Hili jambo nadhani ni very challenging kuliko tunavyoliona.
Kuna mdahalo ITV waliitisha kati ya TABOA, Madereva, Abiria, na chama cha watetezi wa abiria kuhusu gharama za vyakula njiani.
Changamoto zilikuwa kama ifuatavyo,
* Abiria wenyewe hawakuwa wanaafikiana,abiria wengine walikuwa wanataka hoteli za hadhi na wako tayari kulipia, na abiria wengine walikuwa wanapendekeza gari lisimame kwenye hoteli za hadhi ya chini. Swali likawa ni Je, basi lisimame mara mbili kukidhi matakwa ya abiria wote? Abiria nwengine hawakuridhia kwa kuona ni upotezaji wa muda.
*Madereva wao wakasema wanatafuta hoteli ambayo kimsingi ipo katikati ya safari, ambapo kiuhalisia ni interior sana na hoteli ni chache. Wakaja na hoja kwamba, huwezi kumtoa abiria katika route ya Dar- Babati alafu ukamshusha akale kibaha mjini kwenye mahoteli mengi kwa sababu ya bei.
*Madereva wakaja na hoja nyingine yenye mgogoro kuhusu CHOO. Wakasema serikali inataka abiria wakashushwe sehemu sahihi za kujisaidia, na mara nyingi hizo sehemu unakuta ni za kulipia na abiria hawataki kabisa gharama, kwa hiyo wanachofanya ni kutumia tu busara kutokana na mazingira ili wananchi wajisaidie majoring bila kuwatesa.