Kuweka Records Sawa: Utaratibu alioupendekeza Shabiby ndio uliokuwepo kabla, Haufai

Kuweka Records Sawa: Utaratibu alioupendekeza Shabiby ndio uliokuwepo kabla, Haufai

Urusi haijawekwa vikwazo kwenye mafuta na gesi, hata Ulaya bado inanua mafuta na gesi kutoka Urusi. Hujui unachosema, akili yako imedumazwa na kufungwa na mawazo ya kijamaa yaliyopitwa na wakati na ambayo hayajawa na tija kwa nchi yetu kwa muda mrefu sana tangu kuwepo kwake.

Urusi imewekewa vikwazo miamala.
 
hili aliliweka wazi kinaga ubaga

Shabiby kasema sababu ya kuletwa Bulk Procument System ni Wazungu wa TOTAL kulalamika ku loby serikalini kwamba Wahindi wa JAMNAGAR (walionunua GapOil na GapCo) wameshusha bei ya mafuta kupindukia walipokuja Tanzania.

BPS ilipoanzishwa JAMNAGAR akaona hakuna ushindani, business plan yake ya kuja Tanzania ilikuwa kushusha bei kuteka soko, akaondoka zake.

Bei zikafumuka tena.

Wewe hujui kununua makampuni mawili kwa mpigo sokoni na kushusha bei ilikuwa mkakati wa kuua ushindani ilibadae wa monopolize soko? Washukuriwe TOTAL kwa kuistua serikali vilaza hawakuliona hilo.
 
sasa kama serikali ya tozo inategemea kuvuna hela humo humo kwenye mafuta unategemea waruhusu watu binafsi kujiagizia wenyewe? haya mambo hayahitaji digirii kujua tatizo lilipo, nilishawahi kusema mtu kama mwigulu anakuaje waziri w fedha, for God sake how?
Mama anaupiga mwingi, tena miguu yote…
 
Serikali haiwezi kwenda deep sea

Kifupi kuna machinga wauza mafuta mengine ya wizi 'magendo nk huko deep sea.Mengine yanatoka nchi zilizowekewa vikwazo hivyo wenye business vya mafuta huamua kuyauza kwa magendo .Serikali na magendo wapi ns wapi

Shabby alichoshauri watu binafsi waachie hiyo shughuli Serikali isubiri Meli bandarini kachukue kodi zao mafuta bei rahisi waingie

Hizo meli zinaitwa Ro Ro kama sikosei ziko nyingi deep ni machinga waliochangamka ambao huuza bidhaa nyingi tu ikiwemo.mafuta

Huu no wakati muafaka Serikali iruhusu sekta binafsi waingize mafuta itashangaa. Mafuta ya bei chee yataingia
Mkuu,
Ndio maana nikasema Serikali ijiridhishe ubora na usalama wake, me and uhalali wake kwanza
 
Muhindi anapata wapi mafuta ya bei nafuu ilhali source ya mafuta ni moja na bei zinajulikana?
Muhindi wa JAMNAGAR anaongoza dunia kwa uwezo wa ku refine mafuta.

Kama alivyosema Shabiby bungeni.

REFINERY CAPACITY LIST.png

Screenshot at Apr 08 21-08-57.png

Mafuta ghafi duniani yanauzwa bei ya kutupa, sasa hivi ni shilingi laki mbili kwa pipa, yalishuka mpaka elfu 40 kwa pipa mwaka jana... Kinachokinza upatikanani wa mafuta duniani ni uwezo wa kuyachakata...

Nigeria inachimba mafuta lakini wana import mafuta kwa sababu hawana uwezo wa refinery... wanayauza nje machafu (crude) kama yalivyo...

Mhindi aliyekuja Tanzania kabla ya mfumo wa Bulk Procument alishusha bei ya mafuta kwa sababu yuko vizuri kupita mtu yeyote duniani kwenye refinery

Ahmed Shabiby was spot on, he should be listened to
 
Kwanini Shabiby asipewe rungu bei zianguke 50%. Kwanini kukaa kubishana badala ya kumpa mtu nafasi akafanya mambo?
Kila nchi duniani hadi Ulaya wanalalamika bei ya mafuta, unadhani wao hawaja assess hizo hoja za Shabuby?

Hapo hakuna cha maana ingekuwa ni nafuu basi nchi nyingi zingefanya hivyo lakini hakuna anayetekeleza hayo sababu wanajua
 
we na huyo magufuli wako, kamfufueni aisee, kwani wakati wake mafuta hayajawai kupanda?? Au alikuwa na visima vya mafuta huyo mungu wenu, wenzio wanaongelea mambo ya msingi, we na huyo kiumbe wenu
tuliza wenge mtoto, nadhani umeelewa hoja unajaribu kujitoa ufahamu
 
Muhindi wa JAMNAGAR anaongoza dunia kwa uwezo wa ku refine mafuta.

Kama alivyosema Shabiby bungeni.

View attachment 2180868

View attachment 2180865

Mafuta ghafi duniani yanauzwa bei ya kutupa, sasa hivi ni shilingi laki mbili kwa pipa, yalishuka mpaka elfu 40 kwa pipa mwaka jana... Kinachokinza upatikanani wa mafuta duniani ni uwezo wa kuyachakata...

Nigeria inachimba mafuta lakini wana import mafuta kwa sababu hawana uwezo wa refinery... wanayauza nje machafu (crude) kama yalivyo...

Mhindi aliyekuja Tanzania kabla ya mfumo wa Bulk Procument alishusha bei ya mafuta kwa sababu yuko vizuri kupita mtu yeyote duniani kwenye refinery

Ahmed Shabiby was spot on, he should be listened to
Crude oil kwa bei ya leo ni karibu dola 98, ni zaidi ya laki mbili! Labda nikuulize huyu muhindi nchi zote za Africa hazimjui ? Kwa nini hawanunui mafuta kutoka kwake?,;mombasa leo mafuta ni zaidi ya ksh 150, Kenya hawamjui mhindi?
 
Naona wangeweka import quotas kwenye bidhaa kama mafuta na katika swala la ubora kuna quality assurance na watu wa bureau of standards wataenda kukagua kabla hayajaingia sokoni
 
dola 98, ndio hiyo laki mbili na ushee hiyo niliyosema, tunabishana nini sasa?

na hiyo dola 98 ni leo, lakini mwaka jana kulikuwa na oil glut, mafuta yalishuka mpaka dola 20 kwenye soko la dunia la Brent Crude na soko la West Texas Intermediate... yani shilingi 40,000 kwa pipa...

Waafrika ndio waliwao, ndio wazembe na mazoba kwenye biashara za dunia kama mafuta. Nigeria ina import mafuta japo inachimba mafuta. Haina refineries. Mganda nae anaenda kuuza mafuta machafu kama yalivyo, hana refinery capacity. Julius Nyerere, alikuwa kidume, alianzisha refinery Tanzania, japo hatuchimbi mafuta, hakupenda kusikilizia upepo wa wazungu kwa kila kitu.

Sisi Waafrika ni mazoba, no wonder hatununui mafuta rahisi ya Mhindi wa JAMNAGAR, mwenye refinery capacity kubwa kuliko mwarabu, mrusi na mmarekani.
 
Naona wangeweka import quotas kwenye bidhaa kama mafuta na katika swala la ubora kuna quality assurance na watu wa bureau of standards wataenda kukagua kabla hayajaingia sokoni
Rushwa itasababisha Tbs asikague chochote na mafuta mabovu yataingia sokoni
 
Rushwa itasababisha Tbs asikague chochote na mafuta mabovu yataingia sokoni
Nachoona hapa mchawi ni hiyo kamati ya BPS, kama tunaweza au tunawaza kudhibiti TBS, TRA, TPA basi twende mbele/mbali zaidi tuidhibiti na hii kamati pia. Huko Deep Sea yanakopatikana mafuta ya bei rahisi kamati haiwezi kuagiza huko?
 
Wakuu Kwema?

Mimi kwa kiasi fulani ni mdau wa mafuta, kwani hapo kabla miaka ya nyuma nilishawahi kufanya kazi katika kampuni ya mafuta Kwa kama miaka kadhaa Hivi

Hivi karibuni Mbunge wa Gairo Bw. Ahmed Abdallah Shabiby amependekeza kua ili Bei ya mafuta iweze kushuka basi Serikali iruhusu Wafanyabiashara binafsi waagize mafuta hayo.

Napenda kuweka taarifa sawa tu kua Utaratibu huu anaoupendekeza Bw. Shabiby utumike ndio uliokuwepo hapo awali. Serikali ilikuja kuubadilisha huu utaratibu kutokana na sababu au mapumgufu yake kadhaa, na chache nitazitaja hapa chini.

Kwanza ni ku avoid "Transfer Pricing". Yaani kampuni A iliyopo Tanzania ni tawi la Kampuni B iliyopo labda S.A. Sasa kampuni B ndio inayonunua mafuta inakokujua kisha inaiuzia kampuni A ya hapa nchini kwa bei kubwa kuliko bei ya soko.

Sasa kampuni A ya hapa katika hesabu zake za kodi ya faida 30%x (Mapato - Matumizi) inajikuta inalipa kodi kidogo sababu gharama za uendeshaji zimekua kubwa kutokana na gharama kubwa za manunuzi ya mzigo. Kwa mtindo huu kampuni zingine hufikia hata kuandika wamepata hasara (Manunuzi + Gharama zingine vimezidi Mapato). Kifupi kampuni hukwepa kodi kwa kusingizia gharama kubwa za manunuzi kumbe humo humo anapomlipa Kampuni Mama na faida au dividend anasafirishia hapo hapo kinyemela.

Sababu ya pili Mpaka Serikali ikaondoa utaratibu huu ni kufaidi "Discount on Bulk Purchases". Yaani kampuni 10 zikinunua labda lita million 10 kila moja ni tofauti na kampuni moja ikinunua lita 10mil x 10 = Lita 100mil. Huyu anaenunua lita nyingi ni rahisi ku bargain na kupewa Discount kubwa tofauti na yule anaenunua kidogo. Discount hiyo hupelekea unafuu wa bei Mwishowe kwa finale user.

Tatu ni kua na records za mafuta yaliyoko nchini. Yaani soko likiwa holela kila mtu anaagiza mnaweza kushindwa kujua hata mahitaji ya nchi kwa kipindi husika ni kiasi gani. Hii pia huwezesha Serikali kukadiria (bajeti) Kodi itakayokusanywa kutokana na mafuta haya.

Nne ni kupata bidhaa iliyo bora na standard. Kutokana na Bei mbalimbali zinazosababishwa na ubora mbalimbali basi wengine wanaweza kuchukua au kuagiza hata yale yenye ubora wa chini sababu tu ya unafuu wa bei bila kujali athari zake kwenye matumizi yake. Standard hapa ni viwango vifanane kati ya kampuni moja na ingine. Kusiwe na tofauti kati ya anaejazia BP/Puma au yule anaejazia Oilcom (Ceteris Peribus).

Tano ni kuondoa mafuta ya magendo kwenye soko. Since Mnunuzi wa kutoka nje atakua ni mmoja tu na ndie atakaewasambazia Makampuni ya ndani then kunapunguza uwezekano wa mafuta mengine yasiyolipiwa ushuru kuingia kwenye soko.

Sita, Kwa kuagiza pamoja kunaleta uniformity kwenye Bei. Ingawa Labor na Other Overhead Expenses zaweza kua tofauti lakini bei ya kununulia bidhaa ambayo ndio huchukua sehemu kubwa ikiwa sawa basi Bei hazitapishana sana. Ingawa bei Hupangwa na Ewura lakini kipindi hicho huu utaratibu unawekwa ni Makampuni yenyewe yalikua yanajipangia Bei baada ya kukukokotoa Gharama mbalimbali za kuanzia Manunuzi na Undeshaji pia.

Saba, Kuzuia kuficha mafuta. Kampuni zingeweza kusema hazina mafuta (lower supplies) ili kutengeneza Demand kubwa then bei zipande. Lakini since uagizaji na/kisha ugawaji wa mafuta hufanywa Kwa pamoja then ni rahisi kujua stock ya kila kampuni. Hivyo si rahisi kwa Kampuni husika kuficha taarifa za mafuta iliyo nayo.

Sababu zilikuwa nyingi, nimejaribu kukumbuka chache. Inawezekana mazingira ya wakati ule yangechochea tuhamie kwenye uagizaji wa pamoja labda sababu hizo sio valid anymore so turudi tu kule kule tena. Nimeona kama (nilieliekua) mdau wa mafuta basi nisikae kimya watu wafikiri kua hatujawahi kua katika huo utaratibu alioupendekeza Bwana Shabiby.

Muwe na Siku njema.
Kinadharia uko sahihi kabisa.
Sasa, jaribu kuthibitisha kwa kulinganisha takwimu za wakati huo na sasa hivi ili kupata uhakika.
Inawezekana uhalisia ukawa tofauti kutokana na urasimu, rushwa n.k.
 
sababu za msingi wapi mkuu, hapo zaidi nachoona ni kutokuwajibika kwa taasisi na wahusika wao.
TBS
EWURA
TRA

hizi taasisi zikiwajibika mambo yataenda vizur .
Kiasili taasisi za uma zipo kukusanya mapato zaidi na siyo vinginevyo.
Ukifanyika utafiti rasmi, yawezekana hata weledi hautakuwepo, ni nadharia tu.
 
Nachoona hapa mchawi ni hiyo kamati ya BPS, kama tunaweza au tunawaza kudhibiti TBS, TRA, TPA basi twende mbele/mbali zaidi tuidhibiti na hii kamati pia. Huko Deep Sea yanakopatikana mafuta ya bei rahisi kamati haiwezi kuagiza huko?
Biashara ifanywe na watu binafsi, sio kamati kama tuko Korea Kaskazini.
 
Bei zishuke lakini kwa kufuata sheria na taratibu.

Hatutaki serikali ikose chanzo cha mapato, matokeo yake deni la taifa lina skyrocket.

Tanzania itajengwa na Watanzania, serikali ikusanye kodi na kuzuia ama kupunguza ukwepaji.
Watu wasiojua uchumi utawafahamu.... Hivi hata serikali ikifuta ushuru kabisa ama tuseme magendo yote yakiingizwa obviously bei itashuka na multiplier effect inaonyesha kwamba hta inflation hushuka bei ya mafuta ikishuka. Pia uzalishaji utapanda na mapato ya serikali yatapaa zaidi so usiangalie direct revenue kuna indirect kupitia kuchochea uchumi.

Then kukwepa Kodi sio mpaka waagize watu binafsi hata sasa flow meter imechezewa sana tu so ufisadi upo kwenye process zote tu isitumike kujustify. Maana kama kuna crisis huwezi force kitu kile kile but unaruhusu njia hata tatu au nne wakati Bado unaangalia namna bora ya kufanya.

Huwezi ukang'ang'ania kitu kile kile wakati unaona crisis, eti kuepusha ufisadi as if sahivi huo ufisadi haufanyiki bandarini.
 
Wewe si unajua uchumi kuliko Serikali zote duniani bhana! 👏 👏 👏
 
Wewe si unajua uchumi kuliko Serikali zote duniani bhana! 👏 👏 👏
Mbona kuna nchi zinaitwa tax havens yaani Kodi kibao zilishafutwa mpaka Corporate tax ishafutwa!!! Serikali ilikosa mapato direct ila kupitia kujaa kwa makampuni ajira zikaongezeka so wamegain pesa kupitia Income tax za waajiriwa na mzunguko wa pesa ulioongezeka nchini mwao.

Economics ni long-term strategy sio unaangalia eti ushuru wa mwaka mmoja bila kuangalia picha kubwa ya benefits za mafuta kwa uchumi kwa miaka 5 ijayo!!!
 
Very right. Bahati mbaya awamu iliyopita iliturudisha kwenye dhana ya awamu ya kwanza ya “command economy” na kuaminisha watanzania wengi kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya kudhibiti ufisadi na kukuza mapato ya serikali na uchumi kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom