Kuwa maskini Tanzania ni chaguo la mtu mwenyewe. You can choose to die poor

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
1998 nikiwa na miaka 12 kijijini kwetu alikuja kijana mmoja kutoka mkoa mwingine, alikuja kutafuta maisha.

Alisema baada ya miaka 10 atawapa watu vibarua. Alifika hana kitu, kibarua chake cha Kwanza alilimishwa na Doni mmoja pale kijijini kwa makubaliano ya kupewa baiskeli used phoenix.

Alipewa baada ya kumaliza kazi. Mda huu naongea watoto aliowazaa akiwa pale kijijini mmoja ni daktari, mwingine lieutenant wa TPDF, yule bro ana nyumba kali kijijini na Wilayani ana nyumba kama 4 mpaka sasa.

Ana gari mbili za kutembelea.
Ushuhuda huu ukupe nguvu unapoamua kuinuka na kutafuta
Tanzania ina kanda kuu takribani 5, hali ya hewa inatofautiana kutoka Kanda moja mpaka kanda nyingine.

Ni zao gani duniani ambalo unatamani kulima likutoe kimaisha lakini Tanzania halistawi? Km² 950000 kwa watu 60ml ni nyingi sana.

Kama wito wako ni Uvuvi au kuwekeza kwenye usafiri wa majini tuna km za mraba 61000.
Kuna mahali unaamua tu kujimilikisha hata hekta 1000 bila kuulizwa na mtu ndani ya Tanzania.

Madini nayo usiguse, yapo mengi. Nenda kaishi porini huko ujigundulie dhahabu uchimbe taratibu.

Sijasema lazima uwe tajiri.
Sizungumzii utajiri nazungumzia umaskini.

Unakuwaje maskini katika nchi hii huku una exposure?
Mababu, mabibi na wazazi wetu waliridhika na hali zao hivyo wao hawakuwa maskini.

Wewe unayelalamika daily kuwa Maisha magumu ndiye mhusika mkuu wa Uzi huu.

Inuka nenda kokote kajitafutie.
 
Watakupangia Bei ya kuuza!

Tulishaamua kwamba watz wenye asili ya Asia wawe wanatakatisha fedha na utajiri wa wanasiasa waliopo nchini na hao watz walindwe na kuandikwa kwamba wao ni matajiri !

Ndio maana top ten wamejaa wao!

Ni kama kule Kenya wasomali walivyo matajiri kuliko wazawa kwa mgongo wa wanasiasa!!

No hivyo tu!
 
Tanzania ina kanda kuu takribani 5, hali ya hewa inatofautiana kutoka Kanda moja mpaka kanda nyingine.
Ni zao gani duniani ambalo unatamani kulima likutoe kimaisha lakini Tanzania halistawi?
Km² 950000 kwa watu 60ml ni nyingi sana.
Kama wito wako ni Uvuvi au kuwekeza kwenye usafiri wa majini tuna km za mraba 61000.
Kuna mahali unaamua tu kujimilikisha hata hekta 1000 bila kuulizwa na mtu ndani ya Tanzania.
Unajua bei ya mbegu, mbolea na dawa??
 
Pambaneni sana
Kila mahali kuna maisha, ukiona sehemu moja imekataa unaenda kwingine
Naona kuna wadau wanasema kila ardhi utaulizwa, sio kweli waende bara huko hata ukitaka eka 100 unapata
Kuna maeneo hata binadamu wa kutafuta utafikiri Amazon 😄
Mdau mwingine anawataja matajiri na wanasiasa hilo nalo sio kweli
Kuna wasomali wengi kenya wamefungua biashara tena wa kuja, sasa huyo na mwanasiasa wanakutana wapi? Na wana biashara gani na mwanasiasa?

Vijana hela haziji kwa kubet
Mleta mada ana hoja
 
1998 nikiwa na miaka 12 kijijini kwetu alikuja kijana mmoja kutoka mkoa mwingine, alikuja kutafuta maisha.

Alisema baada ya miaka 10 atawapa watu vibarua. Alifika hana kitu, kibarua chake cha Kwanza alilimishwa na Doni mmoja pale kijijini kwa makubaliano ya kupewa baiskeli used phoenix.

Alipewa baada ya kumaliza kazi. Mda huu naongea watoto aliowazaa akiwa pale kijijini mmoja ni daktari, mwingine lieutenant wa TPDF, yule bro ana nyumba kali kijijini na Wilayani ana nyumba kama 4 mpaka sasa.

Ana gari mbili za kutembelea.
Ushuhuda huu ukupe nguvu unapoamua kuinuka na kutafuta
Tanzania ina kanda kuu takribani 5, hali ya hewa inatofautiana kutoka Kanda moja mpaka kanda nyingine.

Ni zao gani duniani ambalo unatamani kulima likutoe kimaisha lakini Tanzania halistawi? Km² 950000 kwa watu 60ml ni nyingi sana.

Kama wito wako ni Uvuvi au kuwekeza kwenye usafiri wa majini tuna km za mraba 61000.
Kuna mahali unaamua tu kujimilikisha hata hekta 1000 bila kuulizwa na mtu ndani ya Tanzania.

Madini nayo usiguse, yapo mengi. Nenda kaishi porini huko ujigundulie dhahabu uchimbe taratibu.

Sijasema lazima uwe tajiri.
Sizungumzii utajiri nazungumzia umaskini.

Unakuwaje maskini katika nchi hii huku una exposure?
Mababu, mabibi na wazazi wetu waliridhika na hali zao hivyo wao hawakuwa maskini.

Wewe unayelalamika daily kuwa Maisha magumu ndiye mhusika mkuu wa Uzi huu.

Inuka nenda kokote kajitafutie.
Rubbish, stupidity of highest level, unafikiri umaskini unaondoka kwa kusikiliza motivation speakers, au, maombi ya mwamposa!? Au, kujiangalia kwenye kioo na kujisemea nitakuwa tajiri kama Bakheresa, harafu iwe!?!!
China, USA, Vietnam, Malaysia, Singapore, umaskini uliisha au kupungua, kwa viongozi wa kisiasa, kuweka Sera Bora za kunufaisha wananchi,
Nikupe kidogo history ya china,
Ili wapate tekinolojia ya kutengeneza, ndege, meli,train, simu, siraha, walikalibisha makampuni yajenge viwanda, watu wake wapate ujuzi, huku wakitumia mbinu za kijasusi kuiba tekinolojia, walipojiweza tu, wakaanza kutengeneza wao hizo bidhaa, kilichofata, ni ama kuyataifisha hayo makampuni ya nje, au kuyawekea mashariti magumu,. Partnership, covert theft of technology, nationalisation, reverse engineering,
Sasa china anatisha kwa magari ya umeme, na tekinolojia aliiba ulaya,!
Hapa kwetu ujasusi unatumika kuua wapinzani ili vilaza watawala waendelee kubaki!
Jiulize mbongo Fernandez, boss wa Nala, kwanini aliwekewa kauzibe kuwekeza bongo? Kuna internet safi ya Starlink, ya, eron musk, Kenya, Rwanda, IPO, bongo, imezuiwa kisa makampuni yaliyopo yametoa rushwa kwa wana siasa,
Hiyo huduma ni nafuu sana,
 
Point ni kukataa umaskini sabb rasilimali zipo nyingi. Shida ni moja nchi yetu haijawa na mifumo mizuri ya watu kutumia rasimali zake kwa usawa na usahihi. Wenye nguvu tu na wajanja janja ndio wanawin situations...na kutokuwa maskini dhana yake si lazima iwe TAJIRI, ila uwezo wa kutatua mahitaji ya msingi bila stress kubwa. Kwanza serikali yetu ione umuhimu wa sera jumuishi na zenye upemdeleo kwa wananchi wote..sera za uchumi nzuri zinazoweza mbeba mtu wa chini pale anapoamua kujishughulisha iwe kwa mtaji mdogo au bila mtaji pesa. Isielekeze zaidi kukusanya kodi kwa wanaoanza uwekezaji , wamlee hadi aanze kujipata..ni suala la mifumo hakuna awezaye kukimbia..atatemper na hesabu kidogo lakini kodi atalipa..hivyo kila mwaka biashara mpya, au ajira mpya zingerekodiwa na zinazoanza kumature zinaanza kulipa kodi..ila kwa hali ilivyo ni mara chache ukaenda jichimbia wapi sijui huko kisha ukafanikiwa..utapasua ila kuuza utakutana na madalali/watu kati wana vitambi balaa...bila wao hugusi soko..yani mifumo ovyo kabisa..all in all tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii..kutokaa sehem moja coz Tz ni kubwa sana...enyi vijana msio na majukumu mengi hasa hujaoa au huna watoto zurula nchi hii mpaka kieleweke.. ila kwakweli KAZI IPO
 
Rubbish, stupidity of highest level, unafikiri umaskini unaondoka kwa kusikiliza motivation speakers, au, maombi ya mwamposa!? Au, kujiangalia kwenye kioo na kujisemea nitakuwa tajiri kama Bakheresa, harafu iwe!?!!
China, USA, Vietnam, Malaysia, Singapore, umaskini uliisha au kupungua, kwa viongozi wa kisiasa, kuweka Sera Bora za kunufaisha wananchi,
Nikupe kidogo history ya china,
Ili wapate tekinolojia ya kutengeneza, ndege, meli,train, simu, siraha, walikalibisha makampuni yajenge viwanda, watu wake wapate ujuzi, huku wakitumia mbinu za kijasusi kuiba tekinolojia, walipojiweza tu, wakaanza kutengeneza wao hizo bidhaa, kilichofata, ni ama kuyataifisha hayo makampuni ya nje, au kuyawekea mashariti magumu,. Partnership, covert theft of technology, nationalisation, reverse engineering,
Sasa china anatisha kwa magari ya umeme, na tekinolojia aliiba ulaya,!
Hapa kwetu ujasusi unatumika kuua wapinzani ili vilaza watawala waendelee kubaki!
Jiulize mbongo Fernandez, boss wa Nala, kwanini aliwekewa kauzibe kuwekeza bongo? Kuna internet safi ya Starlink, ya, eron musk, Kenya, Rwanda, IPO, bongo, imezuiwa kisa makampuni yaliyopo yametoa rushwa kwa wana siasa,
Hiyo huduma ni nafuu sana,
Una stress
 
Hii ni moja ya mada ya kijinga sana, wewe unakeep factors zote constant kwenye uchumi unaongelea perfect market conditions kitu ambacho ni nadharia tu, kiuhalisia hakipo.. sasa sijajua ni utoto au umeamua tu kujitoa akili!
 
Back
Top Bottom