uungwana classic
JF-Expert Member
- Jun 9, 2014
- 2,324
- 2,085
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpaka sasa hakuna nchi iliyo na uhakika wa matibabu not to mention means to be used to totally tackle down the epidemic virus, sisi wale tunaitwa shit hole countries, Rwanda, Kenya na hizo nyingine unazozing’ang’ania combined, unategemea nn kipya haswa kutoka kwenye hizo nchi?
Hutaki jifukiza, omba, hutaki omba jifungie ndani.
“We are born to die, why fight to live?” The game.
Yeah! We are deadly different,and the difference is--------our ignorance!!Huu ni ukweli usiopingika kabisa, approach yetu katika kudeal na majanga, maendeleo na vingine vingi haipaswi kufanana na Ulaya as we are quite so different in terms of many things, almost everything by the way.
Ukiongea na wazungu wenye mtizamo walau chanya juu ya maendeleo ya Afrika watakuambia, kuna mmoja alini-expose kusoma kitabu kinaitwa “Dead Aid”, humo utajua kwanini Afrika tumepewa misaada ya mabilioni ya dola za kigeni lakini mpaka sasa maendeleo hakuna.
Jiwe ni jiwe kweli kweli na kwa hilo nampa kudos from mi heart.
Hauna mawazo mapya juu ya namna serikali inaweza kupambana na ugonjwa wa corona zaidi ya c&p? hauko productive mkuu,,,Na Wolle;
Kwanza niseme kwenye ukweli huwa siko affiliated na chama chochote kile. Katika mijadala ya tahadhari dhidi ya Corona nimefuatilia sana wengi wakisema serikali ya Magufuli inafanya mzaha na kuhatarisha uhai wa watu.
Wanaosema haya hasa ni viongozi wa Vyama Vya Upinzani na wachache wa CCM na zaidi sana wanasema kwamba uhai haulinganishwi na mapato ama uchumi. Ni kweli uhai haulinganishwi na kitu chochote kile lakini siyo kweli kwamba serikali ya Magufuli inacheza na kuhatarisha uhai wa watu kuhusu uchukuaji wa tahadhari dhidi ya janga la Corona.
Wakati naelekea kwenye point yangu tukumbuke pia kuwa Afrika na Ulaya ni mabara mawili tofauti, kitamaduni, kiuchumi na kijiografia. Mifumo ya maisha ya raia wa Ulaya na nchi za Magharibi ni tofauti na yetu Afrika, mifumo ya biashara ya Ulaya ni tofauti na yetu, miundombinu ya Ulaya ni tofauti na yetu. Ukuaji wa Uchumi wa Afrika ni tofauti na ule wa Ulaya.
Hivi uliwahi kujiuliza kwamba ni kwanini Afrika tusiige mbinu walizotumia Ulaya ili tujikwamue kiuchumi tuondokane na umaskini? Viongozi wengi wa Afrika wamejaribu sana kuziiga hawajafanikiwa, unadhani ni kwanini? Kwasababu ile modeli ya uchumi wa ulaya (European economic model) haiwezi kukidhi haja ya bara la Afrika. Sasa kwanini katika kudhibiti Corona tutumie model inayotumiwa na bara la Ulaya? Tuachane na hayo.
Hapa tujipime wenyewe kwa nchi yetu ya Tanzania tuachane na bara la Afrika. Uchumi wa Watanzania wengi hasa kwenye miji na majiji makubwa ni ule wa 'hand to mouth,' kabla hata ya lockdown yaani hali ikiwa kawaida tu watu wana-starve! Je vipi wakiwa locked down? Haijalishi nusu karantini au karantini nzima (Patial or total lockdown), watu watahangaika sana. Ndiyo maana nasema Kuwafungia raia kwa kitu kinachoitwa 'Lockdown' ni kuwapa ‘DEATH MULTIPLE CHOICE’ Yaani mtu atachagua;
A) Akae ndani kuepuka corona afe kwa njaa au
B) Atoke aende kwenye shughuli za kumpa mkate aepuka njaa afe kwa corona.
Huku nafasi kubwa ya kifo ikiwa kwenye lockdown kuliko wangeachwa wafanye shughuli huku wakichukua tahadhari, kwasababu kumbuka kwenye lockdown raia watapambana na njaa pamoja na polisi ama vyombo vya ulinzi na usalama kwa ujumla. Hapa naungana na Mh. Rais Dr. Magufuli. Na hapa naongezea kuwa lockdown itaua zaidi kuliko Corona yenyewe.
Denis Waitley, mwandishi wa vitabu na mwanasaikolojia aliwahi kusema, “Life is inherently risky. There is only one big risk you should avoid at all costs, and that is the risk of doing nothing.”
Kwa tafsiri ya kawaida kabisa akimaanisha kwamba, “Maisha ni hatari kwa asili. Kuna hatari moja tu ambayo unapaswa kuepukana nayo kwa gharama zote, nayo ni hatari ya kutofanya chochote."
Fikiria Tume-lockdown Dar es Salaam, hapo tutakuwa tunapoteza watu kwa corona na kwa njaa huku uchumi na mapato vikiwa vimesimama. Kuacha watu waendelee na shughuli huku wakichukua tahadhari ni jambo la busara zaidi kuliko kukaa ndani watu wakiwa hawafanyi chochote wakisikiliza habari za corona.
Kumbuka namna ya kurudisha uchumi uliopotea Ulaya ni rahisi zaidi kuliko kurudisha kurudisha uchumi uliopotea Afrika (hasa Tanzania)
Mwisho kabisa nampa Rais Magufuli alama ya “A” kwa kufaulu mtihani ambao somo lake niliwahi kufundishwa na mwalimu wangu wa chuo kwenye kipengele kimoja kinaitwa ‘Professional Dilemma’. Walio wengi wameshindwa kufaulu changamoto hii, wamechanganyikiwa, mara walaumu uchumi kuyumba mara walaumu kutoku-lockdown.
Nakutakia kazi njema, endelea kufanya kazi huku ukijilinda wewe na uwapendao.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
Kumbe ndiyo maana Uganda vifo vimekua vingi sana!
Covid isipoisha je?.Mkuu bandiko lako linakosa usahihi kabisa. Uganda, Rwanda, Kenya ni Afrika wala si ulaya au marekani kama unavyojaribu kujidanganya. Baadhi wamekwenda total lockdown na partial lockdown. Wengine ni masikini kuliko hata sisi. Wako vizuri na wanasonga mbele.
Ugonjwa umedhibitiwa na hakuna aliye kufa njaa.
Acheni kufanyia siasa Jambo hili ambalo liko wazi mno. Hivi tafsiri zenu mnazipatia wapi? Mbona yameelezwa sana haya mkuu?
Hoja za wanaoona lockdown haifai ni zipi? Tuelimishane - JamiiForums
Hizi njaa mnazoimba kila siku mnaziota tokea wapi?
View attachment 1429029
Wenzetu wasingekuwa na lockdown, ungekuta sasa wako kwenye malaki wanaelekea kwenye millions of cases and deaths! Nawashangaa sana mnaosema eti Mbona lockdown haijawasaidia! Tumieni akili! Hili gonjwa mtatafutana. Haya!Kuna ushahidi wowote wa takwimu kwamba Nchi za Afrika mashariki zilizofanya lockdown zimepunguza maambukizi kwa asilimia ngapi na sisi ambao hatujafanya lockdown maambukizi yameongezeka kwa asilimia ngapi dhidi ya wenzetu? kwa kuangalia tu madhara ya lockdown waliyoyapata hao unaowasema ni makubwa sana vikiwemo vifo sisi hicho kitu kwetu hakipo. Msipende kuiga na kukosoa masuala ya msingi kama haya, acheni!
Covid isipoisha je?.
New infections mtazipunguza tu na sio kuzizuiaMkuu hii ni sayansi siyo ramli. Ugonjwa utakwisha na ndani ya muda si mrefu.
Lockdown inasaidia kuwapata wote walioambukizwa na kuwatenga kwa hatua stahiki. Huu ni ugonjwa wa siku 14 tu.
Kadri maambukizi yalivyo mengi kabla ya lockdown ndivyo zoezi la kuwapata wote litakavyo hitaji muda zaidi.
Logically lockdown inatumika kuweza kuidhibiti kasi ya maambukizi. Baada ya hapo shughuli zinarejea katika hali yake ya kawaida na tahadhari zaidi ikiwapo.
Kumbuka serikali ingeitikia mapema kabla ya ugonjwa:
1. Kuzuia ndege na wageni toka nchi zenye maambukizi
2. Kuweka quarantine wageni kwa siku 14
Ugonjwa usingeingia nchini au ungedhibitiwa mapema kama ilivyokuwa kwa case ya Uganda.
Lockdown itatufanya tusafishe ndani kisha sasa tunaporejea hali ya kawaida tu implement hayo hapo juu kuzuia ugonjwa usiingie tena. Huko ndiko ambako Rwanda na Uganda wanaelekea sasa:
Corona virus: Tunajifunza nini toka kwa wengine? - JamiiForums
Wewe unawasikia wakililia Lumumba?
Tunaowasikia sisi wako huku:
New infections mtazipunguza tu na sio kuzizuia
Its all over the world
Naona Mh kaona arisk watakaokufa wafee tu ila wengi watabaki
Labda nikwambie kitu.mimi sipo ccm siku zote ni mpinzani.
Ila mimi sio mpinzani FUATA MKUMBO NINA AKILI ZANGU TIMAMU..
siwezi kupigia kelele lock down ambayo hainisaidii kitu.wakati kazi zangu ni za kutoka nje.
Niliwahi kukuuliza UNAFANYA KAZI GANI AMBAYO ITAKUFANYA HUMUDU MAKALI YA LOCKDOWN DOWN.
Mpaka unakufa hautakuja kunijibu
Sent using Jamii Forums mobile app
Inatosha kukwambia kwamba Tanzania bila "lockdown (partial/total)" au "Curfew" itashinda vita dhidi ya COVID-19, upende usipende.Mkuu kwanini tunakomalia sana marekani?
Kwa nini siyo Rwanda, Uganda, Kenya wala South Africa?
Au labda mkuu huu ugonjwa utaondoka je hapa kwetu? Si unajua kuutokomeza ni mpaka kila mwathirika apatikane mmoja mmoja kutoka kokote kule aliko nchini?
Mkuu nini mbadala?
Kwa nini mstakabala huu wanaotumia Rwanda na Uganda ni mwiba kwetu? Tatizo liko wapi?
View attachment 1429085
Uganda wana uzoefu wa muda mrefu wa kupambana na majanga (km ukatili wakati wa utawala wa Amini) ikiwemo magonjwa yanayoambukiza (km ebola). Sikiliza hiyo "video clip" uliyoweka kwa umakini.Umeuliza kupata majibu? Au kujikoki kufikia conclusion unayotaka?
Mind you the two are different. Ila kama unataka ushahidi mmoja huu hapa:
Kama unataka zaidi tutakupa.
Inatosha kukwambia kwamba Tanzania bila "lockdown (partial/total)" au "Curfew" itashinda vita dhidi ya COVID-19, upende usipende.
Baada ya ushindi, Tanzania itakuwa imara katika nyanja zote za maendeleo kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia. Kwa mfano:-
1) Kijamii: watu watakuwa wamebadili tabia za kiafya kutoka nyakati za giza za kutokujali usafi wa miili yao na mazingira.
2) Kisiasa: mshikamano bila kujali itikadi zao.
3) Kiuchumi: kuzingatia kanuni mhimu za uchumi hususani matumizi mazuri ya rasimali watu na vitu.
4) Kiteknolojia: uvumbuzi wa zana za uzalishaji mali, pale ambao bidhaa mhimu zinazalishwa hapa nchini badala ya kutegemea kuagizwa kutoka nchi za nje kulikofungwa mipaka.
Ni kweli kutahitajika nguvu za ziada ili kila mwananchi azingatie ushauri wa kitaalamu kujikinga dhidi ya maambukizi ya COVID-19. LAKINI, mwisho wa siku faida ni kubwa kuliko hasara, kama zilivyotajwa hapo juu.
TANZANIA bila korona inawezekana kama kila mwananchi atatimiza wajibu wake wa kuthamini uhai wake na wa mtu mwingine bila kujali siasa, dini, rangi, elimu, hali ya maisha nk
Niwatakie Waislam mfungo mwema na salama.
Uganda wana uzoefu wa muda mrefu wa kupambana na majanga (km ukatili wakati wa utawala wa Amini) ikiwemo magonjwa yanayoambukiza (km ebola). Sikiliza hiyo "video clip" uliyoweka kwa umakini.
Kenya na Rwanda, ni nchi ambazo ziko kwenye "total/partial lockdown" kiwango cha maambukizi ni kikubwa kuliko Tanzania na Burundi ambako wananchi wanaendelea na shughuli zao kwa kuzingatia tabia sahihi za kiafya.
Hali halisi kwa leo ni kama ifuatavyo:Isije kuwa unayo sikiliza siyo hii tunayoisikiliza wengine?
Acheni siasa. Waachieni wataalamu wa afya washauri kitaalamu hatua za kuchukua:
1. Uganda na Rwanda hawana vifo vya Corona.
2. Uganda na Rwanda wana wagonjwa wachache wa Corona kuliko sisi..
3. Uganda na Rwanda maambukizi yamepungua mno na wanaelekea kulegeza hizi lockdowns kwenda kwenye maisha ya kawaida.
Hawa wanaelekea kwenye hiyo prosperity uliyotumia muda mwingi kuielezea. Hawa jamaa watatupita katika yote hayo ya prosperity.
Sisi tusipoangalia wakati tukiwa tunahangaika na huu ugonjwa wenzetu watakuwa kwenye real mavuno.
Umeisoma au umepita tu kwa kuwa tayari una maoni hasi. Katika bandiko langu hilo, na michango yangu humu JF, kuhusu gonjwa hili, nimeandika: TANZANIA bila korona inawezekana kama kila mwananchi atatimiza wajibu wake wa kuthamini uhai wake na wa mtu mwingine bila kujali siasa, dini, rangi, elimu, hali ya maisha nkMkuu umeandika mengi zaidi kwenye faida ikiwa ugonjwa umeondoka. Yaani umeongelea mno ubora wa peponi baada ya kufika badala ya kujikita kwenye namna ya kufika kwanza.
"Inatosha kukwambia kwamba Tanzania bila "lockdown (partial/total)" au "Curfew" itashinda vita dhidi ya COVID-19, upende usipende."
Ni jambo la kheri sana kuishinda Corona kwa namna yoyote ile. Ila tutaishinda vipi tupe mkakati au mikakati mkuu.
Mikakati iko wapi?
Utajiri na kheri ya baadaye bila kujali hatari ambayo hujaivuka kitabu cha "Lila na Fila Havitengamani" kinatambua mada muhimu yenye kufanana na hali yetu leo: "Tamaa mbele, Mauti nyuma".