Kuwafukuza uanachama Wanawake mashujaa 19 ni kujipiga risasi mguuni

Yaani mchepuko unatoa ushauri kwa mama mwenye nyumba namna ya kumthibiti mumeo
 
Huu ni mtego mkubwa Sana, chama kuogopa kuchukua hatua kwa wanachama wake kisa umaarufu wao.kwa maoni yangu hata wangekuwa wanachama 100 ni kuadhibu tu
Mtaji wa kwanza wa chama ni watu mkuu, na kila unapokua na watu Mia, ujue Una matatizo mia kwa sababu hatufanani! Mdee huyu na Bulaya huyu, wale wale Wanawake wetu mashujaa wa CHADEMA, ila huu ni upande wao wa pili wa shilingi! Kwa hili hawa ni bora kuliko lile Lijuhalikali, lililonyesha mvua ya machozi bungeni!
 
Ushiriki wetu kwenye uchaguzi hakukuhalalisha tume haramu ya ‘uchafuzi!’ Pia tulijua kwamba tume si huru, hata wakati tunaahiriki, lakini ushiriki wetu ulikua na manufaa makubwa kwa sababu, hata vipofu ambao hawakuona udhaifu wa tume, wamesikia kushindo chake! Kupitia ushiriki wa chama na upinzani kwa ujumla kwenye uchaguzi huu, uliofanywa kuwa ‘uchafuzi’ dunia imeona, na haijatulia. Tuna pa kuendelezea mapambano, mnafikiri mmeshinda, lakini tutawaibukia kwa nguvu zaidi!
 
tunawatimua waje huko CCM wawaonyeshe huo ushujaa wao.
Kuna neno limekosewa kwenye sentensi yako mr. Mchambuzi, Sema ‘waende’ huko ccm na si ‘waje’ Huko ccm, kanakwamba na mimi Nipo huko ccm! Tuendelee kuheshimiana mkuu!
 
Cdm watulize boli soon wataanza lamba ruzuku za wabunge hao 20 je watazitema. Nani kakwambia watz wanataka ukombozi watajikomnoa wenyewe siku wakichoka. Kumpigania masikini ni kumkufuru Mwenyezi Mungu aliyewafanya wawe masikini, achana nao wapiganie haki zao wenyewe.
 
Bora ubaki na wanachama 10 waaminifu kuliko kua na wanachama milioni wasaliti fukuzia mbali ili na wengine waogope Tena ikiwezekana uchunguzi ufanyike ili wote waliohusika kufanya uhuni huu waadhibiwe vikali.
Na kweli tukitaka kukaa kwa amani tufukuze wote, tubaki na cream ya wachache, ‘milele’ Lakini kama ni kukua na kuongezeka, matatizo na usaliti, vitazaliwa na kuishi na mafanikio, kama ambayo tumeona tangu yale mafuriko ya Lowasa yalivyo kuja, yakiwa na faida na hasara!
 
Huo mtazamo wako kwamba Mungu aliwafanya kuwa masikini unaitwa fatalism, watu wengi wenye imani kama yako, wana huo mtazamo! Tatizo mtazamo huo unawafanya waendelee kuwa masikini na wasipambane na umasikini kwa sababu wanaamini hiyo hali yao ni mapenzi ya Mungu! Ni mtazamo fake, potofu ambao siyo mapenzi ya Mungu aliye hai, ambaye kuna watu tunamwabudu!
Kwa kusema hivyo, nataka ujue harakati za kumkomboa Mtanzania zimefanyika, zinaendelea kufanyika na zitanyika sana, mpaka kieleweke! Labda wengi wenu hamjui au hamuoni, Lakini hata kazi ya juzi juzi Lisu kwenye kampeni zake, ina mafanikio makubwa, kwa Watanzania na madhara makubwa kwa ccm na mfumo wake!
 
Wamfukuze na MBOWE aliyewasaliti wenzake kipindi kile cha KUIBADILISHA GIA ANGANI ili Lowassa AGOMBEE URAIS....

MBOWE hakuijali katiba Yao Wala mawazo HURU ya WENZAKE....


Leo hii Lowassa Yuko nyumbani...amerudi kwetu LUMUMBA!!!
 

Kama masikini ndo wamaeamua kuichagua ccm ili waendelee kuwa masikini utawasaidia vipi sasa.Check mfano mapolisi wanaishi maisha mabovu wanayosababishiwa na ccm na still wako radhi Hadi kuwaamiza watz wenzao ili ccm ishinde ccm inashinda na haiboleshi maisha ya police Sasa hapo unasemaje.Swali kwann Africa ndo inapata watawala vimeo
 
Ni kwa sababu umasikini na ujinga ni ‘mapacha’! Lakini hatutakiwi kukata tamaa, kwa sababu hii siyo vita ya kuisha leo, au ya Mtu mmoja!
 
Wamfukuze na MBOWE aliyewasaliti wenzake kipindi kile cha KUIBADILISHA GIA ANGANI ili Lowassa AGOMBEE URAIS....

MBOWE hakuijali katiba Yao Wala mawazo HURU ya WENZAKE....


Leo hii Lowassa Yuko nyumbani...amerudi kwetu LUMUMBA!!!
Wewe mwenyewe ni msaliti wa nafsi yako, lakini bado hujafukuzwa!
 
Mbowe ni msaliti namba moja.
1. Alivunja maandamano ya ukuta akasema ameshauriwa na viongizi wa dini. Watu wakakata tamaaa
2. Maandamano ya Mange Kimambi akasema Chaaademu hatuhisiki watu wakakata tamaa.
3. Alipoona Docta Slaa hana pesa akamsaliti akamleta Lowasa Chadema wakatii. Watu wakakata tamaa.
4. Akakodi ndege na kuwapeleka wabunge Dodoma kutafuta maridhiano sisiem wakamshangaa na wapinzani wakamshangaa na huku akimsaliti Ben saa nane aliyekuwa msaidizi wake.
5. Tundu Lisu kwenye kampeni alisimamishwa Siku saba, hakukubali akasema yuko tayari kwa lolote, lakini Mbowe akaitisha kamati ya dharura na kubariki Tundu Lisu kusimama na Tundu Lisu alisimama kwa shingo upande.
6. Mbowe kapeleka wanawake kwa makubaliano na Mdee bungeni anajua atapata ruzuku na mdee atapata ajira. Akawaambia baada ya hapo tutangaza kuwafukuza chama. CCM watawang'ang'ania. Huyo ndiye Mbowe Chadema wanamwini huku yeye anafanya biashara ya siasa.
 
Chuki yako kwa Mbowe inatambulisha upo upande gani, na mpo wengi!
 
upinzani nchi hii hautakufa kwa sababu hakuna chadema. wala chadema haitakufa kwa kufukuza watu 19. upinzani hauwezi kufa kamwe kwa sababu ccm haina mawazo ya kuongoza nchi. ni hajuza. kizee. haina uwezo wa kufanya lolote mbali na kutumia maguvu na hujuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…