Kuuziwa chakula bei juu kwa Wasafiri ni kero kubwa

Kuuziwa chakula bei juu kwa Wasafiri ni kero kubwa

sijawai ona hotel ya hadhi ya juu barabara zote za mkoa ambapo magari husimama kwa ajili ya vyakula ni upigaji tu wa madereva ili wapewe msosi wa bure
Inshu Sio msosi, madereva wanalipwa kati ya sh 15000 hadi 30000 inategemea na hotel.kila akileta abiaria na timu yake Kula bure
 
inawezekana hivi vihotel vya barabarani vinamilikiwa na wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi wao. haiwezekani unakuta msikaki wa vipande vitatu tu vidogo unauzwa 1000 kwenye kihoteli kichafu, watu wanakula karibu kabisa na vyoo, serikali za mikoa na wilaya zipo zinaangalia tu.
Hii inaitwa ''unoko standard''
 
Hii inaitwa ''unoko standard''
wachukue hatua. chakula kinauzwa mazingira machafu kwa bei ghali sawa na hoteli za kitalii huku wataalamu wa afya ya jamii wapo wanalipwa mishahara tu nao wakuu wa mikoa na wilaya wanaona tu hawachukui hatua
 
Mbona hili jambo kila siku linajadiliwa humu, mwisho juzi thread kama hii ilikuwemo humu.

Suluhisho ni moja tu, beba kiporo chako cha ubwabwa na ndondo usafiri nacho kama ukiona humudu gharama za chakula humo barabarani. Uzuri ni kwamba hushurtishwi kununua hicho chakula ni hiari yako.
Hiyo sio solution unadhani kila mmoja akifanya hivyo uchumi wa Nchi itakuwa?? Mamlaka husika zinatakiwa zifanye kazi.
 
Hiyo sio solution unadhani kila mmoja akifanya hivyo uchumi wa Nchi itakuwa?? Mamlaka husika zinatakiwa zifanye kazi.
Ni dunia huru chief. Wewe fikiria uchumi wa nchi acha wenye ukomo wa upeo wafikirie uchumi wa mifuko yao. Na hiyo hasa ndio hadhira lengwa ya comment yangu.
Naamini hata muuza biskuti ni mchangiaji wa uchumi wa nchi pia unless kwa uelewa wako mchangia uchumi ni yule muuza chakula kwenye migahawa ya barabara za mikoani tu.
 
Hili janga ni kama limerejea tena kwa speed ya kasi mnooo fikiria unapokuwa safarini sahani ya wali maharage unanunu kwa 4000, wali nyama. 5000, kuku robo ni 10,000, Chaji ya rangi 1000.

Kuwa msafiri sio kuwa kosa la kulanguliwa vitu bei juu au ndio kusema na wao wameathiriwa na vita vya Ukraine?
Beba msosi wako kutoka nyumbani kwako wa kula safarini.ndiyo njia pekee ya kuwakomoa hawa.

Kule kigoma kuna kitu wanaita "LOWE" .huo ugali unawezakl kukaa hata wiki bila kuharibika
 
Tumia akili.

Sio kila safari mtu anatokea nyumbani.

Safari zingine unatokea mkoani kikazi (mfano Musoma/Rukwa), unarudi zako Dar es Salaam.

Unatoka Musoma/Rukwa saa kumi usiku, unafika Dar 11 alfajiri au kesho yake kabisa
Tumekupata bana kobaaz
 
Tumia akili.

Sio kila safari mtu anatokea nyumbani.

Safari zingine unatokea mkoani kikazi (mfano Musoma/Rukwa), unarudi zako Dar es Salaam.

Unatoka Musoma/Rukwa saa kumi usiku, unafika Dar 11 alfajiri au kesho yake kabisa
Mtandikiwe tu pia mikeka hadharani mswali kuwaringishia watu nyinyi ni watu wa dini
 
Kuna kahotel tulisimama ,kuna vichips vinauzwa elf 5,kwa mie niliezoea sembe ni Tonge moja namaliza vyote!..
 
Hili janga ni kama limerejea tena kwa speed ya kasi mnooo fikiria unapokuwa safarini sahani ya wali maharage unanunu kwa 4000, wali nyama. 5000, kuku robo ni 10,000, Chaji ya rangi 1000.

Kuwa msafiri sio kuwa kosa la kulanguliwa vitu bei juu au ndio kusema na wao wameathiriwa na vita vya Ukraine?
Watu waache ubuge safarini wawe na nidhamu
 
Tumia akili.

Sio kila safari mtu anatokea nyumbani.

Safari zingine unatokea mkoani kikazi (mfano Musoma/Rukwa), unarudi zako Dar es Salaam.

Unatoka Musoma/Rukwa saa kumi usiku, unafika Dar 11 alfajiri au kesho yake kabisa
vitu vimepanda bei kama ni hivyo msilalamike kuleni au mfunge, mbona kwa pisi huwa mnatuma ya safari nayakutolea hamulalamiki
 
Unasafiri 'kikazi' na ulalamikie 5000 ya chakula, wewe ni FUTUHI tu.
kweli wabongo watu waajabu kabisa hao ndo sawa na wale wakuagiza chakula cha elf10 lakini safarini anaona taabu kulipia choo cha mia mbili yuko radhi kukaa na mafi hadi mwisho wa safari aingie choo cha bure
 
Shida ya wabongo tunapenda sana kula safarini, safari fupi tu ya Dar -Moshi/Dodoma/Iringa mtu anataka ale nyama choma kuku/mbuzi.! Wakati unaweza kukausha tu ukafika kwako ukapika ugali maharage ukashiba bila gharama
Waambie hao
 
Ujue sio lazima safarini ule ule cuz hakuna kazi ngumu unayoifanya inayokuhitaji kula. Mimi nikiwa safarini nanunuaga biskuti aidha Digestive au Roman Creams gari itakaposimama nanunua soda tu mpaka nafika ninakoenda na biskuti zinabaki. Kuna faida kusafiri hivi najiepusha na matatizo ya tumbo na kunya kunya hovyo.
Ila mi naona hawa jamaa tunawaendekeza sie wenyewe abiria, tukiamua kuwalia buyu akili zitawakaa sawa tu mbona.
 
Kwani mnalazimishwa,mwambie mkeo akupakilie kiporo
 
Mtoa mada acha kulalamika do something.
Nunua chupa ya chai na hotpot saizi ndogo. Unaposafiri Safari ndefu say Dar/Mza. Weka chai kwa flaski, tupia wali wa Jana mu hotpot, wengine wakienda kulanguliwa hoteling, wewe kula wali wako na chai.
Nakumbuka enzi za OTC /DMT mama alikua anabeba vyakula Kama kuku wa kukaanga na chai mu flaski
 
Back
Top Bottom