Kuwatumia vibaya Diamond na Ali Kiba kwenye siasa za Simba na Yanga ''kutaua" soka la Tanzania

Haikuwa promotion mkuu. Watu walikuwa wanaambiwa tu wiki ijayo kuna mechi ya Simba na Yanga. Hakukuwaga na blah blah blah sijui Msanii fulani atakuwepo etc
Ndo promotion yenyewe hiyo mkuu, watu wakishaambiwa kuna mechi siku fulani ni nini hicho kama si promo!?
 
Tunakoelekea itabidi tuwaombe CCM tekiniki za kujaza uwanja Kwa kusomba watu kwenye malori
 
Haikuwa promotion mkuu. Watu walikuwa wanaambiwa tu wiki ijayo kuna mechi ya Simba na Yanga. Hakukuwaga na blah blah blah sijui Msanii fulani atakuwepo etc
Sasa unataka tuishi kama zamani? Hata huko ulaya kukiwa na big match huwa inapigwa promo kupita maelezo. Msilazimishe kila jambo la zamani lionekane bora kuliko la sasa, kwanza zamani watu walikuwa wanalazimika kwenda uwanjani kwasababu mpira ulikuwa hauoneshwi kwenye luninga na hata ikibahatika unaoneshwa ilikuwa hovyo sana.

Tofauti na sasa, mpira unaoneshwa live na kwa ubora kabisa lkn maelfu bado wanaenda uwanjani licha ya maisha ya sasa kuwa na changamoto nyingi kuliko zamani.
 
Kizazi hiki kinawaza hela na kubet kuliko mahaba ya dhati ya timu zao.


Leo hii Yanga ikicheza ikashinda mashabiki wa Simba wanafurahi maana mikeka imetiki and viceversa is true.

LIKUD mzee mwenzangu wahenga walisema kila zama na kitabu chake, hivyo zama za sasa hazitaki tuishi kwa misingi ya 1970's bali tuishi kwa misingi ya 2020's
 
Sahihi kabisa mkuu
 
Reactions: K11
Miaka ya tisini kulikua na uwanja unaobeba watu elf sitini?
Elfu 40 shamba la.bibi. elfu 40 com kirumba. Elfu 30 sokoine. Elfu 25 Sheikh Amri Abeid Arusha . Elfu 25 mkwakwanj Tanga. Elfu 30 Ali Hassan Mwinyi Tabora. Elfu 30 uwanja wa Amani Znz. To mention but a few
 
Kadri miaka inavyozidi kwenda Tasnia ya Michezo na Burudani hapa Bongo inazidi kukosa wapenzi mashabiki.
 
Mapato yalikuwa sh ngp [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kama ulitaka kuzungumzia mapato ungefanya hivyo ila mada iliyopo na majibu yako yalikuwa idadi ya watazamaji
 
SAGAI,
Nadhani tuangalie mienendo ya wanamuziki wetu na jinsi wanavyojipatia kipato kupitia umaarufu na umaarufu huo wanaupataje?
Mara nyingi umaarufu wa wanamuziki wa nchi hii unapatikana kutokana na mabifu.

Hadija Kopa Vs Nasma Khamis.
Msondo Vs Sikinde
Vijana Jazz Vs Bima Lee
TOT Plus Vs Twanga Pepeta
Ali Kiba Vs Diamond
Nk nk nk.

Ukiangalia vizuri ni kama Diamond kafuata upepo wa mafanikio ya Yanga ya miaka 2 hii ili kutengeneza fedha, lakini akaegemea kwenye bifu la Manara na Barbara (Simba) ili apate mapokezi Makubwa toka Yanga akijua baada ya tukio lile atazoa subscribers wengi toka mashabiki wa Yanga na akaunti itatuna. Yaani mashabiki wake wa siku zote ukiunganisha na wapya wa kutoka Yanga watakaofuata mkubwa, kipato hakitakuwa haba. Na naamini alifanikiwa.

Baada ya kuona hivyo Kiba naye akatafuta Nitoke vipi ili apokelewe Simba. Kama zali tamasha la Simba ambalo miaka ya nyuma lilifana Kwa kutumia mafanikio ya uwanjani ya msimu husika mwaka huu kigezo hicho kikakosekana kikabaki kigezo cha Utambulisho wa Wachezaji pekee. Ndipo Kwa ubunifu mkubwa Ahmed Ally akaibuka na Kibegi. Kibegi kikawa Kibegi na tena kikatengenezewa Version. Kikawa na version I, II na III ambayo Kiba aliibuliwa from no where. Kwa vile ni Msanii akaibuka na Wimbo àmbao ulipambwa Sana na Wanasimba ili kunogesha tukio wengine wakidiriki kusema ndio wimbo Bora wa Simba hivyo ufanywe wimbo rasmi wa timu (Team anthem). Lakini ukisikiliza wimbo wenyewe na rithym ya kawaida ya Simba Simba vinakwenda tofauti. Hata baadhi ya maneno yaliyomo kama vile Simba ndiyo timu No.1 Afrika hayaakisi uhalisia.

Kwa maoni yangu nakubaliana na wewe kwamba kuhamisha muziki bila tahadhari na kuupeleka kwenye soka letu kutakuwa na athari chanya na hasi na ni dhahiri hasi itazidi chanya.
Ukiangalia kwenye siasa kama uwanja wa kufanya siasa Tanzania ungekuwa level, hawa wanamuziki usinhewaona wote wakiwa CCM. Huko wamekwenda kulinda vitumbua vyao wakihofiwa kupigwa rungu na serikali wakionekana upande wa pili au kuwa neutral. Utakumbuka Diamond alitaka kulinda hadhi yake Kwa kubaki neutral kisiasa akapelekewa TRA na akaangushiwa bill ya Kodi bil.4?

Nimalizie Kwa kusema viongozi wenyewe wa timu wanapaswa kuchukua tahadhari za makusudi kulinda Kwa wivu hadhi ya soka isitekwe na kitu kitakachofubaza radha yake.
 
Unapobisha uwe na takwimu siyo kumpinga Mtu ionekane wewe wa kisasa wakati yeye ni wa zamani na Wa kisasa pia maana nyakati zote mbili alikuwepo. Una Taarifa Mechi ya Simba Vs Pamba ilikuwa inajaza uwanja wa CCM Kirumba bila promo na watu wengi wanabaki nje kama walioko ndani? Je, uwanja wa Kirumba u achukua watu 8000 kama ulivyosema? Unajua mwaka 1990 Tanzania ilikuwa na watu wangapi na Sasa inao wangapi?
 
Nilitaka nimjibu hivyo hvyo, eti anachukulia poa watu kufika 40k uwanjani, tuviwanja twa zamani wakiingia watu 15k tu tumejaa.
Ali Hassan Mwinyi
Kirumba
Kambarage

Vimejengwa mwaka 2020?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…