Kuwanyima watu uhuru ni chanzo cha viongozi wengi wazalendo Afrika kufeli

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
KUWANYIMA WATU UHURU NI CHANZO CHA VIONGOZI WENGI WAZURI KUFELI

Wakuu nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi. Wote kwa pamoja muitikie CHAMA KIENDELEE. Wale wasiotaka kujibu nawakumbusha kwamba CCM ndo imebeba matumaini ya watanzania wote.

Kwa siku za hivi karibuni niliamua "kujilipua" kuutafuta upande wa pili ukoje kwa hawa viongozi wetu wazalendo wa muda wote hapa Afrika. Kina Thomas Sankara, Lumbumba, Kwame Nkrumah, Siad Barre, na wengine. Huu uamuzi wangu umechangiwa na mambo mengi yaliyojitokeza kwenye mapinduzi ya Rais Alpha Conde huko Guinea. Kiongozi wa mapinduzi amesifiwa ni mzalendo lakini nafsi yangu imegoma kumwamini.

Toka nimepata ufahamu wangu nimeona sifa nyingi sana zikimiminika kwa viongozi wengi wa awamu za kwanza wakati nchi za Afrika zinapata uhuru. Ni wachache sana ambao husemwa vibaya kama kina Bokassa, Mobutu, Idd Amin na Kamuzu. Wengi wao kwa haraka unaweza dhani ni malaika watakatifu. Kimsingi tukubaliane kila binadamu ana kasoro. Hakuna mkamilifu kwahiyo yale mema tuyaige na zile kasoro zao tuzitumie ili kutorudia makosa yao.

Naweza sema kwamba baada ya kusoma vyanzo mbalimbali za historia za viongozi wengi wazalendo niligundua kasoro zao kuu zilikuwa zinafanana. Uzalendo kwa nchi zao ulikuwa wazi kabisa na sio kitu cha kubishana. Kuwaminya wananchi waliokuwa na mawazo tofauti, kuwaumiza wanasiasa waliokuwa na itikadi tofauti, kuendesha nchi kiimla na matendo mengine yaliyofanya waogopwe kupitiliza zilikuwa ni kasoro za hawa wazalendo ambao wengi walikuja kupinduliwa hivyo kupelekea anguko kisiasa. Kwa mfano Sankara alifanya maajabu kiuchumi chini ya miaka mitano kwenye utawala wake lakini alipinduliwa na kuuwawa na swahiba wake ambapo ukitafuta sababu ni haya mambo ya kuminyana na kukosa uhuru wa kuongea hisia zako.

Binadamu unaweza kumpa kila kitu kwenye hii dunia ila unapomnyima uhuru basi kila kitu kinakuwa hakina thamani.. watawala wajifunze kupitia kwa wazalendo. Tunaweza kuwalaumu Mabeberu lakini tukumbuke beberu kashajua watu wanataka kuwa huru hivyo kupitia sisi wenyewe anafanikisha mambo yake. Nawapongeza marais wote wa Tanzania kuanzia waliopita hadi aliyepo kwa namna wanavyojua kucheza na hisia za makundi yote bila kuleta madhara.
 
Ufisadi. Waafrika wamekuwa mafisadi wakubwa sana. Mfano kwenye nchi yetu ni watu wawili tu walijitahidi kupambana na ufisadi kwa moyo wote. Nyerere na Magufuli.

Nchi kama Nigeria pamoja na utajiri mkubwa wa mafuta lakini ina ufisadi wa kutisha. Wanasiasa wa Nigeria ni matajiri kufuru. South wakina Zuma wamepiga tu ufisadi. Wala shida siyo uhuru, labda useme uhuru wa kiuchumi.
 
Unazungumzia viongozi gani na uhuru upi mkuu? Zito Kabwe alitaka kutumia uhuru wake na demokrasia ya ndani ya chama ili agombee uenyekiti wa chama chake cha zamani.. kilichomkuta hata mwenyewe mleta mada unakifahamu. Marehem Chacha Wangwe na yeye alitaka kutumia uhuru wake na demokrasia ya ndani ya chama ili agombee uenyekiti kwa bahati mbaya akashughulikiwa kwa style ya kuchukua uhai wake. Leo hii waliofanya hayo niliyoandika hapo juu wanasota na kusaga meno maana Mungu anawahukumu kimya kimya kwa style anayoijua yeye. Ama kweli dunia ina mambo!
 
Ufisadi. Waafrika wamekuwa mafisadi wakubwa sana. Mfano kwenye nchi yetu ni watu wawili tu walijitahidi kupambana na ufisadi kwa moyo wote. Nyerere na Magufuli.

Nchi kama Nigeria pamoja na utajiri mkubwa wa mafuta lakini ina ufisadi wa kutisha. Wanasiasa wa Nigeria ni matajiri kufuru. South wakina Zuma wamepiga tu ufisadi. Wala shida siyo uhuru, labda useme uhuru wa kiuchumi.
Kweli kabisa mkuu
 
KUWANYIMA WATU UHURU NI CHANZO CHA VIONGOZI WENGI WAZURI KUFELI

Wakuu nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi. Wote kwa pamoja muitikie CHAMA KIENDELEE. Wale wasiotaka kujibu nawakumbusha kwamba CCM ndo imebeba matumaini ya watanzania wote.

Kwa siku za hivi karibuni niliamua "kujilipua" kuutafuta upande wa pili ukoje kwa hawa viongozi wetu wazalendo wa muda wote hapa Afrika. Kina Thomas Sankara, Lumbumba, Kwame Nkrumah, Siad Barre, na wengine. Huu uamuzi wangu umechangiwa na mambo mengi yaliyojitokeza kwenye mapinduzi ya Rais Alpha Conde huko Guinea. Kiongozi wa mapinduzi amesifiwa ni mzalendo lakini nafsi yangu imegoma kumwamini.

Toka nimepata ufahamu wangu nimeona sifa nyingi sana zikimiminika kwa viongozi wengi wa awamu za kwanza wakati nchi za Afrika zinapata uhuru. Ni wachache sana ambao husemwa vibaya kama kina Bokassa, Mobutu, Idd Amin na Kamuzu. Wengi wao kwa haraka unaweza dhani ni malaika watakatifu. Kimsingi tukubaliane kila binadamu ana kasoro. Hakuna mkamilifu kwahiyo yale mema tuyaige na zile kasoro zao tuzitumie ili kutorudia makosa yao.

Naweza sema kwamba baada ya kusoma vyanzo mbalimbali za historia za viongozi wengi wazalendo niligundua kasoro zao kuu zilikuwa zinafanana. Uzalendo kwa nchi zao ulikuwa wazi kabisa na sio kitu cha kubishana. Kuwaminya wananchi waliokuwa na mawazo tofauti, kuwaumiza wanasiasa waliokuwa na itikadi tofauti, kuendesha nchi kiimla na matendo mengine yaliyofanya waogopwe kupitiliza zilikuwa ni kasoro za hawa wazalendo ambao wengi walikuja kupinduliwa hivyo kupelekea anguko kisiasa. Kwa mfano Sankara alifanya maajabu kiuchumi chini ya miaka mitano kwenye utawala wake lakini alipinduliwa na kuuwawa na swahiba wake ambapo ukitafuta sababu ni haya mambo ya kuminyana na kukosa uhuru wa kuongea hisia zako.

Binadamu unaweza kumpa kila kitu kwenye hii dunia ila unapomnyima uhuru basi kila kitu kinakuwa hakina thamani.. watawala wajifunze kupitia kwa wazalendo. Tunaweza kuwalaumu Mabeberu lakini tukumbuke beberu kashajua watu wanataka kuwa huru hivyo kupitia sisi wenyewe anafanikisha mambo yake. Nawapongeza marais wote wa Tanzania kuanzia waliopita hadi aliyepo kwa namna wanavyojua kucheza na hisia za makundi yote bila kuleta madhara.
Wanajiita wazalendo lakini sio wazalendo kweli.
 
Nilivyoona CCM nichama kilichobeba matumaini ya watanzania sikujisumbua kusoma zaidi, kawaambie wenzako CCM muache wizi wa kura na securities za nchi kutishia maisha ya wananchi
 
Back
Top Bottom