Kuwa mtanashati au handsome ni mzigo mkubwa

kiredio Jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2024
Posts
989
Reaction score
1,843
Nimeamini kuwa mtanashati ni mzigo mkubwa, hasa ukiwa hauna strong financial stability, expectations zinakuwa kubwa kwa watu wanao kuona, wanalinganisha muonekano wako na kipato chako.

Ukiwa umebarikiwa muonekano nadhifu, wengi watadhani hata mfuko wako upo vizuri, huenda unabangaiza na kupata kidogo. Ukazingatia unadhifu na mavazi mazuri yasiyo na gharama, lakini bado watadhani wewe ni pedeshe.

Hayo yote yananikuta mimi, kila sehemu nikienda nakaribishwa kifalme kwa sababu ya muonekano tu, kumbe mfukoni ni mtu wa hali ya kawaida kabisa.

Am tired of this......
 
ukiombwa unatoa siyo kutuhangaisha na kututamanisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…