Kuvaa suruali zilizochanika chanika (masempele) ni kufilisika kifikra na kimtazamo

Kuvaa suruali zilizochanika chanika (masempele) ni kufilisika kifikra na kimtazamo

Kwani haya mambo wanafanya wabongo tu?

Nakumbuka miaka ya tisini mwanzoni Komandoo Salmin Amour alipokuwa rais wa Zanzibar alisema sana hili TVZ.

Ujinga ni kum judge mtu kwa mavazi.

Ndipo hapo jambazi atakapokuja na suti ya Savile Row na utamuita "huyu mwanamme kweli" atakusainisha mikataba mibovu na kukuibia mamilioni ya dola.

Wakati wewe unafukuzana na waliovaa Jeans za kuchanika.

Unavyowasakama kwa jambo lisilo la msingi ndivyo unawapa umuhimu.

Kama hutaki mtu mwenye jeans hizi aje kwako kavaa hivyo weka bango.

Lakini kuanza kupangiana nguo za kuvaa ni ujinga.

Na mini naandika hivi si mshabiki wa jeans hizi na sijawahi kuvaa hata siku moja.

Ila natetea haki zao kuvaa wanavyotaka bila kubughudhiwa kama mimi nisivyotaka kubughudhiwa nikipiga golden French cuffs zangu on Brunello Cuccinelli.

Sent from my Kimulimuli

Karibu tena Kiranga
 
Napenda sana suruali za vitambaa hizo jeans waendelee kuvaa vijana wenzangu tu mi siziwezi.
 
Ni fashion tu, mwanzo walikuwa wanaonyesha makalio sasa wameamua kuongezea matobo kwenye mapaja na magoti. Baada ya muda watakuwa hawafungi zip. Uzuri sheria za nchi hazijasema kama hili ni kosa. Tuwaache waendelee na fashion zao mkuu.....
 
Sijawai nunua Jeans aina yeyote tangu nijitambue, kila mtu ana Uhuru wa kuvaa,mi huwa wananishangaa kutovaa jeans ! Live your life dude

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nguo walizokuwa wakivaa vichaa zamani ndio watu wenye akili zao wanavaa hivi sasa.
Nguo wanazovaaa wanawake ndio wanaume wanavaa pia (za kubana)
 
  • Thanks
Reactions: nao
Sijawahi kujutia kupigilia misumari ya ton jeans
1569d7bc30f0bbf752eb0f485c9c97f7--dope-style-guy-style.jpg
 
Kuna baadhi ya watu hawajielewi kabisa hata kama ni fasheni
 
Kajifunze kuandika kwanza kabla hujaivaa

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
Ukisha vaa hivyo unakuwa na swagar kama hizo...

Pole sana mkuu naona uzee unakunyima mengi...
 
Endelea kupangia watu maisha yao ukikua utaacha

Sent using Jamii Forums mobile app

Watu wenye matumizi hafifu ya akili zao wanahitaji msaada,mtoa mada na wachangiaji wa awali wametoa msaada unaohitajika.Inawezekana wewe pia unavaa nguo zinazoonyesha hadharani unayotakiwa kuoyesha sirini.Unahitaji msaada,mchango unathibitisha hivyo.
 
Watu wenye matumizi hafifu ya akili zao wanahitaji msaada,mtoa mada na wachangiaji wa awali wametoa msaada unaohitajika.Inawezekana wewe pia unavaa nguo zinazoonyesha hadharani unayotakiwa kuoyesha sirini.Unahitaji msaada,mchango unathibitisha hivyo.
[emoji57]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi huwa sielewi kabisaaa kwanini wanavaa hivo

Ukweli nimambo ya ajabu...nasipendi kuona hilo jambo kabisa.. Unless huyo mtu ni kichaa na hajitambuwi

AU Maskini hakiwezi.
 
Mimi kuna kitu sijaelewa...mtu asiyekuhusu kuvaa hivyo we unakereka vipi?
 
Kesho ntavaa yenye matobo kama hiyo

Sent from my Priceless H40-D00 using JamiiForums mobile app
 
Maisha ya ujana ni nusu ya uwendawazimu......

Akili ya ujana ni kutaka kufanya kila ambacho kinampendeza nafsini mwake......

Nyakati za ujana matumizi ya hisia yanakuwa juu kuliko matumizi ya akili.......

Hisia zinapotawala akili ndipo mtu huenenda na kutenda kama mwendawazimu.........

Kadri miaka inavyoenda ndivyo fahamu zinaporejea na kuanza kujishangaa wewe mwenyewe.........

Mtu mwenye akili timamu hawezi kuvaa nguo iliyochanika.....mara nyingi wanavaaga watu wenye matatizo ya akili......
 
Back
Top Bottom