Kuweni makini na wanaojipima HIV kabla ya tendo

Kuweni makini na wanaojipima HIV kabla ya tendo

Mbona kuvisoma vile vipimo ni simple tu.
Ukiona "Mistari miwili au zaidi POSITIVE(Anao)" ukiona ""Mstari mmoja Negative (Hana).
 
Wasalam

Rafiki yangu mmoja alikuwa mzee wa totozi mawazo mgando akiamini kuwa nurse au daktari yoyote huwa hawapati HIV kwa vile ndio wataalam.

Akawa amempenda Nurse anayemzidi umri kidogo ,wakaanzisha mahusiano kama miezi kadhaa kwa vile nurse alikuwa mbali na yeye alikuwa anamueleza kuwa akija atampima ndo amuruhusu kumla kisongonyi.

Siku huwa hazigandi nurse akaja kumtembelea jamaa yangu ,kabla ya kulala naye yule nurse akampima na kumwambia jamaa yuko negative na nurse nae akamwambia yupo salama Kwa vile jamaa yangu hajui mchanga na jiwe. Test and control ya kile kipimo aliamini vipimo akamla nurse kavu.

Jamaa yangu akamla nurse kama siku tatu hivi. Siku zimeenda siku zimerudi ikawa ni kutembeleana na kulala.

Siku moja nurse alikuja ghetto kwa jamaa na dawa za HIV. Pap jamaa akaona dawa kwenye mkoba wa nurse maneno yenye ukakasi zipo kwenye kopo ...jamaa akadhani ameletewa ameze,kumuuliza nurse wake ,nurse akamjibu aliiba kazini ili akaziuze kwa wale wagonjwa ambao wanaona aibu kwenda kuchukua dawa clinic .

Kila mara nurse alikuwa anampima jamaa kwa siku za kutembeleana alipogundua jamaa tayari ni positive ndo akazidisha mapenzi mlo kamili wa mwili na akili vikazidi miaka akaenda miaka ikasonga siku moja yule nurse alimletea dawa jamaa yangu kama kopo 6 hivi na siku ya mwisho kunyandua nurse akamwambia jamaa atumie condom kwa vile yupo kwenye danger .

Na hiyo ndo ikawa siku ya mwsho jamaa kumuona na nurse na ndo siku nurse alimtumia jamaa sms ya neno moja tu .Kunywa mbaazi nimeacha hapo uvunguni.

Vijana kuweni makini na hao manesi wa kike wanaowapima na ku-fake majibu kumbe wana nia ovu ..kama hujui kipimo tembelea hata youtube na Google utajua test na control humaanisha ..
dooh!
 
Hiyo mistari inakuwa na rangi gani?
1591174905536.png


1591175112704.png


Ikitoke kimstari kimoja katoe sadaka, vikitokea viwili anza tiba mara moja. Kuna maisha baada ya maambukizi.
 
Hebu tudadavulie hapo kila moja ina maana gani? Hasa hio C hapo maanake nini?
Ikisoma C - inasimama kama Negative

Positive inasoma C-1 na C- 2 , lakini inaposoma kwenye hiyo mistari inaonyesha na hali yako kiafya kama HIV yako ipo Strong,Mediuma na Weak pia kwahiyo utajua kupitia hiyo mistari mkuu.
 
Ikisoma C - inasimama kama Negative

Positive inasoma C-1 na C- 2 , lakini inaposoma kwenye hiyo mistari inaonyesha na hali yako kiafya kama Hiv yako ipo Strong,Mediuma na Weak pia kwahiyo utajua kupitia hiyo mistari mkuu.
Ahaa wacha nikatoe sadaka basi kama mdau alivyoshauri pale awali!
 
Mbona kama title imebadilishwa? au Mods washafanya yao
 
Back
Top Bottom