Kuvaa suruali zilizochanika chanika (masempele) ni kufilisika kifikra na kimtazamo

Kuvaa suruali zilizochanika chanika (masempele) ni kufilisika kifikra na kimtazamo

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2016
Posts
8,658
Reaction score
15,793
Jana nimemuona kijana mmoja ninayemuheshimu akiwa amevaa suruali iliyochanika chanika kwenye magoti nikasikitika sana.

Nikajikuta najisemea kuwa huyu naye kafirisika kimtazamo?

Sasa nimejua ni kwanini ni rahisi ku control minds za Mbongo. Wabongo ni watu wa 'wengi wape'. Yani kile kinachofanywa na wengi ndio kinaonekana kuwa sawa. Sasa jamani, mtu na heshima zako unaanzaje kuvaa suruali zilizotoboka toboka kwenye magoti? Hii ni akili au matope?

05422a4d404715316873acfdfe96d537--ripped-jeans-men-mens-jeans.jpg
 
Jana nimemuona kijana mmoja ninayemuheshimu akiwa amevaa suruali iliyochanika chanika kwenye magoti nikasikitika sana.
Nikajikuta najisemea kuwa huyu naye kafilisika kimtazamo?

Sasa nimejua ni kwanini ni rahisi ku control minds za Mbongo! Wabongo ni watu wa 'wengi wape'...
Yani kile kinachofanywa na wengi ndio kinaonekana kuwa sawa...
Sasa jamani, mtu na heshima zako unaanzaje kuvaa suruali zilizotoboka toboka kwenye magoti? Hii ni akili au matope?

05422a4d404715316873acfdfe96d537--ripped-jeans-men-mens-jeans.jpg

Mbona we unavaa shati lina mistari mistari, ...hizo ni fashion tu ndugu
 
Huenda bado unaishi kwenye pango ama una umri mdogo,staili ya kuchana suruali ilikuwepo tokea miaka ya 70,tena sio bongo tu,worldwide.Mie siwezi kuvaa nguo ilochanika lakini wanaovaa wana uhuru wa kufanya hivyo so we achana nao fanya yako.
 
Jana nimemuona kijana mmoja ninayemuheshimu akiwa amevaa suruali iliyochanika chanika kwenye magoti nikasikitika sana.
Nikajikuta najisemea kuwa huyu naye kafilisika kimtazamo?

Sasa nimejua ni kwanini ni rahisi ku control minds za Mbongo! Wabongo ni watu wa 'wengi wape'...
Yani kile kinachofanywa na wengi ndio kinaonekana kuwa sawa...
Sasa jamani, mtu na heshima zako unaanzaje kuvaa suruali zilizotoboka toboka kwenye magoti? Hii ni akili au matope?

05422a4d404715316873acfdfe96d537--ripped-jeans-men-mens-jeans.jpg
cc: Babu Tale
Diamond
Ally Kiba
wasanii wote feki wa bongo fleva.
 
Mob psychology plus technological pace inaharibu kizazi cha sasa.
Tunawakati mgumu wakujizuia kufanya mambo ya kijinga.

mafisadi hayana chama
 
Kwani haya mambo wanafanya wabongo tu?

Nakumbuka miaka ya tisini mwanzoni Komandoo Salmin Amour alipokuwa rais wa Zanzibar alisema sana hili TVZ.

Ujinga ni kum judge mtu kwa mavazi.

Ndipo hapo jambazi atakapokuja na suti ya Savile Row na utamuita "huyu mwanamme kweli" atakusainisha mikataba mibovu na kukuibia mamilioni ya dola.

Wakati wewe unafukuzana na waliovaa Jeans za kuchanika.

Unavyowasakama kwa jambo lisilo la msingi ndivyo unawapa umuhimu.

Kama hutaki mtu mwenye jeans hizi aje kwako kavaa hivyo weka bango.

Lakini kuanza kupangiana nguo za kuvaa ni ujinga.

Na mini naandika hivi si mshabiki wa jeans hizi na sijawahi kuvaa hata siku moja.

Ila natetea haki zao kuvaa wanavyotaka bila kubughudhiwa kama mimi nisivyotaka kubughudhiwa nikipiga golden French cuffs zangu on Brunello Cuccinelli.

Sent from my Kimulimuli
 
Back
Top Bottom