Kuweni makini na wauza vifurushi wa mitandaoni

Kuweni makini na wauza vifurushi wa mitandaoni

Mkuu, umesahau mama Tiba aliposema, alimega fedha kidooooogo ya mboga - 10M, kutoka kwenye ile hela ya Rugemalila?
Dunia hii haina usawa! Wengine hiyo 13,000/= ni ya pipi tu. Wengine ni ya mlo wa familia nzima kwa siku tatu!
Haijalishi. Kuwa na fedha nyingi siyo certificate ya kuruhusu utapeliwe kijinga. Kama huamini nenda katapeli kwa tajiri mwenye fedha uone kitakachokupata.
 
Nilikuwa najua nimatapeli tu wa mitandaoni mpaka jamaa ninaemjua kabisa nilipoona tangazo kutoka kwake. Ndio ninaemtumia huwa ananiunga mbs tu gb 1 huwa nanunua bei kitonga.
Kwa mtu ambae humfahamu vizuri usijaribu matapeli ni wengi kuliko waaminifu.
 
Attachments

  • Screenshot_20240609-083909_Messages.jpg
    Screenshot_20240609-083909_Messages.jpg
    90.4 KB · Views: 5
Umekutana na kitu kizito ila waunga vifurushi og wapo, me ninae mmoja ukitaka vifurushi vya tigo au halotel anakuunga kwanza kisha ndio unamlipa. Nimeshafanya nae kazi karibia mwaka sasa.
Umefunga PM mzee.
 
Eeee kwan inakuuma nafanyia utafiti hela yako?
Sijaumia hata kidogo kwa sababu ya ujinga wako. Unapigwa mchana kweupe halafu unadanganya ni utafiti? Kwa anayetumia akili kidogo tu anaweza kujua huu ni utapeli. Ni kama ule ujinga wa mtu kukuuzia Iphone 15 kwa sh laki moja. Hujiulizi maswali tu?
 
Nikiri nimechagua kuibiwa kibwege kabisa. Niliona mtu mmoja anayetangazwa na KIGOGO2014 huko Instagram kuwa anauza bando kwa bei nafuu. Nikamfata inbox kuomba kujua zaidi kuhusu hiyo huduma. Akanieleza huduma ni ya uhakika kabisa, nikaangalia kwenye comment zake sikuona comment yeyote mteja akilalamika kutapeliwa.

Nikaamua kuchagua kifurushi cha bei ya chini kabisa cha 13,000 nitest nione yaliyomo kama yamo. Nikatuma hela kwa namba elekezwa, nikampigia akasema ameipata fedha na soon nitaona SMS ya kifurushi. Baada ya masaa manne, nikapiga simu tena, akasema subiri kidogo. Baadaye nikawa napiga simu, hapokei.

Toka juzi mpaka leo hakuna kifurushi wala nini. Nimecheka sana.

Wengine, naomba msiingie kwenye huo mtego tafadhali.
Wapo wanao unganisha kweli
 
Kama unatumia halotel,nicheki inbox
Uhakika.
 
Kwahiyo nawewe umepigwa tukio sio. Wanaopigwa tukio huwa wanakaa kimya kama si wao, wewe umepata wapi ujasiri?
 
Kwanza hakuna KIGOGO wa Instagram, Facebook ,Wala telegram. Wote ni magumashi wanatumia jina. KIGOGO og huwa yupo twita na Sasa haandiki tena habari za udaku anajiita KIGOGO MEDIA
Huyo Kigogo og inasemekana alikuwa Makamba Jr alipotimuliwa kazi na Jpm
 
Mkuu, umesahau mama Tiba aliposema, alimega fedha kidooooogo ya mboga - 10M, kutoka kwenye ile hela ya Rugemalila?
Dunia hii haina usawa! Wengine hiyo 13,000/= ni ya pipi tu. Wengine ni ya mlo wa familia nzima kwa siku tatu!
😁😁😁
 
Umekutana na kitu kizito ila waunga vifurushi og wapo, me ninae mmoja ukitaka vifurushi vya tigo au halotel anakuunga kwanza kisha ndio unamlipa. Nimeshafanya nae kazi karibia mwaka sasa.
Vodacom havipatikani?
 
Back
Top Bottom