wa maazimio japokuwa wazo la TPN ni zuri. Mimi nafikiri watanzania tunahitaji kujikita zaidi ktk utekelezaji wa maazimio lukuki yaliyo kwisha tolewa miaka ya nyuma na yamewekwa kapuni.

Kwa mfano, suala la ku-review mikataba ya madini ambayo imesainiwa wakati wa mwinyi na mkapa linahitaji utekelezaji lakini shangaa kwamba kila mtu yuko kimya.

Kuwa na tume huru ya uchaguzi inayo shirikisha vyama vyote vya siasa, hili nalo linahitaji utekelezaji tu, je wasomi tumefanya nini ktk hili?? au tunaona ni sawa??

Nakubaliana na wewe kuwa kuna sera nyingi ziliasisiwa hapa lakini utekelezaji wake ni wa kisanii sanii tu na ndio maana sera zile zile zinarudiwa kwa majina tofauti katika awamu tofauti!! Mfano mzuri ni hii mpya ya KILIMO KWANZA; mambo ya kuweka msisitizo kwa sector ya kilimo yamezunngumziwa toka enzi ya marehemu BRYSON NA BARONGO wakati wakiongoza wizara ya kilimo , baadae ikaja SIASA NI KILIMO, KILIMO CHA KUFA NA KUPONA etc. Je, hao wakubwa wametafakali na kufanya tathmini ya wapi hatukufaulu huko nyuma katika kufanikisha kilimo kabla ya kuasisi KILIMO KWANZA ili makosa hayo yasirudiwe? Waswahili husema kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa!! Sijui kama wanamtandao wanauelewa huo.
 
Wazalendo na Wanataaluma wa JF; nashukuru mambo yameisha salama inagawa uchovu ni mwingi sana. Kongamano limefanikiwa zaidi ya tulivyorarajia.

Washiriki waliofika walkitoka Nje ya Nchi; Ndani ya Nchi DSM na Mikoani. Na wengine wametuma maoni yao kwa maandishi na barua pepe. Idadi ianfika 100. Hakika pia walikuwapo wanataaluma maarufu na baadhi ya wanasiasa amabo wote walikuja na kofia zao kama wanataaluma.

Majadiliano yaliendeshwa kwa namna ya Elezea Issue; Toa Problem au Challenge; Propose Solution, Kisha Utekelezaji wake. Then Wengine Wanachangia na Makubaliano yanafikiwa. Ilikuwa ni issues tu, hakuna lawama wala personalities. Ilikuwa kama tunatafuta Plan B ya kufanya mambo yafanyike na tulitambua weakness zetu kama Wanataaluma na nini tufanye.

Mimi sikujua kuwa kumbe tunaweza kuleta mabadiliko makubwa sana na hata kuwawajibisha wanaofanya makosa au wasiotenda kwa kuwa katiba na sheria zinatupa uwezo huo ila ama tulikuwa hatujui ama tulikuwa hatutaki kuchukua hatua.

Maazimio na Mikakati ya Utekelezaji ni Mizuri sana na nina imani. Nitafanya jitihada ikiwa tayari niipost hapa JF na Kutoa Press Release. Tulimaliza Usiku.

Tusaidiane kuanza kubadili mindset za watu, hii pia ni sehemu ya tatizo kubwa.

Wasalaam.

SM
ahsante!walau nimeelewa kitu fulani!
tunasubiri hiyo mikakati utupostie.

hilo la MINDSET.dah!ni process.enewei ngoja tuone mlichokiplan
 
Kongamano la wanataaluma linakutana kutwa nzima ya ijumaa. Je matarajio yako ni nini hasa? Litakuwa kama makongamano mengine yaliyosifiwa kwa kutoa kauli kali na maazimio yenye vipengele hadi vya herufi za kichina? Tutarajie nini tofauti na kwa nini au ndio yaleyale?

Vyovyote vile.. kongamano hili la wanataaluma wetu chini ya mwamvuli wa TPN ninaliunga mkono na kuwapa benefit of the doubt kwamba watawasha moto wa fikra mpya..

Mzalendo Mwanakijiji;

Ndiyo kwanza nimeiona hii thread leo. Bila shaka ni kwa ajili ya pilika pilika nyingi za maandalizi.

Mimi si mtaalamu wa nahau na misamiati, kwa hiyo katika hili sijui Kuunguruma ni nini na Kujiuma Uma ni nini.

Toka mwanzo wa Kongamano, wahiriki na waliokuwa wanafuatilia lilikuwa na dhumuni moja: Kutafuta majibu yanayotekelezeka ni nini Wanataaluma wafanye katika kuchochea maendeleo ya Nchi. Nadhani tofauti inaanzia hapa.

Maazimio yote ni ya Kiutekelezaji zaidi baada ya kupata majibu yake.
 
Ndugu unafikiri mwanataaluma anawezaje kuchangia jamii yake kwa njia ya kujificha kama hii kutumia majina bandia and so on nafikiri kwanza tuanze kwa wanataaluma wenyewe kuwa wawazi , Mimi nilikuwepo kwenye Kongamano it was Nice
 
Hii ni social gathering na ubishoo tu/kutafuta headline kwenye press.

Cynic;

Moja ya mambo yanayoosekana katika nchi yetu ni sauti ya pamoja ya wanataaluma. Tujaribu kuliangalia hili kwa mtazamo chanya. Kongamano hili halikuwa na per diem, wala mfadhili. Kila moja aliyetoka ndani na nje ya nchi na mikoani alijilipia nauli, malazi, gharama zingine na hata adana ya ushiriki kuchangia gharama.

Hakika aliyekuja kwa ajili ya kutafuta headlines au ubishoo kama unavyoita basi atakuwa ana matatizo.

Binafsi sijawahi kuona muitikio wa namna hii, ambao watu wanaacha kazi zao na kuja kujadili masuala muhimu mpaka wanaafikiana.

Hata hivyo, kama una alternative solution ya nini ulitaka kifanyike tutafurahi kukusikiliza pia.
 
Ndugu unafikiri mwanataaluma anawezaje kuchangia jamii yake kwa njia ya kujificha kama hii kutumia majina bandia and so on nafikiri kwanza tuanze kwa wanataaluma wenyewe kuwa wawazi , Mimi nilikuwepo kwenye Kongamano it was Nice


Shy;

Nafarijika sana kama ulikuwapo. Walau unaweza kuwa na maelezo ya ziada kama yangu yamepungua.

Kama ulikuwapo hadi mwisho, baadaye kulikuwa na mikakati ni vipi tutumie mifumo ya habari mawasiliano kuhakikisha kuwa mambo yanatekelezeka.

Tukp pamoja mzalendo.
 
Kutakuwa hakuna jipya...don't hold your breath.

Walau utuambie mawazo yako mbadala ambayo unafikiri yatakuwa na jipya. Tutashukuru kuyafanyia kazi baada ya kupimwa na wanataaluma wenzako kwa muktadha wa kitaaluma kabla ya kukubalika na kuyafanyia kazi kama ilivyokuwa katika Kongamano.
 
Binafsi sitarajii kipya kutoka kwenye hilo Kongamano. Tatizo la Tanzania ni la kisiasa zaidi na siyo la kiuchumi. Nimeangalia mada nyingi naona zimejikita kwenye uchumi zaidi ambako wanaenda kuongeza idadi ya middle class ambao siku zote huwa hawana muda na politics.



Ni hiyo mada ya 6 pekee ndio ambayo naona inaweza kuwa na mwelekeo wa kuleta mabadiliko ambayo tunayahitaji. Lakini je wana ubavu wa kufuatilia na kuhakikisha kwamba kutakuwa na utekelezaji wa maamuzi/maazimio ya hilo Kongamano?

Kwa maoni yangu, pindi tutakapoweza ku-fix tatizo la kisiasa, hayo mengine itakuwa rahisi sana kuya-fix. Kikwete ameishasema kwamba 70% ya wapiga kura wanafuata mkumbo. Ni tusi, lakini ndiyo ukweli kwamba watanzania wengi hatujui tunataka nini na hivyo walio nacho wanatutumia ili waendelee kutuvuna na kupora rasilimali zetu. Hao wana taaluma siku wakija kuamua kupeleka elimu ya uraia vijijini kwa hao 70% ya wapiga kura, hapo ndio nitaona kweli wanataka maendeleo ya kweli.

Kwa mfumo uliopo sasa, hayo yote wanayoya-discuss hayawezi kuisaidia nchi. Ni nani atawekeza mahali ambako hakuna umeme wa uhakika, hakuna barabara nzuri, sheria zipo lakini wasimamiaji wa hizo sheria wanaangalia kwanza nani amekosa, nani apelekwe mahakamani na nani asipelekwe mahakamani. Nani ushahidi wake ukusanywe kwa nguvu zote na nani ushahidi wake uharibiwe. Tukiweza ku-fix tatizo la kisiasa, sheria zitafanya kazi, DPP, IGP na Hosseah wataanza kuwajibika na siyo kufanya kazi kisiasa. Sheria zikianza kufanya kazi hakutakuwa na ufisadi, hela inayoliwa kwa ufisadi itaweza kuwekezwa kwenye vipaumbele vya taifa. Hakutakuwa na mikataba hewa wala uporaji wa rasilimali unaofanywa na wawekezaji mchana kweupe.

Keil; I wish ungekuwepo kuona hali halisi katika Kongamano uliyoyaandika yasingekuwa haya.

Matatizo mengi yaliyokuwapo ni ya kiuwajibikaji na yanweza kufanyiwa kazi kama Wanataaluma kwa uelewa wenu mkikubali kujitoa mhanga na kuyafanyia kazi kuliko kuongea tu.

Hata kama tatizo ni siasa, walau tuambie ni nini kifanyike kwa maoni yako kiutendaji si kinadharia tu ili kubadili mfumo na pia tuambie utatumia rasilimali gani (resources) kubadili mfumo huo.

Mengine yote uliyoongea, tumepata majibu yake na mikakati ya utekelezaji. Nitatuma maazimio yote na mikakati ya utekelezaji yatakapokuwa tayari.
 
Back
Top Bottom