Kuwa makini na haya makundi, muda wowote yanaweza kukuumiza

Kuwa makini na haya makundi, muda wowote yanaweza kukuumiza

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Makundi makuu matatu, yanayoweza kukuumiza kwa kiwango kikubwa wakati wowote bila wewe kutarajia/kutegemea:-

Marafiki wako wa karibu
Hawa wakiamua kukuumiza, watakuumiza kweli;kwa sababu wanajua uimara wako pamoja na udhaifu ulionao.
Wanaweza hata kuharibu familia yako kwa kutembea na mpeni wako.

Wafanyakazi wenzako
Hawa wako tayari kukufitini au kukuzunguka, ili uonekane mbaya kwa bosi wako, na wao waonekane wazuri. Wengi ni wasaka fursa.

Ndugu zako
Hawa wanaweza kuwa, mliozaliwa tumbo moja, mashangai, wajomba n.k
Ni wachache sana, ambao hufurahi inapotokea ndugu yao anapiga hatua; wengi huwa wana ile roho ya kwanini.
Wanaweza kutumia njia zozote zile, uweze kuporomoka.

Muhimu, ni kuwa makini na haya makundi; usiyategemee sana, katika harakati zako; kama umeolewa/umeoa na una watoto; pambana na hiyo familia yako, hawa wengine ni wakulungwa tu.​
 
Back
Top Bottom