KAGAMEE
JF-Expert Member
- Dec 20, 2013
- 4,457
- 5,454
Nikiri nimechagua kuibiwa kibwege kabisa. Niliona mtu mmoja anayetangazwa na KIGOGO2014 huko Instagram kuwa anauza bando kwa bei nafuu. Nikamfata inbox kuomba kujua zaidi kuhusu hiyo huduma. Akanieleza huduma ni ya uhakika kabisa, nikaangalia kwenye comment zake sikuona comment yeyote mteja akilalamika kutapeliwa.
Nikaamua kuchagua kifurushi cha bei ya chini kabisa cha 13,000 nitest nione yaliyomo kama yamo. Nikatuma hela kwa namba elekezwa, nikampigia akasema ameipata fedha na soon nitaona SMS ya kifurushi. Baada ya masaa manne, nikapiga simu tena, akasema subiri kidogo. Baadaye nikawa napiga simu, hapokei.
Toka juzi mpaka leo hakuna kifurushi wala nini. Nimecheka sana.
Wengine, naomba msiingie kwenye huo mtego tafadhali.