Kuwafungia raia yaani kitu kinachoitwa Lockdown ni kuwapa ‘DEATH MULTIPLE CHOICE’

Kuwafungia raia yaani kitu kinachoitwa Lockdown ni kuwapa ‘DEATH MULTIPLE CHOICE’

Na Wolle;

Kwanza niseme kwenye ukweli huwa siko affiliated na chama chochote kile. Katika mijadala ya tahadhari dhidi ya Corona nimefuatilia sana wengi wakisema serikali ya Magufuli inafanya mzaha na kuhatarisha uhai wa watu.

Wanaosema haya hasa ni viongozi wa Vyama Vya Upinzani na wachache wa CCM na zaidi sana wanasema kwamba uhai haulinganishwi na mapato ama uchumi. Ni kweli uhai haulinganishwi na kitu chochote kile lakini siyo kweli kwamba serikali ya Magufuli inacheza na kuhatarisha uhai wa watu kuhusu uchukuaji wa tahadhari dhidi ya janga la Corona.

Wakati naelekea kwenye point yangu tukumbuke pia kuwa Afrika na Ulaya ni mabara mawili tofauti, kitamaduni, kiuchumi na kijiografia. Mifumo ya maisha ya raia wa Ulaya na nchi za Magharibi ni tofauti na yetu Afrika, mifumo ya biashara ya Ulaya ni tofauti na yetu, miundombinu ya Ulaya ni tofauti na yetu. Ukuaji wa Uchumi wa Afrika ni tofauti na ule wa Ulaya.

Hivi uliwahi kujiuliza kwamba ni kwanini Afrika tusiige mbinu walizotumia Ulaya ili tujikwamue kiuchumi tuondokane na umaskini? Viongozi wengi wa Afrika wamejaribu sana kuziiga hawajafanikiwa, unadhani ni kwanini? Kwasababu ile modeli ya uchumi wa ulaya (European economic model) haiwezi kukidhi haja ya bara la Afrika. Sasa kwanini katika kudhibiti Corona tutumie model inayotumiwa na bara la Ulaya? Tuachane na hayo.

Hapa tujipime wenyewe kwa nchi yetu ya Tanzania tuachane na bara la Afrika. Uchumi wa Watanzania wengi hasa kwenye miji na majiji makubwa ni ule wa 'hand to mouth,' kabla hata ya lockdown yaani hali ikiwa kawaida tu watu wana-starve! Je vipi wakiwa locked down? Haijalishi nusu karantini au karantini nzima (Patial or total lockdown), watu watahangaika sana. Ndiyo maana nasema Kuwafungia raia kwa kitu kinachoitwa 'Lockdown' ni kuwapa ‘DEATH MULTIPLE CHOICE’ Yaani mtu atachagua;

A) Akae ndani kuepuka corona afe kwa njaa au

B) Atoke aende kwenye shughuli za kumpa mkate aepuka njaa afe kwa corona.

Huku nafasi kubwa ya kifo ikiwa kwenye lockdown kuliko wangeachwa wafanye shughuli huku wakichukua tahadhari, kwasababu kumbuka kwenye lockdown raia watapambana na njaa pamoja na polisi ama vyombo vya ulinzi na usalama kwa ujumla. Hapa naungana na Mh. Rais Dr. Magufuli. Na hapa naongezea kuwa lockdown itaua zaidi kuliko Corona yenyewe.

Denis Waitley, mwandishi wa vitabu na mwanasaikolojia aliwahi kusema, “Life is inherently risky. There is only one big risk you should avoid at all costs, and that is the risk of doing nothing.”
Kwa tafsiri ya kawaida kabisa akimaanisha kwamba, “Maisha ni hatari kwa asili. Kuna hatari moja tu ambayo unapaswa kuepukana nayo kwa gharama zote, nayo ni hatari ya kutofanya chochote."

Fikiria Tume-lockdown Dar es Salaam, hapo tutakuwa tunapoteza watu kwa corona na kwa njaa huku uchumi na mapato vikiwa vimesimama. Kuacha watu waendelee na shughuli huku wakichukua tahadhari ni jambo la busara zaidi kuliko kukaa ndani watu wakiwa hawafanyi chochote wakisikiliza habari za corona.

Kumbuka namna ya kurudisha uchumi uliopotea Ulaya ni rahisi zaidi kuliko kurudisha kurudisha uchumi uliopotea Afrika (hasa Tanzania)

Mwisho kabisa nampa Rais Magufuli alama ya “A” kwa kufaulu mtihani ambao somo lake niliwahi kufundishwa na mwalimu wangu wa chuo kwenye kipengele kimoja kinaitwa ‘Professional Dilemma’. Walio wengi wameshindwa kufaulu changamoto hii, wamechanganyikiwa, mara walaumu uchumi kuyumba mara walaumu kutoku-lockdown.

Nakutakia kazi njema, endelea kufanya kazi huku ukijilinda wewe na uwapendao.

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
Acha kuzungumza kama unaishi kisiwani jiongeze.
Umezungukwa na nchi 8 bado unataka kuishi kwa mazoea?
Magu ameishafanya majaribio ya lockdown kwao Chato,kesho akikwambia tufunge baadhi ya mikoa au wilaya utakuja hapa tena kutoa sifa?
Kumbe ndio maanake Mwingereza alitaks tupate uhuru miaka ya 2030 hadi 3000 !!!
 
Machozi yako ya mamba siyahitaji jitu lisolujilikana wahedi wee!

Machozi yako ya mamba peleka kwa waliokutuma uwaambie wamekundua.

Ni wazi kuwa vifo vya watu kwenu si issue.w wangapi mmewaua au kuwapoteza. Nini kipya kwenu kuhusu mtu kufa au kuishi?

Ndiyo maana mmetumwa kuja na hizi propaganda ili kununua muda dawa au chanjo ipatikane?

Kwenu nyie matumbo yenu ni muhimu zaidi even if the entire nation perishes, au siyo?

Ila bakini mkijua yote yana mwisho.
Mwisho ni pale wewe binafsi utakapojitambua.

JILINDE NA MLINDE JIRANI
 
Tafuta elimu utajikomboa. Ujinga ulionao ni zaidi ya zigo la miba umejitwika.

Nenda shule.hata ngumbalu itakusaidia.

Kwa eti nyie ndiyo washauri no wonder leo twapanga foleni Loliondo kujipatia kikombe na tunaongelea kujifukiza mvuke wa 100°C kupambana na Corona katika karrne ya 21.

No wonder too hatujui mkakati ni nini na kwa nini unaweza kuwa muhimu.

Kalagabaho - kaa hivyo hivyo. Uko vizuri mkuu.
Huna mbinu yoyote ya kupambana na maambukizi zaidi ya kulaumu. Si ajabu wewe ni mmoja wa wale wasiotii au/na wanakejeri ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya kujikinga dhidi ya maambukizi na kusambaza. Katika mazingira hayo, hata nchi ikiwekwa kwenye "lockdown" COVID-19 haitakwisha. Kenya, Rwanda, nchi za Ulaya (Italia, Uhisoania, Marekani), nk kwa mifano michache hiyo, kuna ripoti za maambukizi mapya kila siku.

Kukusaidia, japo unaweza kuwa na kichwa kizito au ujeuri tu, ili kuzuia maambukizi na kusambaa kwa COVID-19 tunashauriwa na kusisitizwa:-
1) Kuvaa barokoa unapokuwa karibu na mtu au mkusanyiko wa watu kuzuia usisambaze (kama umeathirika) au usiambukizwe (kama haujaathirika). Hii ni kwa sababu kama hujapima huwezi kujua iwapo umeambukizwa au la.
2) Kutakasa mikono (kwa maji ya kutiririka na sabuni au "sanitiser") kabla ya kushika/kugusa mdomo, pua, au/macho, viungo vya mwili vilivyo katika hatari ya kupokea virusi vya korona.

Iwapo kila mtu atazingatia ushauri, hakika virusi vya korona avitasambaa na Tanzania bila COVID-19, inawezekana.

Mengine unayodai ni ya unafiki mtupu.
 
Sijausoma upuuzi wako.

Tafadhali acha kuiandikia si uhitaji upuuzi wako kaa nao
 
Inakufaa wewe na familia yako, inatufaa unajua hali zetu wote mpaka ugeneralize? Wewe ni Mpumbavu na wakupuuzwa, partial lockdown unayoongelea imeshafanyika tayari as shule na vyuo vimefungwa tayari, uwezi ingia taasisi yeyote before hand washing na nyinginezo nyingi, unless otherwise, hujui tofauti ya partially na totally.
Mkuu hii ya kuruhusu makanisa, masoko kujazana???? Hii ya kutudanganya level sit wakati tunatakiwa tukae umbali almost 2m ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hii ya kuruhusu makanisa, masoko kujazana???? Hii ya kutudanganya level sit wakati tunatakiwa tukae umbali almost 2m ...

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hiyo inaitwa kisebu sebu na kiroho papo! Uchumi au maisha kwanza? Tuko njia panda.

Sala si za kukimbiza Corona, bali kumwombea beberu apate dawa au chanjo. Atakaye kufa acha afe atakaye pona haituhusu.

Hii wanaita "The devil's alternative".
 
Be
Mkuu hii ya kuruhusu makanisa, masoko kujazana???? Hii ya kutudanganya level sit wakati tunatakiwa tukae umbali almost 2m ...

Sent using Jamii Forums mobile app
realistically inawezekana? Au ni uwepesi wa kuongea tu. Likiisha hili tatizo watu sijui tutaficha wapi sura zetu, historia ni mwalimu, utadhani hili ndio janga la kwanza na la mwisho duniani. Life goes on no matter the situations.
 
Back
Top Bottom