Kuna umaarufu na ushawishi yaani Fame vs Influence, kwenye matangazo inaangaliwa influence. Je, neno lako linaweza kumuaminisha mtu anunue unless anaekupa tangazo anataka biashara yake ijulikane
Kingine ni targeting, hapa wasanii wengi kwenye branding wanakwama sana kwa sababu hawana positioning kabsaaa
Mfano shilole anapata sana endorsements za bidhaa zinazohusiana na mapishi kwa sababu kajitanabaisha kama mpishi. Wasanii wengi hawana hiki kitu
Mimi Mars mdada flani classic and fashionable lakini pia analinda sana reputation yake ndio maana matangazo ya nywele na bidhaa za middle class wengi anapata
Diamond jamaa flani bad boy mwenye pesa, mafanikio na flash life kama mbele, kiufupi anaishi dream life ya vijana wengi inayomfanya kuwa fame na influence
Kingine wengi hawana managers ambao elimu zipo kichwani na kaujanja ka mujini kapo. Mfano Hamisa na Idris wanafanya sana kazi na professionals kama dr. Ulimwengu ndio maana wanapata sana deals
Kuwa na fame ni jambo moja, kuwa na influence ni jambo jingine na kubadili followers kuwa pesa ni jambo jingine