GE2025 Kuwafungia watu ndani na kuwazimia internet ni zaidi ya ukatili

GE2025 Kuwafungia watu ndani na kuwazimia internet ni zaidi ya ukatili

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,916
Reaction score
6,527
Mara zote nimekuwa nikiwashauri baadhi ya wanasiasa kwamba, watanzania wa miaka ya 90 sio hawa wa miaka ya 2000. Watanzania wa sasa wamekula 'matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.' Mema wanayajua na mabaya wanayajua.

Hawa wa sasa sio watanzania wa kanga na chumvi. Wala sio wa kurubuniwa na baiskeli zilizo chini ya viwango. Watanzania wa sasa wanaelewa mambo kwa kina.

Viongozi badilikeni acheni mazoea. Ukweli ni kwamba hii nchi sio ya wajinga tena. Heshimuni mawazo ya wananchi. Kuwazimia internet ni kuwanyima uhuru wa kuwasiliana. Hii si sawa hata kidogo.
 
Walichokitafuta (Madaraka) wameyapata sasa kuna kisasi cha huyo mtawala na company yake.
 
Back
Top Bottom