Wakuu,mnafahamu kuwa wenye migahawa/hoteli za barabarani wanalipishwa hela nyingi na madereva na wakati mwingine wenye makampuni ya mabasi,ili mabasi hayo yaingie kwenye hoteli zao?Pia kuwa madereva na wafanyakazi wa mabasi hayo wanakula wanachotaka na kunywa ama maji au soda bure?Na kuwa gharama za kulipia kwa basi kwa siku ili basi liingie, zinafika hata elfu sitini,chini kabisa elfu ishirini?
Hili linasababisha gharama za uendeshaji kuwa juu na hivyo gharama za vyakula kupandishwa ili waweze kuendesha biashara hiyo.
Hii sekta ya huduma za chakula kwa wasafiri serikali haijaitupia macho kabisa,ndio maana iko kienyeji hivi!
Wizara husika,hasa inayohusika na Uchukuzi,isaidie hili jambo.