NDESSA
JF-Expert Member
- May 2, 2013
- 1,946
- 1,796
Hili suala mimi naliangalia kwa mtazamo tofauti nilichokifikiria ni nn kusudi la WhatsApp na mitandao mingine kutuwekea dp, mimi nimechukua maana halisi ya profile kama sehemu ya kuweka personal details za mhusika wa account, Kwahyo mimi natarajia dp iwe utambulisho wangu kwa mgeni wa acc yangu kama ni watsap ikiingia namba mpya nikienda watsap nikaona picha naweza kumfaham mhusika mara moja, kama ni Facebook pia nikiingia profile nimjue mhusika wa hyo account, nadhani hili lilikuwa kusidio la waanzilishi wa hizo networks, leo hii ni nadra kukuta picha ya mwenye acc mara mtu kaweka kiatu etc huwa nakerwa sana na hayo matumizi ya dp na bora wanaoweka wake/waume, wanaoweka boyfriend/girlfriend anamnadi dp siku chache wameachana anaweka dp za kulaumu au kuponda au za kumlilia Mungu, akipata mpenzi mwingine anaanza tena, na zaidi ni hawa wanaoweka dp watoto wachanga yani mtoto kazaliwa leo kesho yuko dp hajafungua hata macho, na ujinga wote huu unafanywa na wanaojiita wasomi.