Kuvunjika kwa ndoa siyo sawa, Jamii inapaswa kubadilika

Kuvunjika kwa ndoa siyo sawa, Jamii inapaswa kubadilika

Me naona point inayotaka kusemwa ni kuwa kama shida zipo kokote kwanini usiwe mtu wa kutafuta suluhu ya mambo badala ya kukimbia kila unapokuta shida. Utakimbia mangap na yote yanashida zake
Kwa nini nioe ? Faida ya mimi kuoa ni ipi ? Je kama nilishajaribu kuoa nikaachana na nikapima kukaa mwenyewe ni bora kuliko kuishi na mtu , mimi naona kuoa ni uamuzi tu unaweza kuacha tu wala hakuna tatizo.
 
Mkuuu sjui umejuaje me nipo kwenye wakati mgumu muda wote nawaza hata nipate kibarua .hata nje ya mkoa nikae hata mwaka mzima nimechoka .mwanamke hapendi kabisaa tuwe na amani .Kwa mwezi mzima tnaweza ongea labda siku2 .tunawasikiana Kwa sms tu .hapo natakiwa nifanyeje ?
Just a season.itapita. kama ni mtu wa imani, jitahid kujiweka karibu na mwenyezi Mungu seasons kama hizi for guidance. It wont last
 
Sijakasirika unataka kuntuhumu na kunlisha maneno
Sipo hivyo mkuu, ila kwa nini huwa mnawachukia sana kataa ndoa??[emoji16][emoji16]

Mbona kuoa nakuto kuoa ni maamuzi tu mkuu? Kwan kama wewe umeoa au utakuja kuoa kataa ndoa wanakuathiri vip mkuu?
 
Kwa nini nioe ? Faida ya mimi kuoa ni ipi ? Je kama nilishajaribu kuoa nikaachana na nikapima kukaa mwenyewe ni bora kuliko kuishi na mtu , mimi naona kuoa ni uamuzi tu unaweza kuacha tu wala hakuna tatizo.
Sema mambo kwa sasa yamekua complicated sana aisee. Rengo la ndoa haswa linapotea kabisa.
 
Sema mambo kwa sasa yamekua complicated sana aisee. Rengo la ndoa haswa linapotea kabisa.
Mimi ndio maana huwa nashauri kama nikuoa oa ukiwa huna chochote ,ukisema ujipate ndio uoe lazima uangukie pua , ukiwa na uchumi mzuri macho hayawezi kuona mke ila ukiwa hauna kitu macho yanaona wife material wakutosha.
 
Kukimbia tatizo sio njia ya kupata suluhu.
Muhimu ni kuangalia namna gani unasolve tatizo.

USHAURI
Kumbuka mwanaume akiudhiwa hutafuta mahali atulie atafakari tatizo ni nini ndio arudi kulitatua. Ila kwa mwanamke sio hivyo, mwanamke akiudhiwa hutaka lawama zake zote zisikiwe na mtu mwingine awe ni rafiki yake, mume wake, mzazi wake ndugu yake yoyote yule, akishazisema tuu ndio hasira hupungua.

1. Mchunguze mke/mchumba wako anataka nini hasa, kisha jaribu kumtimizia kadili ya uwezo wako, najua katika hayo malalamiko kuna vitu anasema vitimizwe na wew hautimizi ndio mana anaishia kununa kwa sababu hajatimiziwa, kama wewe unapokua na mahitaji labda anakutimizia jaribu na wew kumtimizia kadili ya uwezo wako.

2. Kutokana na utalam ulioandikwa kwenye vitabu vya watalam ni kwamba mwanamke ni mtu ambae ana tabia ya kupenda kusikilizwa anapokua anatoa tatizo, pale unapoacha kumsikiliza yeye anatafsiri kuwa humpendi. Hivyo jitahidi anapokuwa anatoa malalamiko kaa tulia msikilize na msapoti kabisa katika point anazosema
ANGALIZO
Anapokua anatoa malalamiko usianze kujitetea kwa kuonyesha anachosema sio kweli, mfano analaumu kwamba kwanini haumsikilizi wewe unamkatisha unasema "hunioni nimekaa apa nakusikiliza".
Wew tulia msikilize akimaliza jaribu kutatua shida zote alizokwambia kadili ya uwezo wako, kama ni shida kubwa kukuzidi mwambie kwa hilo hutaweza kwa muda huo labda mpaka siku nyingine.

3. Kuna mahala pengine mwanamke anaweza akawa amekerekwa na mtu mwingine kabisa tofauti na wew kabisa, ila akiwa mbele yako anataka kukutolea hasira wewe, na hapo sio kwamba atasema alivoudhiwa huko alikotoka ila atasema ambayo yanakuhusu wewe. Ikifikia hapa kazi yako mwanume inakuwa moja tuu. KUSIKILIZA. Mpe nafasi ya kutoa hasira zake akimaliza utaona anatulia, akirudi katika hali yake ya kawaida hata sho unapata fresh tuu.
Mkuu umemaliza kila kitu
 
Ulishawahi sikia malalamiko ya waliopo single kuhusu ndoa humu jukwaani?
Ndugu nimesikia unasema "kwanini utafute shida kwenye ndoa"


Lakini sisi tunaongelea uhalisia wa maisha ya binadamu kwamba kuna raha alafu kuna shida na hakuna anaye penda majanga au kama unavyosema kwamba huwenda "ametafuta huyu shida" hapana ila ni sehemu tu ya mzunguko wa maisha



Siamini kama kuna mtu mwenye IQ kubwa anaweza kupoteza mda wake kujitengenezea shida kwa makusudi ila wale wenye uelewa mdogo na IQ hufanya hivyo


Lakini mtu anayejitambua anajua kwambaanahitaji ndoa anaitaji mke anaitaji mtoto na anaitaji pesa wala hatazamii kutafuta shida kwenye ndoa ila kama ilivyo kawaida mtu hawezi kukosa upele au hata kidonda cha bahati mbaya basi ndivyo maisha yalivyo
 
Hatna ndoa lakni tmezaa watoto wawili
My big brother,

Kumbe bado ujaowa basi hakuna sehemu nyeti unayotakiwa kuiangalia kwa kina kama kumjua yule unayemuowa je, anaendana na wewe aijalishi labda umezaa naye lakini nakushauri hakikisha unaye oana naye mnaendana vizuri

Usipo zingatia kigezo hiki basi utapitia shida za juu sana na mateso kwa mda mrefu kwahiyo nakushauri mchunguze huyo mwanamke kama unaendana naye siumesema sijui hamuelewani basi jaribu kutafuta solution ukiona aeleweki wala habadiriki sijui hakueshimu huyo kwa hakika aendani na wewe siyo nyota yako
 
Back
Top Bottom