Kuweka au Kutokuweka WhatsApp status: Kuna uhusiano na mtu kuwa smart, msomi au tajiri?

Kuna makundi mengi sana ya Binaadamu.

Kundi moja ni lile linalojiona (SPECIAL) huwa na kitu kinaitwa EGO.

ubaya wa Ego ni kwamba kuna uhusiano mkubwa sana na ROHO mbaya + Wivu.

Niende kwenye Mada.

Binafsi ni muwekaji mzuri wa Status (Napostigi Memes) hii hali imenifanya hata siku nisipoposti huwa naulizwa leo kulikoni?!.

Napenda Maisha ya kiujamii ndio maana ikaitwa mitandao ya KIJAMII.

kuna kundi la wenye Sonona.. mfadhaiko.. na Mateso ya kiroho (ROHO MBAYA) hawa watu.. huwa hata Profile Picture hawaweki.. hili kundi linajificha katika kivuli cha PRIVACY and MATURITY.

mtu mwenye Privacy hatumii Whatsapp kabisa.. hilo liko wazi

Mwisho wa siku nikikuona una hizo Element's huwa nafutaga Namba tu ukawafanyie Umaturity ndugu zako huko sio mie.. napenda watu low key na wapo real.

NB: nina contacts 120 nilioruhusu waview status ni watu 30.
 
Kuna prof yy status yake haikauki video za vichekesho ...na slogan yake ni moja ana "Furaha panapo huzuni"
 
Iko hivi status za WhatsApp zimewekwa kwa matukio maalum ni km ka-album fulani ka picha za mnato ambazo mtu anaweza ku-post ila sasa kuna baadhi ya watu wanatumia vibaya

Status ipo kwa ajili ya kuonyesha matukio ya video na picha na km una kadarasa kako unataka kuelimisha watu au kuhamasisha unaweza kutumia status

Kingine kupitia status unaweza ukaisoma saikolojia ya mtu anapitia hali ipi ya kimaisha maana wale wazee wa kupost post ovyo ovyo kupanga reli hua hawafichagi hisia zao za ndani na hua wanazielezea kwa lugha ya picha

Wengine ni wale ambao kwanza huwezi kuiona hata picha yake WhatsApp hata status huwezi kuiona picha yake hata iweje ni hawako social kabisa wao ni kuangalia status maalum tu na wapo WhatsApp kwa ajili hio tu

Mfano:- wazee wa connection hawa wao huangalia status kuona connection zipi zimepostiwa na zipo wapi? Kwa hio huo ndio mlengo wake

Wengine wanasaka madili kwa kupitia WhatsApp status unakuta kuna deal imepostiwa pamoja na vigezo vya deal husika huyo anajiweka sawa anaenda kuingiza pesa

Ila kuna wale bora liende hawa sitaki hata kuwazungumzia maana hawajui hata nini maana ya status wao hupost chochote hadi mavi walitoka kunya wakiamua kupost wanapost bila uoga na bila kufikiria mara mbili impact ya like wanachokifanya

Naweka karamu chini..
 
Mimi napost sana status lakini KAMWE sipost maisha yangu, picha yangu au Shughuli zangu.
Napostig mauza uza tu😂, hasa hasa comedy videos design kama zile za Mwaisa 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…