macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Haijalishi. Kuwa na fedha nyingi siyo certificate ya kuruhusu utapeliwe kijinga. Kama huamini nenda katapeli kwa tajiri mwenye fedha uone kitakachokupata.Mkuu, umesahau mama Tiba aliposema, alimega fedha kidooooogo ya mboga - 10M, kutoka kwenye ile hela ya Rugemalila?
Dunia hii haina usawa! Wengine hiyo 13,000/= ni ya pipi tu. Wengine ni ya mlo wa familia nzima kwa siku tatu!
Wajinga hawaishi. Mtu unatapeliwa kijinga namna hii!Acha kujifariji na kutudanganya huku. We umepigwa na haukuwa unafanya research yoyote ile.
Kuna nyingine za "work from home bei 170,000 per hour..." Nilicheka sana.haina haja ya kuwashitua. acha wapigwe hongera kwa kupigwa hiy pesa
Sijaumia hata kidogo kwa sababu ya ujinga wako. Unapigwa mchana kweupe halafu unadanganya ni utafiti? Kwa anayetumia akili kidogo tu anaweza kujua huu ni utapeli. Ni kama ule ujinga wa mtu kukuuzia Iphone 15 kwa sh laki moja. Hujiulizi maswali tu?Eeee kwan inakuuma nafanyia utafiti hela yako?
Wapo wanao unganisha kweliNikiri nimechagua kuibiwa kibwege kabisa. Niliona mtu mmoja anayetangazwa na KIGOGO2014 huko Instagram kuwa anauza bando kwa bei nafuu. Nikamfata inbox kuomba kujua zaidi kuhusu hiyo huduma. Akanieleza huduma ni ya uhakika kabisa, nikaangalia kwenye comment zake sikuona comment yeyote mteja akilalamika kutapeliwa.
Nikaamua kuchagua kifurushi cha bei ya chini kabisa cha 13,000 nitest nione yaliyomo kama yamo. Nikatuma hela kwa namba elekezwa, nikampigia akasema ameipata fedha na soon nitaona SMS ya kifurushi. Baada ya masaa manne, nikapiga simu tena, akasema subiri kidogo. Baadaye nikawa napiga simu, hapokei.
Toka juzi mpaka leo hakuna kifurushi wala nini. Nimecheka sana.
Wengine, naomba msiingie kwenye huo mtego tafadhali.
Unaona ulivyo mjinga sasa? Hapa utapigwa tena halafu utasingizia kufanya utafiti!Umefunga PM mzee.
Kitendo tu cha kumfuata PM kinaonyesha umeamini. Hii ni stepu ya kwanza ya kupigwa!Kwa hyo namfata PM kutoa hela ulivyo ndezi?
Huyo Kigogo og inasemekana alikuwa Makamba Jr alipotimuliwa kazi na JpmKwanza hakuna KIGOGO wa Instagram, Facebook ,Wala telegram. Wote ni magumashi wanatumia jina. KIGOGO og huwa yupo twita na Sasa haandiki tena habari za udaku anajiita KIGOGO MEDIA
Hiki ni kifurushi cha sh ngapi mkuu?sema asilimia kubwa wengi ni matapeli ila wachache sio, mm kuna mdada ndy ananiungiaga gb 25 vifurushi vya CUG (halotel) na sijawah onana nae kuna jamaa yang alini link nae tu almost miez 9 sahz nafanya nae hii kazi
View attachment 3012271
😁😁😁Mkuu, umesahau mama Tiba aliposema, alimega fedha kidooooogo ya mboga - 10M, kutoka kwenye ile hela ya Rugemalila?
Dunia hii haina usawa! Wengine hiyo 13,000/= ni ya pipi tu. Wengine ni ya mlo wa familia nzima kwa siku tatu!
Vodacom havipatikani?Umekutana na kitu kizito ila waunga vifurushi og wapo, me ninae mmoja ukitaka vifurushi vya tigo au halotel anakuunga kwanza kisha ndio unamlipa. Nimeshafanya nae kazi karibia mwaka sasa.