MASSANDA OMTIMA
Senior Member
- Mar 22, 2017
- 159
- 47
Hebu nambie rafiki, mtu anakupigia simu na katikati ya mazungumzo anakuuliza 'ni saa ngapi sasa hivi ili tuone muda mzuri wa kukutana'? Unafanyaje? Tuseme, simu yako imepotea / imeharibika au imeishiwa moto, unafanyaje?Chukulia una simu ya screen touch, ambayo ili ifanye kazi, unahitaji kuianzisha; na muda wa kuianzisha ni mrefu na wa usumbufu kuliko ule wa kuangalia saa. Je huoni kama hali hii hiyo ni upotezaji wa muda?
Aidha, saa ni mwajiri mkubwa sana kuanzia viwanda vyenyewe, wauzaji na wale wanaozitengeneza zinapoharibika (repairers). Je, hawa waajiriwa wote wataenda wapi iwapo watu wataacha kuvaa saa kwa kujifanya kwamba wao ni wa kisasa na wale wenye kuzivaa ni washamba?
Kila kitu kina nafasi yake katika maisha. Wala si haki kusema uvaaji saa ni ushamba (nami ni mvaa saa mkongwe)! Aidha kuna saa ambazo, kuzinunua, kunahitaji mahesabu makali!
Jitafakari!