KERO Kuweka Smart Lock kwenye Magorofa ya TBA Magomeni Kota ili kufunga milango kodi inapoisha ni ukatili kwa wapangaji

KERO Kuweka Smart Lock kwenye Magorofa ya TBA Magomeni Kota ili kufunga milango kodi inapoisha ni ukatili kwa wapangaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nawapongeza TBA. Wabongo usipokaza hawalipi hasa ikiwa mradi ni wa serikali. Kama mtu hana hela ahame hapo awapishe wanaoweza kulipa.
 
Tatizo exposure
Hujaishi ulaya na marekani wewe
Hizo smart lock kule kiboko .Ukipanga nyumba kodi unayolipa imeunganishwa na maji,umeme na gesi na milango yenyewe
Ikifika muda wa kulipa kodi hujalipa milangi inajifunga yote,umeme,maji na gesi vyote vinakatika uwe ndani ya nyumba au nje na ripoti zinapelekwa kwenye database ya wenye nyumba za kupangisha kuwa wewe ni mpangaji mkorofi na taarifa zingine zinaenda kwa madalali wa kuja kukutoa kwa nguvu.Na toka hapo jiandae kuwa Homeless hakuna mwenye nyumba yeyote atakayekuja kukupangisha wewe chumba au nyumba

Ndio maana waweza kuta homeless wengine wanalala kwenye magari au viambaza wengine sababu ni hiyo
Nchi za wenzetu kodi ya nyumba ni kitu cha kwanza ambacho hawezi cheza nacho

Watanzania tubadilike Uswahili swahili una mwisho wake
Tunaingia ulimwengu wa kidigitali ambapo sio kila wakati mwenye nyumba anakuja kupiga hodi kwako kikudai kodi .Unafungiwa huko .
Aisee noma kweli
 
Wabongo hatuwezi kuendana na teknolojia hata kidogo , hapo awali kulikuwa na huduma za maji kwa kuweka sarafu tu unapata maji kulingana na pesa yako ...Sijui ilikuwaje mkaondoa ule mfumo ili mkope .

Hizo mita nilisikia zipo Iringa kwa sasa ..Lazima uapte utakacho kila siku zile mashine za ATM mnaharibu pia .
Vipato vyenyewe viko wapi majobless tumejaa kila kona. We hv no purchasing power. Sisi ni watu wa kuunga unga
 
Back
Top Bottom