Kuweka taa za barabarani kwenye Barabara kuu iangaliwe vizuri

Kuweka taa za barabarani kwenye Barabara kuu iangaliwe vizuri

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Nafikiri katika technologia ambayo inatakiwa ifanyiwe maboresho ya haraka (kama bado) ni taa za barabarani kwa matumizi ya Highway kwani kwa sasa naona kama hazina manufaa stahiki.

Najaribu kufikiria kwa akili ya kawaida tu, kuruhusu Barabara kuu itumike pengine kwa masaa 6 hadi 10 hivi kati ya masaa 24 na unakuta kuna wakati njia moja haina kabisa magari ila taa inalazimisha magari kusubiri.

Kwa kuwa bado tuna maeneo makubwa, nafikiri ipo haja ya kufikiria kutumia round about kuliko taa za barabarani ikiwa ni Pamoja na kujumuisha vivuko vya watembea kwa miguu kwa maeneo yenye watu wengi

Nakumbuka Barabara ya Morogoro iliyojengwa na Wajapani miaka hiyo; walipo fika eneo la Msamvu moja ya muunganiko wa Barabara ambao ni busy Tanzania kwa kupitisha MALORI na mabasi, waliamua kuweka round about kubwa na kumaliza kabisa msongamano wa magari eneo hilo; Pale Chalinze pia walifanya hivyo hivyo. Kuna uwezekano walitambua madhaifu ya technology ya taa......

Tofauti na round about, nafikiri ipo haja ya kufikiria technologia ya taa za barabarani zenye sensor ya kuweza kuwasha tu barabara yenye magari na pengine kuwasiliana na taa inayofuata ili gari likiruhusiwa, liende moja kwa moja na sio kusimamishwa na taa nyingine pengine ndani ya kilometa mbili....
 
Najaribu kufikiria kwa akili ya kawaida tu, kuruhusu Barabara kuu itumike pengine kwa masaa 6 kati ya masaa 24 na ukakuta kuna wakati njia moja haina kabisa magari ila taa inalazimisha magari kusubiri.
wakati wa regine ya Kikwete kuna adogo walikuja na teknolojia yao ambayo walifanya simulation ikakukalika sana na baadhi ya watendaji wenye mamlaka wakati huo shida ikaja naona kwenye maslahi, baadhi yao wakaona itakuwa mwisho wa upigaji hasa kwenye issue za tender etc....

Madogo wa DIt nadhani walikuja na teknolojia ya traffic light control ambapo teknolojia inaruhusu njia yenye foleni ndefu kuruhu magari kupita, inaendelea hivyo hadi kwa barabara yenye less foleni.

Kwa sababu ya kuabudu vya wazungu hili halikufika mbali likajifia kifo cha mende!!
 
Back
Top Bottom