Kuweka au Kutokuweka WhatsApp status: Kuna uhusiano na mtu kuwa smart, msomi au tajiri?

Childish stuff.
 
Namba moja sio kweli DP na smartness ya mtu wapi na wapi
 
Mimi na uzee wangu kwenye status unikuti ila JF mimi ni mteja haswa.
 
Sasa wewe kwakua kusaga na Mo ameweka ...na wewe unaweka ....!

Huna sababu zako binafsi za kuweka au kuto weka..!!


Kama huna sababu ya kuweka sio lazima...

Kama ipo sawa weka...



Mi binafsi sio mpenzi wa status, sioni sababu ya kuweka ... Najiulizaga niweke kwa nini?

Najikunta sina jibu naacha. Na huo muda wa kuzitazama za watu sina.


Kalaghabaho ......mo akiwa shoga na wewe uwe shoga
 
Kuna mama mmoja, ni mtu wa kanisa mke wa mtu.
Tunafanya naye matusi sana tena kuliko mwenzie.
Hizo status zake za wasap sasa!!!
- Mungu muweza wa yote
- Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu,
- Methali 14:1-18 Mwanamke mwenye hekima
- Wewe, Mungu, Bwana wetu,

ANGALIZO: MAISHA YA MITANDAONI NI MAIGIZO TU, KWA WALIO SMART HAWANA HIZO TAKATAKA
 
Wengine ni wafanyabiashara na status ni sehemu ya matangazo ya bidhaa zake......na hata akiweka sura kwa ajili kuwajengea wateja wake Hali ya kuaminika..........Mimi nadhani ni jambo personal kulingana na utashi na lifestyle ya mtu.....
 
Kwa hiyo unaumia?
 
Naona unaniongelea mkuu asante nilikuwa sijijui kama ni smart.
 
Suala la status limetupa sana obsessions zisizo za lazima. Watu wanatafuta self worth kupitia status, na ndio maana neno status kwa kiswahili maana yake ni Hadhi.
 
Mimi kupitia status nina uwezo wa kujua uzito wa akili ya mtumaji kama ni feather ,middle au heavyweight....ila 90% nimegundua ni feather weight na wapo kwa ajili ya kuexpose hisia zao za kimaisha bila kujua kwamba akili zao nazo zinakuwa exposed zipo uchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…