Wolle Melkas Fernando
JF-Expert Member
- May 4, 2016
- 253
- 360
Na Wolle;
Kwanza niseme kwenye ukweli huwa siko affiliated na chama chochote kile. Katika mijadala ya tahadhari dhidi ya Corona nimefuatilia sana wengi wakisema serikali ya Magufuli inafanya mzaha na kuhatarisha uhai wa watu.
Wanaosema haya hasa ni viongozi wa Vyama Vya Upinzani na wachache wa CCM na zaidi sana wanasema kwamba uhai haulinganishwi na mapato ama uchumi. Ni kweli uhai haulinganishwi na kitu chochote kile lakini siyo kweli kwamba serikali ya Magufuli inacheza na kuhatarisha uhai wa watu kuhusu uchukuaji wa tahadhari dhidi ya janga la Corona.
Wakati naelekea kwenye point yangu tukumbuke pia kuwa Afrika na Ulaya ni mabara mawili tofauti, kitamaduni, kiuchumi na kijiografia. Mifumo ya maisha ya raia wa Ulaya na nchi za Magharibi ni tofauti na yetu Afrika, mifumo ya biashara ya Ulaya ni tofauti na yetu, miundombinu ya Ulaya ni tofauti na yetu. Ukuaji wa Uchumi wa Afrika ni tofauti na ule wa Ulaya.
Hivi uliwahi kujiuliza kwamba ni kwanini Afrika tusiige mbinu walizotumia Ulaya ili tujikwamue kiuchumi tuondokane na umaskini? Viongozi wengi wa Afrika wamejaribu sana kuziiga hawajafanikiwa, unadhani ni kwanini? Kwasababu ile modeli ya uchumi wa ulaya (European economic model) haiwezi kukidhi haja ya bara la Afrika. Sasa kwanini katika kudhibiti Corona tutumie model inayotumiwa na bara la Ulaya? Tuachane na hayo.
Hapa tujipime wenyewe kwa nchi yetu ya Tanzania tuachane na bara la Afrika. Uchumi wa Watanzania wengi hasa kwenye miji na majiji makubwa ni ule wa 'hand to mouth,' kabla hata ya lockdown yaani hali ikiwa kawaida tu watu wana-starve! Je vipi wakiwa locked down? Haijalishi nusu karantini au karantini nzima (Patial or total lockdown), watu watahangaika sana. Ndiyo maana nasema Kuwafungia raia kwa kitu kinachoitwa 'Lockdown' ni kuwapa ‘DEATH MULTIPLE CHOICE’ Yaani mtu atachagua;
A) Akae ndani kuepuka corona afe kwa njaa au
B) Atoke aende kwenye shughuli za kumpa mkate aepuka njaa afe kwa corona.
Huku nafasi kubwa ya kifo ikiwa kwenye lockdown kuliko wangeachwa wafanye shughuli huku wakichukua tahadhari, kwasababu kumbuka kwenye lockdown raia watapambana na njaa pamoja na polisi ama vyombo vya ulinzi na usalama kwa ujumla. Hapa naungana na Mh. Rais Dr. Magufuli. Na hapa naongezea kuwa lockdown itaua zaidi kuliko Corona yenyewe.
Denis Waitley, mwandishi wa vitabu na mwanasaikolojia aliwahi kusema, “Life is inherently risky. There is only one big risk you should avoid at all costs, and that is the risk of doing nothing.”
Kwa tafsiri ya kawaida kabisa akimaanisha kwamba, “Maisha ni hatari kwa asili. Kuna hatari moja tu ambayo unapaswa kuepukana nayo kwa gharama zote, nayo ni hatari ya kutofanya chochote."
Fikiria Tume-lockdown Dar es Salaam, hapo tutakuwa tunapoteza watu kwa corona na kwa njaa huku uchumi na mapato vikiwa vimesimama. Kuacha watu waendelee na shughuli huku wakichukua tahadhari ni jambo la busara zaidi kuliko kukaa ndani watu wakiwa hawafanyi chochote wakisikiliza habari za corona.
Kumbuka namna ya kurudisha uchumi uliopotea Ulaya ni rahisi zaidi kuliko kurudisha kurudisha uchumi uliopotea Afrika (hasa Tanzania)
Mwisho kabisa nampa Rais Magufuli alama ya “A” kwa kufaulu mtihani ambao somo lake niliwahi kufundishwa na mwalimu wangu wa chuo kwenye kipengele kimoja kinaitwa ‘Professional Dilemma’. Walio wengi wameshindwa kufaulu changamoto hii, wamechanganyikiwa, mara walaumu uchumi kuyumba mara walaumu kutoku-lockdown.
Nakutakia kazi njema, endelea kufanya kazi huku ukijilinda wewe na uwapendao.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA