Kuwa makini sana na ndugu yako wa damu hasa yule ambaye mmeshibana

Kuwa makini sana na ndugu yako wa damu hasa yule ambaye mmeshibana

Sijui wewe ni dini gani lakini nitakuelezea kwa kiislamu

Kijicho ni madhara yatokanayo na mshangao wa furaha usioambatana na kumtukuza mola (kumtukuza huko aghalabu ni kusema maashaallaah). Hii maana ya kijicho siyo rasmi ukisoma vitabu utapata maana nzuri iliyotulia. Tofauti ya kijicho na uchawi ni kwamba uchawi mtu anakusudia kudhuru lakini kijicho mtu hakusudii kudhuru inatokea automatically

Tuchukulie mfano mwanamke umemtembelea dada yako aliyejifungua, baada ya kuona mtoto ukasema "dada yangu umezaa katoto kazuri sana, umetuheshimisha hatimaye nakwenda kuitwa odo, na blah blah nyingi kama tunavyojua tena wanawake. Hapo ni rahisi kitoto au mama kudhurika na kijicho. Kijicho ni jambo la kiasili linakuwa ndani ya mtu na hapa nataka niweke bayana tu kuhusu wale waganga njaa wanaodanganya na kuibia watu eti wanatibu kijicho. Dawa ni mbili tu au tatu kwenye maswala ya kijicho

Kwanza ni kuambatisha neno Maashaallaah kwenye kushangazwa kwetu na furaha zetu mfano huyo mtu hapo juu angesema aisee dada yangu umezaa katoto kazuri sana maashaallaah! Vipi kwa asiye muislamu au hata mwislamu lakini hajui? Vipi kwa msababishiwa maana neno hili tunaona linamhusu msababishaji tu?

Pili ni kujiepusha na kuexpose mambo yetu bila sababu za msingi hasa mambo ya kimaendeleo. Unakuta kwa mfano siku hizi na hizi smartphone kila kitu mtu kinachohusu maisha yake tunakijua kupitia simu yake mwenyewe. Kila afanyacho kila hatua ni lazima atupostie status kama siyo WhatsApp basi facebook nk. Amevaa vizuri status, Kala vizuri status, katoka out status, kanunua gari status, kupata nyumba status, kapata mtoto status, nk. Yaani kwenye status jambo lisilo la kimaendeleo tutakaloona ni msiba au ugonjwa tu mengine yote ni ya kumeremeza watu na kuringishia. Hapo mwenyewe anafurahia kuona viewers wamekuwa wengi kwenye status zake hizo kumbe hajui anajikaanga mwenyewe

Tatu ni kujiegemeza kwa mola muda wote. Kujiegemeza huku ni kwa dua, udhu na twahara, swala, kauli njema, swadaka, nk. Siyo kwamba kila unachojizuia nacho ndio hakitakupata hivyo lazima tukubali kwamba mola ndiye mwamuzi wa yote. Kuna nyiradi mbalimbali za kumuomba mola akukinge na madhara ya uchawi na kijicho

Mwisho ni kutibu sasa maana hizo za mwanzo zilikuwa ni kama kinga. Kama amejulikana msababishaji wa kijicho atatakiwa kutawadha (kutia/ kuchukua udhu) huku yale maji yanakingwa kisha anakwenda kuogeshwa yule aliyesibiwa na kijicho (msababishiwa). Ni ngumu kwa dunia ya leo sijui utaanzaje kumshawishi mtu afanye hivyo, maana atakuona wewe mchawi au atakwambia umemfanya yeye ni mchawi. Bora baba au mama akigundua amemdhuru mtu wa familia ni rahisi tu kumsaidia kwa njia hiyo. Kwa case yako pia kuna afadhali umesema ni mdogo wako unaweza kumwelekeza tu akakuelewa. Chukulia watu tofauti na hao, wengine mnakutana tu barabarani hujui hata watokako wala waendako! Ndiyo maana nimetangulia kusema kujiegemeza kwa mola. Mambo yote ni kwa neema tu na rehema za MwenyeziMungu. Juhudi zetu zinacheza padogo mno

Kijicho hakiishii kwa watu pekee bali kinadhuru hata mali, mifugo, miundombinu nk. Yaani mtu anaangalia tu mifugo yako lakini excitement yake inasababisha mifugo isitoe mazao ya uhakika, ikonde au hata kuanza kufa. Vivyo hivyo kwenye majumba, magari na mali nyinginezo kijicho kinaweza kusababisha zinasambaratika au zikaharibika. Kijicho pia hutofautiana kati ya mtu na mtu. Mwingine kinakuwa kikali zaidi madhara yake ya wazi na ya haraka na mwingine madhara yake ya taratibu au madogo mno
Nimekuelewa sana
 
Eti imani potofu.
Hivi unaweza kuelezea mechanism gani inaweza kutumika kutoka One million views mpaka elfu 1 ndani ya masaa 24?
Kila dakika moja nilikuwa napata followers 2-10 lakini ikawa ndani ya masaa 24 napata 1-5?
Ni hali tu yakibiashara,,kwanza angalia ulipojikwaa,usiangalie ulipoangukia,fanya ivyo kwa umakini,then ndo utoe hukumu.
 
Back
Top Bottom