Sirdick Mashally
Member
- Aug 15, 2022
- 7
- 3
Kumbukumbu zikinijia nakumbuka siku ile ilikuwa ni siku ya furaha sana kwangu na kwa familia kwa pamoja. Siku ambayo dada yangu aliolewa, kila mwana familia na ndugu tulikuwa kwenye furaha isiyokifani, tulisherehekea kana kwamba hakukuwahi kutokea wala hapatatokea tena harusi kwenye ukoo wetu.
Furaha ilikuwa ni kubwa kwa upande wa familia kwa sababu ilikuwa ni heshima ya namna yake kwa wazazi wetu kuozesha binti yao. Pia haikuwa rahisi kuifanikisha ndoa kutokana na kupoteza matumaini juu ya dada yangu baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu, kama miaka minne toka amalize kidato cha nne mwaka 2013. Ndani ya hiyo miaka minne dada yangu hakufanikiwa kupata kazi rasmi ya kufanya, alijaribu kujifunza cherehani lakini mambo hayakuwa mazuri kwahiyo muda mwingi alibaki kuhudumu kazi za nyumbani tu.
Jinsi hali ilivyokuwa ilimnyima amani na kumkosesha furaha na kujihisi hana bahati lakini Mwenyezi Mungu ni mwema alijaalia 2017 akapata mchumba na kufunga nae ndoa.
Baada ya shughuli ya harusi kukamilika dada pamoja na shemeji ambaye ndio mume wake walisafiri kutoka Tabora kueleke Kigoma ambako ndio kwao na shemeji na ndiko alikokuwa anafanya kazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa linalishughulikia masuala ya wakimbizi (UNHCR).
Kwa ujumla hali ya maisha yao ilikuwa ni nzuri hasa kiuchumi lakini baada ya mwaka mmoja kupita tangu wafunge ndoa kuliibuka changamoto ya kukosa mtoto hali iliyopelekea kuanza kuibuka kwa vurugu ndogo ndogo ndani ya ndoa na kila mmoja kumshutumu mwenzie kuwa yeye ndio kikwazo.
Hali iliendelea na kufikia kuwa mbaya zaidi, hapo ni baada ya kuwa miaka miwili imepita sasa na hali kuwa mbaya zaidi ilichagizwa na upande wa mume hasa mama mkwe kutamtaka mwanae ampe talaka mkewe na aoe mwanamke mwingine na kumtolea kashfa mkwewe. Dada alijitaidi kuvumilia huku akitafuta ufumbuzi lakini ulifika wakati akabidi aombe tu ridhaa kwa wazazi wamkubalie arejea tu nyumbani maana ndoa kwa upande wake imekuwa ngumu. Lakini sasa mume wake hakuwa tayari waachane ila msisitizo kutoka kwa mama yake ulikuwa ni mkubwa sana kuwa waachane.
Wakati utaratibu wa kuivunja ndoa ukifatiliwa, shemeji alisimamishwa kazi kutokana na ufanisi wa kazi kushuka na kuambiwa kuambiwa atapewa taarifa baadae ya kurejea. Suala hili lilizidi kuchochea mambo kuwa mabaya zaidi.
Baada ya muda kupita kidogo, mama wa mume alitumia nafasi ya kuwa yeye ni mzazi kumlazimisha mwanae kutoa taraka kwa mke wake na kumwambia mwanae “leo nimeenda kwa mganga kaniambia nyota yako na ya mke wako haziendani ndio maana hampati watoto na kazi umeachishwa” alisema maneno hayo mbele ya mkwewe.Haikuishia hapo bali alimwambia mwanae akishindwa kutoa taraka asimjue yeye kama mama yake.
Basi hakukuwa na namna shemeji alibidi atii maagizo kutoka kwa mama yake na kutoa talaka kumuacha mke wake. Dada baada ya kupokea taraka aliomba apate siku chache kidogo ili ajiandae na safari kurudi nyumbani. Cha ajabu siku akiwa anafua nguo zake kujiandaa na safari, alianguka na kuzimia baadae anajikuta hospitali na kuambiwa kuwa yeye ni mjamzito.
Baada ya kurejea kwake alimuuleza aliyekuwa mume wake hizo taarifa na shemeji kumuomba asiondoke kwanza ili wailee mimba pamoja. Pia baada ya mama wa mume wake kupata hizo taarifa na yeye alishauri pia asiondoke.
Miezi tisa ilipofika alijifungua salama mtoto wa kike lakini mara tu baada ya kujifungua na kukaa kama wiki mbili mama mkwe wake alimtaka aondoke na amuache mtoto huku akiendelea kushikilia imani zake kuwa dada si mke mwema kwa mwanae. Dada hakukubali kumuacha mwanae pale na yeye kurudi nyumbani. Lakini sasa baadae mtoto aliibiwa na mtu asiyejulikana ingawa imani ya dada ilikuwa kwa mama mkwe wake ndio kamuiba mtoto wake na alienda mahakamani kufungua kesi lakini alishindwa kutokana na kukosa ushaidi.
Dada ilibidi arudi nyumbani ila hali yake kiafya (mwili na akili) haikuwa nzuri kabisa na ilimchukua takribani mwaka moja kukaa sawa lakini sio sawa kabisa maana kila wakati yeye ni kulia tu.
Baada ya miaka miwili na nusu kupita aliyekuwa shemeji anampigia simu dada na kuomba aende Kigoma kumuona mwanae. Habari hiyo ilimshtua sana dada na kumpa hamu ya kumona mwanae kwahiyo alibidi afunge safari na pamoja na mimi mpaka Kigoma.
Tulivyofika tulionana na aliyekuwa shemeji akiwa pekee yake na kutuambia ukweli wote kuwa mama yake ndiye aliyemuiba mtoto, kwa kipindi hicho mama yake alikuwa ameshafariki kama miezi minne nyuma. Bhasi tukaongozana mpaka nyumbani kwa aliyekuwa shemeji na tulivyofika nje kabla hata kuingia ndani tulikumta mtoto akiwa nje kibarani akicheza na wenzie na baada ya kumuona baba yake alimfata huku akiita baba lakini hiyo baba haisikiki vizuri kabisa.
Dada baada ya kumuona mwanae alilia sana kwa uchungu na kufikia hadi kupoteza fahamu, ilikuwa ni kama ametonyeshwa kidonda.
Tulivyokaa na mtoto kwa muda tuligundua athari mbali mbali zikiwemo.
Kudumaa kwa mtoto kimwili na kiakili yaani mwili ulikuwa ni dhaifu sana( umri na uzito wake haviendani kabisa).
Kiwango chake cha kujifunza na kutambua mambo mbalimbali kilikuwa chini sana, kwa mfano ilikuwa nikimtuma aendee kikombe yeye analeta hata ndoo ya maji isiyo na maji, ukimfunza kutamka neno fulani inakuwa ni ngumu sana kulitamka.
Pia wakati tupo pale mtoto alikuwa anaumwa mara kwa mara kwahiyo huduma za matibabu zilikuwa ni gharama kubwa isitoshe baba yake alikuwa bado hajarudishwa kazini kwahiyo alikuwa anajishughilisha tu na biashara ndogo ndogo.
Kiufupi mtoto hakuwa na afya ya akili wala mwili na tulivyoenda hospitali tukaambiwa shida ni mtoto hakupata maziwa ya mama yake.
Daktari aliendelea kutueleza kuwa kuna umuhimu mkubwa sana tena sana kwa mtoto kupata maziwa ya mama yake (kunyonya maziwa ya mama yake kwa si chini ya miaka miwili) na miongoni mwa faida hizo alituelezea pia.
Kunyonyesha ni moja ya njia sahihi ya kuhakikisha mtoto anakuwa na afya njema na kupunguza uwezokana wa vifo kwa watoto wachanga.
Kunyonyesha humsaidia mtoto kumkinga na maambukizi ayapatayo akiwa mchhanga.
Maziwa ya mama pia ni chanzo muhimu cha nguvu na virutubisho kwa watoto.
Kunyonyesha kunamsaidia mtoto katika uwezo wake wa utambuzi wa akili.
Baada ya kutoka hospitali tulikaa kwa siku chache na baadae tulirejea nyumbani Tabora kujadiliana na wazazi namna ya kufanya ila tulimuacha mtoto na baba yake maana ndio mtu aliyekuwa kamzoea.
Mwisho
Chanzo cha picha ni
https:// unsplash.com
https://www. Gettyimage .com

Attachments
-
gift-habeshaw-ACse-ieowwE-unsplash.jpg4.3 MB · Views: 32
-
mustafa-omar-tEz8JU1j-00-unsplash.jpg768 KB · Views: 45
-
seven-shooter-ZzE9uKOAchc-unsplash.jpg2.6 MB · Views: 29
-
seven-shooter-ZzE9uKOAchc-unsplash.jpg2.6 MB · Views: 40
-
mustafa-omar-tEz8JU1j-00-unsplash.jpg768 KB · Views: 40
-
gift-habeshaw-ACse-ieowwE-unsplash.jpg4.3 MB · Views: 38
Upvote
0