Kwenye Sura Mbaya nakataa,
Ila sababu zinaweza kuwa Kati ya hizi;
1. Kuigopa Criticism, tuseme kutokujiamini.
Watu wengine huogopa kupost picha au maudhui mtandaoni Kwa kuogopa Maoni ya Watu wengine. Kuogopa kukosolewa aidha kimaumbile au kimavazi au kivyovyote.
Wapo wenye Sura Mbaya na wanapost picha zao mitandaoni. Na wapo wanaoandika vitu vya kijinga na kupost mitandaoni. Hapo ishu ni kiwango cha kujiamini.
Pia wapo Watu wenye sura nzuri wanaogopa kupost mitandaoni picha zao Kwa sababu hawajiamini, na wapo Watu wenye Akili na msawazo Chanya lakini hawajiamini kuyatoa public.
2. Hobby
Wengine sio hobby Yao kupost picha zao mitandaoni au mawazo Yao mitandaoni.
Hapo kuna makundi mawili, wapo ambao huweka picha za maua, majengo, magari, au Watu mashuhuri,
Kundi hili ni lile ambalo likiingia mtandaoni linaingia Kwa ajili ya ku-refresh au kujifunza.