Kuuziwa chakula bei juu kwa Wasafiri ni kero kubwa

Kuuziwa chakula bei juu kwa Wasafiri ni kero kubwa

The best option ni kua na vyakula visivyoharibika u can dry food za ngano na kubeba kwenye begi lako njiani unaweza nunua maji ya kunywa tu. ...km ulivyokua unafanaya enzi unasoma boarding.
 
Ile ni biashara kati ya wamiliki wa mahotel na madreva wa mabasi, yaani kila dreva anapopitisha gari hotelini kwanza anakua na posho yake kati ya elfu kumi na kondakta elfu tano lakini pia dreva na wasaidizi wake hula chakula bure tena na vinywaji bure hivo dreva akipitisha abiria mara kumi na tano kwa mwezi anapata mgao wa laki na nusu huku kondakta akipata 75 kwa mwezi, hali hiyo inaenda hadi kwenye vituo vya mafuta pale anapojaza mafuta wanamuhesabia mgao wake kulingana na lita alizojaza kwenye kituo husika hivo dreva ataangalia ananufaika wapi na sio unafuu wa abiria hapo ndio panapozaliwa bei kubwa za kukomoa ili madreva wapate posho zao na wewe abiria uteswe barabara
 
Hili janga ni kama limerejea tena kwa speed ya kasi mnooo fikiria unapokuwa safarini sahani ya wali maharage unanunu kwa 4000, wali nyama. 5000, kuku robo ni 10,000, Chaji ya rangi 1000.

Kuwa msafiri sio kuwa kosa la kulanguliwa vitu bei juu au ndio kusema na wao wameathiriwa na vita vya Ukraine?
😅😅😅😅
 
Zile hoteli mara nyingi zipo Pori , customer ni hao hao wasafiri , na wako limited , operation cost ni kubwa , ili kucover situation inabd bei iwe kubwa mkuu , mana maharage ya kilala, yanachacha wanamwaga , imagine umeyauza Kwa bukubuku
na mwenye hotel anafidia huduma zake muhimu za bure kama choo,siku mikojo na nnya zenu zikijaa mnataka apakulie mikono yake ama
 
Wao wenyewe wanaouza hawanunui kwa hizo Bei
 
Tumia akili.

Sio kila safari mtu anatokea nyumbani.

Safari zingine unatokea mkoani kikazi (mfano Musoma/Rukwa), unarudi zako Dar es Salaam.

Unatoka Musoma/Rukwa saa kumi usiku, unafika Dar 11 alfajiri au kesho yake kabisa
Kama unatoka Musoma saa 10 usiku na unafika Dar saa 11 alfajiri sasa unataka chakula cha nini hapo?
 
na mwenye hotel anafidia huduma zake muhimu za bure kama choo,siku mikojo na nnya zenu zikijaa mnataka apakulie mikono yake ama
Atoze hizo huduma Kama vipi. So wali maharage wa buku ndio nilipe alfu nne so alfu tatu kisa nya ama wewe Ni mdau tumegusa maslahi yako nini
 
Zile hoteli mara nyingi zipo Pori , customer ni hao hao wasafiri , na wako limited , operation cost ni kubwa , ili kucover situation inabd bei iwe kubwa mkuu , mana maharage ya kilala, yanachacha wanamwaga , imagine umeyauza Kwa bukubuku
Operation kubwa kwa vipi? Chakula kinatoka Arusha kwenda Dar kina gharama ya chini ila hapo njiani gharama ni kubwa?

Na kwanini upike maharage kilo 100 wakati unajua mahitaji halisi ni kilo 70? Migahawa ya mjini wanafanya nini wale wa njiani hawafanyi?

Hapo gharama ni kubwa kwasababu hakuna plan B kwa abiria, lazima utanunua tu.
 
Shida ya wabongo tunapenda sana kula safarini, safari fupi tu ya Dar -Moshi/Dodoma/Iringa mtu anataka ale nyama choma kuku/mbuzi.! Wakati unaweza kukausha tu ukafika kwako ukapika ugali maharage ukashiba bila gharama
Safari zinatumia masaa 12.

Nani anaeweza kaa masaa 12 bila kula ilihali akiwa kwake hawezi kaa bila kula?

Sio kila mtu anaweza kukaa njaa siku nzima.
 
Hili janga ni kama limerejea tena kwa speed ya kasi mnooo fikiria unapokuwa safarini sahani ya wali maharage unanunu kwa 4000, wali nyama. 5000, kuku robo ni 10,000, Chaji ya rangi 1000.

Kuwa msafiri sio kuwa kosa la kulanguliwa vitu bei juu au ndio kusema na wao wameathiriwa na vita vya Ukraine?
Msipende kula vibudu mkiwa safarini, jitahidi kula vyakula visivyokuwa na mchuzi au nyama choma kwani huwa hamkawii kumsaidia dereva kuendesha.
 
Hili janga ni kama limerejea tena kwa speed ya kasi mnooo fikiria unapokuwa safarini sahani ya wali maharage unanunu kwa 4000, wali nyama. 5000, kuku robo ni 10,000, Chaji ya rangi 1000.

Kuwa msafiri sio kuwa kosa la kulanguliwa vitu bei juu au ndio kusema na wao wameathiriwa na vita vya Ukraine?
inawezekana hivi vihotel vya barabarani vinamilikiwa na wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi wao. haiwezekani unakuta msikaki wa vipande vitatu tu vidogo unauzwa 1000 kwenye kihoteli kichafu, watu wanakula karibu kabisa na vyoo, serikali za mikoa na wilaya zipo zinaangalia tu.
 
Nunua mkate wako wa Buku jero Na soda ya take away buku Anza safari yako Njiani shindia mkate tu utanishukuru baadae
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]Kweli shida ya nini,
Kama vitu gharama bora ubebe poti lako usisumbue watu Mambo ni mengi
 
Mim nikisafiri daima naandaa chakula nyumban kwisha kazi, nitakaanga hata viazi au kuchemsha hata magimbi ila siwez nunua chipsi unazihesabu vipande 10 sh 3000 nyama haifiki robo sh 5000
 
Tumia akili.

Sio kila safari mtu anatokea nyumbani.

Safari zingine unatokea mkoani kikazi (mfano Musoma/Rukwa), unarudi zako Dar es Salaam.

Unatoka Musoma/Rukwa saa kumi usiku, unafika Dar 11 alfajiri au kesho yake kabisa
na wewe tumia akili, popote unapotokea hapakosi chakula hata cha kununua kwa bei rahisi. Ikiwa tayari haupo tayari kununua chakula cha bei ghali basi tafuta mbadala.
Si lazima ubebe kiporo, kunauzwa biskuti na soda pia navyo ni vyakula.
 
Wakuu,mnafahamu kuwa wenye migahawa/hoteli za barabarani wanalipishwa hela nyingi na madereva na wakati mwingine wenye makampuni ya mabasi,ili mabasi hayo yaingie kwenye hoteli zao?Pia kuwa madereva na wafanyakazi wa mabasi hayo wanakula wanachotaka na kunywa ama maji au soda bure?Na kuwa gharama za kulipia kwa basi kwa siku ili basi liingie, zinafika hata elfu sitini,chini kabisa elfu ishirini?
Hili linasababisha gharama za uendeshaji kuwa juu na hivyo gharama za vyakula kupandishwa ili waweze kuendesha biashara hiyo.
Hii sekta ya huduma za chakula kwa wasafiri serikali haijaitupia macho kabisa,ndio maana iko kienyeji hivi!
Wizara husika,hasa inayohusika na Uchukuzi,isaidie hili jambo.
 
Dawa,beba chakula chako mwenyewe

Case closed

Ova
 
Back
Top Bottom