Kuweka au Kutokuweka WhatsApp status: Kuna uhusiano na mtu kuwa smart, msomi au tajiri?

kuna wale wa whatsapp GB wanaweza wakawa wanakuchora tu, halafu kuna wale wakuzima read receipt hawa nao wanaweza wakaview na usijue.
 
Nikumbushe tu aliyeidhinisha kuwepo kwa status ni miongoni mwa matajiri katika 10 bora. Sasa ww ambae hujawahi hata kutengeneza chochote cha kuitingisha dunia unasema kuweka status ni kutokuwa smart?? Why Africans are like this??
Kwa hiyo Mark Zuckerberg ndo role Modal wako basi sawa mkuu kazi iendelee [emoji1787][emoji1787]
 
Kaweka private huyo akiview huoni ila kuna wengine hawana muda kuangalia na kuna wengine wanaangalia za watu fulan maalum
 
Mimi nimeondoa sehemu ya status (natumia gb whatsapp) kutokana na hali mbaya nayopitia kiuchumi. Kuna watu nina namba zao afu wako vizuri so najiondolea maudhi madogo madogo kama hayo.

Lakini ukiacha hivyo hata kuna kipindi fulani nilikuwa njema lakini nilikuwa naboeka. Mtu anaweka jambo status wakati lilitakiwa mtu afuatwe inbox. Mfano utakuja " Jack mambo yako haya" ukicheki huyo jack humjui. Hasa mimi nione kwa sababu gani.
Btw kuna wengine status zao unafurahia. Ni asilimia ndogo wengine ni [emoji706][emoji706].

Am introvert by the way sipendagi kufuatilia ya watu.
 
Binafsi nawekaga status mbalimbali,,,,lkn mambo ya personal life na family siwezi nimeshindwaga.

Cha muhimu Kila mtu na akipendacho na kufurahia
🀘🏿🀘🏿
 
Kupitia Whatsapp utajua watu smart na Hawa wenzangu na Mimi

1. Mtu smart huwezi mkuta kaweka DP ya picha yake Whatsapp

2. Mtu smart huwezi kuta anaweka mastatus mara kwa mara na akiweka basi ujue ni jambo muhimu sana ambalo anataka kufikisha ujumbe kwa njia hiyo

3. Mtu smart hana muda wa ku view status za watu, ila hapa Kuna wa aina 2 Kuna ambao Hawa view kabisa na Kuna wale ambao wana view lakini wakiona unapost pumba au unajipost sana wanakukataa Hawa view tena

Wale wenzangu na Mimi wanaenda kinyume chake
 
Mnajishaua sana machuriti pipo
 
Binafsi huwa siweki sana, kwa mwezi naweza kuweka mara moja au mbili na sioni shida mtu kuweka ama kutokuweka....


Kitu ninachokikumbuka kuhusu status ni kuwa zimevunja penzi nililolipepelea kwa mwaka na zaidi..πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sio kwamba hawaweki status watsapp ila wewe umeblockiwa usione wanachokipost.

Unajua watsapp unaweza kumposti hata mchepuko wako na status akaiona yeye peke yake na akajua kuwa unampenda sana hata kuudhihirishia umma wa watsapp !ila kiuhalisia unaset aone yeye peke yake
 
Binafsi niliacha kupost na kuamua kuthamini privacy yangu nilianza toka siko vizuri kimaisha ila nikapenda maisha ya kuplay ghost (anonymous) nikaja kupata wazo la kifungua no zingine nazotumia kwa kuad biashara zangu na kunawateja wengine ni ndugu zangu na hawajui muuzaji ni mimi na wife[emoji16] kwaiyo nkipost ni nikwajili ya pesa tuu na sio kuonesha maisha yangu na nimeyapenda kwakweli[emoji16] unakutana na watu anashangaa kweli ndugu yangu umebadirika umeng'aa mimi ni kucheka tuu[emoji16]
 
Sijui nikoje sipendi na hata huo mda wa kuwaza kuweka Sina yani Niko tuu hapo naona kawaida sana.
 
Binafsi naweza kupost hata kitu cha kijinga watsapp ila nahakikisha watu ninaoheshimiana nao wasikione...nina limit visibility tu!!

Kuna wale wana ambao mnaweza mkakutana mkaongea shits hao hawana shida ila wazazi,wakwe,ndugu na hata mke nahakikisha hawajui activities zangu za mitandaoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…