Uwajibikaji ni dhana inayochukuliwa kwa pande mbili katika viongozi mbalimbali wa umma na wale wa siyo wa umma kutokana na mazingira yanayoweza kusababisha viongozi kuingia kwenye hofu ya kuonekana kuwa ni dhambi na ni aibu kufanya hivo.
Mosi,wanaona aibu baada ya kufanya makosa katika utendaji kazi mathalani wale ambao wamepewa dhamana ya kutoa huduma kwa watu na kuleta hasara kwa taasisi na hata kwa serikali,kwa mfano wale waliobainika kulitia hasara taifa kwenye ubadhilifu wa pesa za umma walipaswa kujiuzuru bila hata ya kushinikizwa kwani wakiona wakifanya hivo wataonekana kuwa ni wadhaibu na pia kuonekana kama hawafai katika jamii,hivo ni jambo la busara kujiuzuru pale tu unahisi kuleta hasara kwa taasisi au serikali hii itakujengea utendaji kazi Bora kwa kujali maslahi mapana ya taasisi husika.
Pili,kiongozi anapaswa kuwajibika ili kutengeneza Imani kwa waajiri au mwenye mamlaka ya uteuzi,kwani hii itampa nafasi ya kujua kiongozi huyu anamtazamo chanya juu ya uongozi Bora unaojali maslahi ya taifa kwa ujumla hivo kwa wakati mwingine huyo kiongozi anaweza kujirekebisha na kuteuliwa au kuchaguliwa tena kwani watu watampima kwa kile alochokifanya hapo awali,kwa mfano tunaomba kina baadhi ya viongozi waliotenguliwa uongozi na mamlaka za uteuzi tukiona wakirudi tena kwenye uongozi kutokana na uchunguzi kufanyika kwa kina kwa muhusika na kukna tena kuna haja ya kumrudisha kwenye uongozi,hivo viongozi wanapaswa kuwajibika ili kujiongezea uaminifu kwa jamii inayowazunguka.
Tatu,uwajibikaji huweza kuleta athari chanya kwa jamii kupata watendaji sahihi wenye Nia ya dhati ya kusimamia miradi mbalimbali katika jamii,hii hutokea pale ambapo kiongozi anayekuwa amechukua nafasi Huwa makini sana katika utendaji wake ili kudhihirisha kuwa yeye si kama yule aliyejiuzuru hivyo husaidia kuleta ufanisi mkubwa katika kazi zake na hii huchochea Imani kwa jamii kuona faida za kuwajibika kwa viongozi mbalimbali.
Nne,husaidia kuokoa pesa za umma na kuongeza thamani katika miradi mbalimbali inayokusudiwa katika jamii husika,hapa ni kuwa pamoja na uwajibikaji wa viongozi hii husaidia kupanga matumizi sahihi ya pesa inayokuwa imetengwa kwa miradi husika,kwa mfano kiongozi ambaye alikuwa ameingia mikataba mibovu yenye kuleta hasara kwa serikali au kwa taasisi akijiuzuru mikataba Ike inaweza kubatilishwa kwa kufuata Sheria na hivo kuokoa pesa hizo ambazo zingetumika vibaya kwa manufaa ya wachache.
Tano,pamoja na kuwajibika kuwe na usawa wa ulipaji wa pesa ambazo kiongozi amesababisha kwa kujua ama kutokujua kwani yeye ndiye aliyepewa dhamana hiyo kwani wakati mwingine viongozi wanaotenguliwa majukumu Yao Huwa hawalipi pesa walizobadhilifu hivyo Sheria iwekwe kwa wale wote wanaosababisha hasara kwa taifa walipe kulingana na kile walichokisababisha na hii itatoa funzo kwa viongozi wengine ambao wanatabia kama hizo na hii itaondoa kabisa kama siyo kupunguza viongozi wenye tabia kama hizo.
Kwa ujumla haya na badhi ya mengi ambayo pengine yakizingatiwa basi tutakuwa tumepunguza kwa kiasi kikubwa ufisadi,rushwa na utawala mbovu usiozingatia maadili ya utumishi na pia serikali itakuwa imejiwekea mazingira mazuri ya kuleta maendeleo kwa taifa kwa ujumla.

Upvote
1