Umeisoma au umepita tu kwa kuwa tayari una maoni hasi. Katika bandiko langu hilo, na michango yangu humu JF, kuhusu gonjwa hili, nimeandika: TANZANIA bila korona inawezekana kama kila mwananchi atatimiza wajibu wake wa kuthamini uhai wake na wa mtu mwingine bila kujali siasa, dini, rangi, elimu, hali ya maisha nk
Mkuu bandiko lako nililisoma vizuri. Hata katika hili pia, haupo mkakati wa kuishinda Corona iliyosambaa sasa tokea Dar hadi Mbeya, Dodoma hadi Mwanza nk.
Kumbuka malkia Elizabeth, waziri mkuu Boris Johnson, Prince Charles, pana na mbunge hapa kwetu nk. Ni kipi ambacho hawakufanya kiasi cha kupata Corona na hata kuambukiza wengine ambacho wewe unadhani hawakufanya wajibu wao?
Acha maneno weka muziki. Weka mkakati wa kumaliza Corona inayosambaa kwa kasi hapa nchini kufikia kwenye community transmission kwa mujibu wa Ummy.
Usisahau pia si Rwanda wala Uganda waliofikia kwenye community transmission.