Kuvaa saa enzi hizi za dijitali ni mbwembwe au usharobaro?

Kuvaa saa enzi hizi za dijitali ni mbwembwe au usharobaro?

Mimi napenda xana kuvaa saa ata ikitokea betri imeisha gafla navaa hivyohvyo ni mazoea tu ya mtu anaejali muda
 
TIME is MONEY
Tumwelimishe mtoa mada,ametoa mawazo yake yanayofanana na kichwa chake.this is Folish age,akikua atajua umuhimu wa kuvaa saa.
Mkuu hapo kwenye red siku hizi tunasema TIME is LIFE
coz muda ndio uhai na huwezi kufananisha thamani ya Muda "Uhai" na Pesa.
Tuheshimu sana muda kwani ikipita hata dakika moja basi haitorudi tena!

Hope umenielewa.
 
View attachment 189231
Mimi nashindwa kuelewa kabisa watu (hasa wanaume) wanaovaa saa enzi hizi za dijitali kama wanafanya hivyo kwa makusudi au ni mbwembwe tu. Kwanini nasema hivyo? Siku hizi yapata 98% ya watanzania wote wanamiliki simu na kwenye simu kuna saa.

Utamkuta mwanamume sharobaro anamiliki simu 3 kwa mpigo na wakati huo huo katupia bonge ya saa kiganjani mwake. Kuvaa saa kwa wanawake inaleta maana kidogo kwa kuwa inachukua nafsi ya bangili &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; ni pambo la kike.

Sikumbuki mara ya mwisho kuvaa saa na sitegemei kuivaa tena labda nikiwa kwenye chumba cha mtihani nitaibeba na kwenda nayo na baada ya kumaliza kupiga paper nitampa demu wangu avae kama bangili. Uvaaji wa saa enzi hizi unawafaa zaidi wanafunzi wa shule za msingi kwa kuwa wengi wao hawamiliki simu. Tujifunze kuishi kulingana na wakati.

:israel:
Hivi ni kwa jinsi uonavyo wewe,kwa mimi saa navaa kwakuwa inanipendeza na ninakuwa huru zaidi,kuangalia saa kwa simu na wakati mwingine kwa saa ya mkononi yote naona poa na inanifanya najiamini zaidi.
 
Wakuu, soma ukurasa wa mbele gazeti la mwananchi leo ijumaa mpate utafiti zaidi kuhusu validity ya hii hoja yangu, msiwe wabishi tu pasipo kufanya utafiti.
 
Watu waliona mbali sana, kutengeneza Simu za Digital ili uweze kumaliza kila kitu ndani ya simu yako, on a soko la Internet Cafe lilivyokufa kifo cha Mende, hakuna haja ya kuvaa SAA kwa kipindi hiki, kwa kuliona hilo kwa sasa hata watengeneza SAA wanaumiza kichwa ili kurudisha hadhi ya SAA mkononi, kwa upande wangu Mimi naona ni mzigo tu, kama kuvaa miwani, mwingine kwake ni pambo lakini mwingine anavalia shida tu kwa ajili ya kuona

Hivyo basi, kuwa na simu tatu mkononi, na bado una SAA mkononi kwangu naona shida tu
 
Hahahhha nacheka kwa dharau hapa nimevaa saa na ninazo 5 zingine chumbani
 
Saa itabaki na nafasi yake tu, ukiiangalia hapohapo unajua muda coz ipo mkononi simu nyingine mpaka ubofye, au uitoe mfukoni, au ukute imezima charge....saa ipo on muda wote haina ishu za kuisha charge wala nini.
 
Mimi huwa nasahau kama kuna kitu simu. Kwa watu wa umri wangu simu kwetu ni by the way wala haiwezi kunifanya nikaacha kuvaa saa. Simu ni kwa vijana sana sana. Bila saa mimi najiona nimepungukiwa kitu kwenye mavazi huwa inabidi nirudi nyumbani hata kama nimekwenda km. 1 itabidi nirudie saa yangu. Yaani niwe nafungua mkoba kila dakika kuangalia saa? Mkono umebeba nini? Angalia watu mashuhuri wote nani anatembea na simu mkononi lakini nani anakuwa hana saa mkononi?
 
Washamba sana wanaovaa saa. Wengi wao saa zao hata majira hazina. Ukitaka kuamini msimamishe muulize tu muda. Utasikia anajichekesha halafu anakujibu eti hili ni kopo nimevaa tu. Ulimbukeni.
 
Pamoja sana mkuu Ighombe, I appreciate your support and positive thinking towards wrist watches (ornaments). Ngoja wale wanaonipinga waje tusikie wanasemaje kwa wazo lako hili.
Asante. Hata mafundi saa waliokuwa wanakodelea misaa macho siku hizi hawapo. Kama unabisha mpeleke mwanao chuo veta akasomee ufundi saa uone kama hata wakufunzi wapo.
 
Washamba sana wanaovaa saa. Wengi wao saa zao hata majira hazina. Ukitaka kuamini msimamishe muulize tu muda. Utasikia anajichekesha halafu anakujibu eti hili ni kopo nimevaa tu. Ulimbukeni.
Neno "washamba" kwa akili yako unalitafsiri vipi?

Mimi natafsiri kua "ushamba" ni kushangaa jambo ambalo wenzako wanaliona ni la kawaida tu,

So kwa tafsiri hii nadhani wewe ndio Mshamba.
 
Back
Top Bottom