Kuwafungia raia yaani kitu kinachoitwa Lockdown ni kuwapa ‘DEATH MULTIPLE CHOICE’


You are wrong. Be fair to yourself. Unknowingly you've subscribed to the doctrine of your master:

Wa kufa acha wafe hadi tunaowaita mabeberu watakapogundua dawa au chanjo. Sasa hivi mko chini ya mnazi kuokota embe dodo.

Beberu mnayemsubiria atafute tiba au chanjo kibongo bongo kwa mlango wa nyuma mna mnanga ati anawaletea corona kwenye misaada yake. Haya ni Tanzania tu!

Watakaopona bahati yao. Watakaokufa tutaita mpango ya Mungu. Shame on you!

Rwanda, Kenya na Uganda wenzetu hao katika EAC wako vizuri. Wanapigana ndani ya machungu yao and they will prevail.

It should concern you if you like, wenzetu tuliochagua kufanana nao ni hawa hapa chini. Disgrace:

 
Yeah! We are deadly different,and the difference is--------our ignorance!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hauna mawazo mapya juu ya namna serikali inaweza kupambana na ugonjwa wa corona zaidi ya c&p? hauko productive mkuu,,,
Mh rais anatakiwa kushauriwa ili atoe maamuzi mazuri.
Unaweza mchoma corona mwilini mwako kwa mvuke wenye 100 C bila wewe kudhurika? hii nayo unaipa A?
Hujawai fikiria namna yoyote ya kupunguza misongamano mijini ili kupunguza kasi ya maambukizi?

Sina chama na sitakuja kuwa na chama.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe ndiyo maana Uganda vifo vimekua vingi sana!

Nadhani kwa wanavyojua wao hata Rwanda vifo vimekuwa vingi sana na vinaongezeka kwa kasi sana kila uchao.

Hao ndiyo werevu wetu na eti wamejizatiti vilivyo vichwani mwao kufungua vinywa vyao mbele za wengine bila hoja wala ushahidi.

Idiots!

Kweli ujinga ni zigo la miiba!
 
Kweli aisee kama hadi leo tunasota kwa hasara ya vita ya Kagera ni kweli kuinua uchumi Africa ni kazi ngumu
 
Covid isipoisha je?.
 
Unafanya mzahaa! Huu ugonjwa ukitupiga kama ulivyopiga Italy halafu tukafanya huo mzahaa unaosimulia hapo juu ndani ya wiki moja nusu ya population ya nchi inaisha!
 
Wenzetu wasingekuwa na lockdown, ungekuta sasa wako kwenye malaki wanaelekea kwenye millions of cases and deaths! Nawashangaa sana mnaosema eti Mbona lockdown haijawasaidia! Tumieni akili! Hili gonjwa mtatafutana. Haya!
 
Covid isipoisha je?.

Mkuu hii ni sayansi siyo ramli. Ugonjwa utakwisha na ndani ya muda si mrefu.

Lockdown inasaidia kuwapata wote walioambukizwa na kuwatenga kwa hatua stahiki. Huu ni ugonjwa wa siku 14 tu.

Kadri maambukizi yalivyo mengi kabla ya lockdown ndivyo zoezi la kuwapata wote litakavyo hitaji muda zaidi.

Logically lockdown inatumika kuweza kuidhibiti kasi ya maambukizi. Baada ya hapo shughuli zinarejea katika hali yake ya kawaida na tahadhari zaidi ikiwapo.

Kumbuka serikali ingeitikia mapema kabla ya ugonjwa:

1. Kuzuia ndege na wageni toka nchi zenye maambukizi
2. Kuweka quarantine wageni kwa siku 14

Ugonjwa usingeingia nchini au ungedhibitiwa mapema kama ilivyokuwa kwa case ya Uganda.

Lockdown itatufanya tusafishe ndani kisha sasa tunaporejea hali ya kawaida tu implement hayo hapo juu kuzuia ugonjwa usiingie tena. Huko ndiko ambako Rwanda na Uganda wanaelekea sasa:

Corona virus: Tunajifunza nini toka kwa wengine? - JamiiForums
 
New infections mtazipunguza tu na sio kuzizuia
Its all over the world
Naona Mh kaona arisk watakaokufa wafee tu ila wengi watabaki
 
Labda nikwambie kitu.mimi sipo ccm siku zote ni mpinzani.
Ila mimi sio mpinzani FUATA MKUMBO NINA AKILI ZANGU TIMAMU..
siwezi kupigia kelele lock down ambayo hainisaidii kitu.wakati kazi zangu ni za kutoka nje.
Niliwahi kukuuliza UNAFANYA KAZI GANI AMBAYO ITAKUFANYA HUMUDU MAKALI YA LOCKDOWN DOWN.
Mpaka unakufa hautakuja kunijibu
Wewe unawasikia wakililia Lumumba?

Tunaowasikia sisi wako huku:


Sent using Jamii Forums mobile app
 
New infections mtazipunguza tu na sio kuzizuia
Its all over the world
Naona Mh kaona arisk watakaokufa wafee tu ila wengi watabaki

Mkuu si kaona kuwa watakaokufa wafe tu wengi watabaki kwani yeye siyo nabii kuwa na uhakika na hilo.

Nadhani kaona wa kufa wafe hadi beberu (anayem-beza kibongo bongo kwa mlango wa nyuma) atakapogundua dawa au chanjo. Atakaye kuwa hai kipindi hicho bahati yake atakaye kufa iwe ni mipango ya Mungu.

Sikiliza madaktari wa wataalamu wengine wa afya - hakuna wanayekubaliana naye kwenye hilo.

Baada ya kuudhibiti na kuisafisha nchi na ugonjwa huu, kwa wananchi panapo nia utazuiliwa kabisa usiwafikie, kama ambavyo ungezuilika kabla ya ugonjwa kuingia kama nia ingalikuwapo. Angalia case ya sasa China, Uganda, Rwanda, South Korea nk.
 

Kwa mawazo yako unadhani nani ana kazi za kubaki ndani? Pana ugonjwa unaosambaa kwa kasi unauwa 5% - 10% ya walioambukizwa. Nadhani ya ugonjwa huu yataonekana zaidi maambukizi yakiwa mengi (yaani likichanganya).

Usipoelewa:

1. Ugonjwa huu siyo siasa. Unapoanza kueleza u CCM au upinzani ujue umeshapotea na unachoongelea siyo Corona tena.

2. Vita zozote kama ilivyo hii inataka sacrifice (kujitoa). Huwezi kupata kote. Pana uchumi na maisha. Lazima kuchagua moja. Hakuna anayesema hakuna athari kwenye uchumi. Hilo hata mtoto mdogo ambaye leo shule haendi kwa sababu vya Corona anajua.

3. Utamudu vipi makali ya lockdown? Hili limeelezewa sana. Kwa mara nyingine nakupa tena hapa:



4. Muhimu kutambua Corona ni vita vya taifa si vita vya mtu mmoja mmoja. Ondoa ubinafsi. Usiseme utamudu vipi sema tutamudu vipi? Sote kabisa kwa umoja wetu.

5. Kwa vile hii ni vita vya pamoja nadhani unaona sasa shughuli yangu, yako na yule si suala tena (yaani ni irrelevant).

Kunywa maji mengi usome kuelewa mjinga utakuwa wewe hadi lini mkuu.

Badilika!
 
Inatosha kukwambia kwamba Tanzania bila "lockdown (partial/total)" au "Curfew" itashinda vita dhidi ya COVID-19, upende usipende.

Baada ya ushindi, Tanzania itakuwa imara katika nyanja zote za maendeleo kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia. Kwa mfano:-
1) Kijamii: watu watakuwa wamebadili tabia za kiafya kutoka nyakati za giza za kutokujali usafi wa miili yao na mazingira.
2) Kisiasa: mshikamano bila kujali itikadi zao.
3) Kiuchumi: kuzingatia kanuni mhimu za uchumi hususani matumizi mazuri ya rasimali watu na vitu.
4) Kiteknolojia: uvumbuzi wa zana za uzalishaji mali, pale ambao bidhaa mhimu zinazalishwa hapa nchini badala ya kutegemea kuagizwa kutoka nchi za nje kulikofungwa mipaka.

Ni kweli kutahitajika nguvu za ziada ili kila mwananchi azingatie ushauri wa kitaalamu kujikinga dhidi ya maambukizi ya COVID-19. LAKINI, mwisho wa siku faida ni kubwa kuliko hasara, kama zilivyotajwa hapo juu.

TANZANIA bila korona inawezekana kama kila mwananchi atatimiza wajibu wake wa kuthamini uhai wake na wa mtu mwingine bila kujali siasa, dini, rangi, elimu, hali ya maisha nk

Niwatakie Waislam mfungo mwema na salama.
 
Umeuliza kupata majibu? Au kujikoki kufikia conclusion unayotaka?

Mind you the two are different. Ila kama unataka ushahidi mmoja huu hapa:


Kama unataka zaidi tutakupa.
Uganda wana uzoefu wa muda mrefu wa kupambana na majanga (km ukatili wakati wa utawala wa Amini) ikiwemo magonjwa yanayoambukiza (km ebola). Sikiliza hiyo "video clip" uliyoweka kwa umakini.

Kenya na Rwanda, ni nchi ambazo ziko kwenye "total/partial lockdown" kiwango cha maambukizi ni kikubwa kuliko Tanzania na Burundi ambako wananchi wanaendelea na shughuli zao kwa kuzingatia tabia sahihi za kiafya.
 

Mkuu umeandika mengi zaidi kwenye faida ikiwa ugonjwa umeondoka. Yaani umeongelea mno ubora wa peponi baada ya kufika badala ya kujikita kwenye namna ya kufika kwanza.

"Inatosha kukwambia kwamba Tanzania bila "lockdown (partial/total)" au "Curfew" itashinda vita dhidi ya COVID-19, upende usipende."

Ni jambo la kheri sana kuishinda Corona kwa namna yoyote ile. Ila tutaishinda vipi tupe mkakati au mikakati mkuu.

Mikakati iko wapi?

Utajiri na kheri ya baadaye bila kujali hatari ambayo hujaivuka kitabu cha "Lila na Fila Havitengamani" kinatambua mada muhimu yenye kufanana na hali yetu leo: "Tamaa mbele, Mauti nyuma".
 

Isije kuwa unayo sikiliza siyo hii tunayoisikiliza wengine?

Acheni siasa. Waachieni wataalamu wa afya washauri kitaalamu hatua za kuchukua:

1. Uganda na Rwanda hawana vifo vya Corona.
2. Uganda na Rwanda wana wagonjwa wachache wa Corona kuliko sisi..
3. Uganda na Rwanda maambukizi yamepungua mno na wanaelekea kulegeza hizi lockdowns kwenda kwenye maisha ya kawaida.

Hawa wanaelekea kwenye hiyo prosperity uliyotumia muda mwingi kuielezea. Hawa jamaa watatupita katika yote hayo ya prosperity.

Sisi tusipoangalia wakati tukiwa tunahangaika na huu ugonjwa wenzetu watakuwa kwenye real mavuno.
 
Hali halisi kwa leo ni kama ifuatavyo:
 
Umeisoma au umepita tu kwa kuwa tayari una maoni hasi. Katika bandiko langu hilo, na michango yangu humu JF, kuhusu gonjwa hili, nimeandika: TANZANIA bila korona inawezekana kama kila mwananchi atatimiza wajibu wake wa kuthamini uhai wake na wa mtu mwingine bila kujali siasa, dini, rangi, elimu, hali ya maisha nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…