KUWA MAKINI unaposhoboka na wanawake barabarani!

Uwezekano upo. Ila ni mdogo Sana Sana.
Wadada wa Sasa wanaangalia masilahi zaidi.

Hawezi kumuuza Mchaina KWA njemba zake Isipokuwa Mchaina kazingua kupitia MAELEZO.

Bi dada akigungua Mchaina anamlipa vizuri KWA uhakika hawezi kuita njemba hata Moja.

Ila tahadhari ni nzuri.
 
Tupe kidogo mkuu ilikuwaje??
Mambo ya ujana bwana, Nilikuwa sio mtu wa kuonekana sana mtaani sasa kuna siku nilikuwa free nikasema acha nitembee tembee niujue mtaa. Nikapita kwa Mangi nichukue juice ndo nakutana na huyo mchumba baada ya salama na kila mtu kuchukua mahitaji yake tukajikuta tunaondoka kwenda uelekeo mmoja.

Baada ya stori mbili tatu na kujiulizisha kile na hiki "Nikajiongeza"πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚. Tukawa tunawasiliana day after day. Sasa siku ya tukio tulipanga tukapate dinner sehemu fulani pamoja na kuuvusha usiku pamoja (eneo alichagua yeye). Baada ya kujiandaa na kutoka home kama Bahati vile machale yakanicheza nilijikuta tuu namcheki mwanangu mmoja na kumuulizia chimbo kali la kupoa hapo mjini, akanipa ramani nzima nikampitia mchumba na kubadili uelekeo wa tulipokubaliana Mwanzo.....

Nilishangaa kumuona kabadilika ghafla na simu zikawa nyingi nikimuambia apokee anajikausha.Baada ya hekaheka za hapa na paleπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ akaenda maliwato ndo nikapata nafasi ya kuona text zikiingia huku mimi ndio nikiwa main target ya huko ambako tulikuwa tuende mara ya kwanza.
 
Duh hatari, ulikuwa unaingia kwenye mfumo!
 
Itakuwa huko uchinani hakuna vikao vya wanaume, unaendaje kwa mwanamke na gest zipo kama hutaki afike kwako?
 
ha
Hao wote ni wezi kuanzia huyo dada yako sasa utamjuaje mke wa mtu km yeye hasemi
 
Yaani nimekupa lift halafu imefika mida ya kushuka uniletee pigo sijui nipe hela yangu????

Mzee hiyo gari itaondoka kwa tyres za nyuma mwendo wa ngiri mpaka ghetto, tunaenda kuelewana ukiwa kitandani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…