uttoh2002
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 17,060
- 32,400
1998 nikiwa na miaka 12 kijijini kwetu alikuja kijana mmoja kutoka mkoa mwingine, alikuja kutafuta maisha.
Alisema baada ya miaka 10 atawapa watu vibarua. Alifika hana kitu, kibarua chake cha Kwanza alilimishwa na Doni mmoja pale kijijini kwa makubaliano ya kupewa baiskeli used phoenix.
Alipewa baada ya kumaliza kazi. Mda huu naongea watoto aliowazaa akiwa pale kijijini mmoja ni daktari, mwingine lieutenant wa TPDF, yule bro ana nyumba kali kijijini na Wilayani ana nyumba kama 4 mpaka sasa.
Ana gari mbili za kutembelea.
Ushuhuda huu ukupe nguvu unapoamua kuinuka na kutafuta
Tanzania ina kanda kuu takribani 5, hali ya hewa inatofautiana kutoka Kanda moja mpaka kanda nyingine.
Ni zao gani duniani ambalo unatamani kulima likutoe kimaisha lakini Tanzania halistawi? Km² 950000 kwa watu 60ml ni nyingi sana.
Kama wito wako ni Uvuvi au kuwekeza kwenye usafiri wa majini tuna km za mraba 61000.
Kuna mahali unaamua tu kujimilikisha hata hekta 1000 bila kuulizwa na mtu ndani ya Tanzania.
Madini nayo usiguse, yapo mengi. Nenda kaishi porini huko ujigundulie dhahabu uchimbe taratibu.
Sijasema lazima uwe tajiri.
Sizungumzii utajiri nazungumzia umaskini.
Unakuwaje maskini katika nchi hii huku una exposure?
Mababu, mabibi na wazazi wetu waliridhika na hali zao hivyo wao hawakuwa maskini.
Wewe unayelalamika daily kuwa Maisha magumu ndiye mhusika mkuu wa Uzi huu.
Inuka nenda kokote kajitafutie.
Ili ufanikiwe Tanzania unaitaji either:
1. Uwe mtu wa Mungu sana
2. Uwe mshirikina sana
Kuhusu Bidii:
Bidii na mipango inaletwa na Imani kwamba utafanikiwa, na hiyo imani inaletwa na Kuwa mcha Mungu an mshirikina!
Muhimu:
Vitu vyote unavyoona kwa macho, vimeanzia kutokea katika ulimwengu wa roho usioonekana!
Huo ujasiri jamaa aliokuwa nao una Siri, na Siri yake nakueleza Hakuna anayeijua maana ni katika ulimwengu usioonekana!
Mimi nimeona watu wenye bidii mno wanakufa maskini huku Hawana hata chakula, bidii haijawahi kuwasaidia!
Wanadamu ni washirikina Sana!