Kuweka sanduku la kura pasipo Haki tambueni masanduku hayo yatageuka kuwa majeneza (Novena inaendelea)

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
12,283
Reaction score
23,443
Uchaguzi Usio na haki ni laana, Hatuwezi kushiriki laana hiyo kwa mabango, nyimbo wala kwa kutiki wagombea haramu pasipo haki.

Haki huinua taifa, Taifa haliwezi kusonga kama watu wake hawakupatana namna ya kwenda pamoja.

Mungu anatusihi tuidai haki kwanza ili mengine yafuate!

Yeremia 7:5–7
wa kweli mkitengeneza njia zenu na matendo yenu; mkihukumu kwa haki kati ya mtu na jirani yake.....”
Sikilizeni enyi watu mnaotafuta vyeo bila haki wala marekebisho!

Mungu anasema: “Jifunze kutenda mema, tafuteni haki, mkaripieni mwenye kudhulumu,....” (Isaya 1:17).

Lakini ninyi mmegeuza mizani, mlitunga sheria za uchaguzi za dhuluma, na mnatafuta kura bila haki.
Ole wenu waandishi wa amri mbaya, maana hukumu inanyemelea! (Isaya 10:1–2).

Mnaotaka uchaguzi bila mageuzi?
Mnaotaka mamlaka bila haki?
Mnaokimbilia ukuu bila kutengeneza njia za haki?

HAKI NI MSINGI WA AMANI KATIKA TAIFA​

  • Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu kwa watu wote (Mithali 14:34).
  • Hakuna uchaguzi wa amani bila mfumo wa haki.
  • Hakuna kura safi bila mizani iliyo sawa.
  • Haki ndiyo msingi wa uongozi thabiti na taifa lenye mshikamano.
Hakuna baraka juu ya taifa lisilo na haki.

SIKILIZENI; Wenye haki wakiongezeka, watu hufurahi; mwovu atawalapo, watu huugua (Mithali 29:2).

Hata kama kura zitaanguka mikononi mwenu, kiti hicho kitakuwa laana kwenu. Hakuna amani kwa waovu, asema Bwana!

OLE WENU MTAKAOTIKI NA KUIKANA HAKI!

Rekebisheni kwanza mifumo ya uchaguzi kabla hamjaita taifa kwenye sanduku la kura.

Vinginevyo, sanduku la kura litakuwa ndiyo Jeneza lenu, na kura zenu zitakuwa hukumu yenu.

Tumsifu Yesu Kristo. Novena inaendelea kila mtu ashiriki popote kwa imani yake
 
Nimesoma andiko hadi natetetemeka,na mwenye masikio asikie
 
Kuna familia za majunia kina msoga na kizimkazi, kwao mantiki hawaelewi (logic haina maana kwao), wanachojua ni kujihami kwani wanajua moto waliopelekewa na JPM, akija mwingine utakuwa zaidi kwa hiyo wanajihami.

Hii yote inatokana na wizi mkubwa na kujilimbikizia kwao mali kinyume na sheria, walikofanya walipokuwa madarakani, msoga hakuna kampuni la maana asilokuwa na ubia nalo, ikiuzwa airport 10% inamuhusu mtu kama huyo hawezi kuachia madaraka hata akistaafu.

Awamu yake mwanae alipatikana na biashara ya dawa china, ikazimwa kwa kugawa rasilimali, hivi sasa anafanyiwa mipango awe raisi baadae, vuta picha mlanguzi wa dawa za kulevya awe rais, haya yote yanasababishwa na kuwapa kina junior madaraka(Ndio kikwete ni junior).
 
Haki huinua Taifa
 
Dunia haiko hivyo.Endelea kujifariji na kujidanganya kupitia biblia ambayo hakuna mtu anayeizingatia zaidi ya kupumbaza watu.
 
Sawa! Neno la Mungu linasema wapumbavu HUSEMA HAKUNA MUNGU zaburi 14:1
 
Tunaendelea na Novena. Nashauri Wiki mbili kabla ya tarehe 29.10. 2025 tufanye mfungo Mtakatifu pamoja na Novena. Mwisho wa sala za Novena kila siku ipigwe Litania ya watakatifu wote.
 
Back
Top Bottom