Kuzaa mapema sio kupata msaada/ suluhu za uzeeni

Kuzaa mapema sio kupata msaada/ suluhu za uzeeni

Kuzaa mapema kuna faida sana kuliko kuchelewa.ukijipanga vizuri ni bora uzae mapema.sio unastaafu au ni mfanyabiashara una 55 bado unasomesha hicho ni kitanzi bwana mdogo.mimi ni mhanga wa kuchelewa kuzaa hapa nilipo najuta sana.sio kwamba sitapata msaada lakini hata baada ya kustaafu natakiwa mafao yangu yatumike kuwasomesha wanangu.
Umesema kweli siku hizi kumekuwepo na kasumba mtu akishindwa jambo anataka na wenzie wawe kama yeye mfano huyo hapo anae pinga kuzaa mapema
 
Sijasema Watu wachelewe kuzaa Mkuu.
Nmesema Watu wazae wakishakuwa wamekomaa Kiakili, hisia na kimaumbile, pili, wakishakuwa na uwezo wa kujitegemea, kujisimamia na kutegemewa, tatu, Utayari.

Hausikii Wanawake wakilalamika kuwa Watoto wametelekezwa?
Hunasikia maelfu ya kesi dunaini kuhusu matunzo ya Watoto.

Vipi kuhusu malezi ya Watoto?

Kuhusu muonekano Ipo kwenye ishu ya Umri Mkuu
Mwanaume akisha barekhe tayali kakomaa akili hata mwanamke akiweza kujifungua akili yake imekomaa inategemea na malezi walio yapata kwao
 
Mimi nimezungumzia kuzaa mapema, sinazungumzia kuchelewa kuzaa.
Jambo moja la hakika ni kuwa Matokeo ya kuzaa mapema na kuchelewa kuzaa yanafanana Kwa kiwango kikubwa.
Sio kweli alie wai na alie chelewa awawezi kuwa sawa
 
Nachukizwa sana na wazazi wanao zaa ili waje wawe mizigo kwa watoto wao, wakati wanasahau kwamba wakati huo watoto wao watakua pia wana majukumu yao.
Kuzaa mapema ni jambo jema ili watoto wakuwe ukingali bado hauja chakaa.
Lakini pia ni wajibu wa mzazi kuandaa maisha yake ya uzeeni/kustaafu.
Akili ndogo mzazi wako tangu lini akawa mzigo kwako kuna kitu kizuri duniani kama kumuhudumia mzazi akili zako zinaweza watoto na mkeo basi wazazi huna habari nao [emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Umesema kweli Kabisa.
Sisi wazazi wa kiafrika wengi wetu tunazaa mapema sio Kwa lengo la kukuza Watoto vyema ili wajiandae Kwa Maisha Yao, hapana, bali tunazaa mapema ili tuwahi Kupata matunda ya kuzaa.

Unakuta Mzee anamiaka 55 lakini anamsumbua kijana wake wa miaka 28 ATI amtumie Pesa vinginevyo atamlaani.
Alafu huyo kijana kazi yenyewe anayoifanya utabaki mdomo wazi
Mtoto kwa nini usimpe mzazi wako kadili ya kipato chako?hizi elimu za kizungu zinaambukiza uchoyo wakati huo wazazi wako wakifa njaa ukweni unahudumia kama kawa
 
Mkuu jamaa pale mwanzo kaichambua dhana ya kuchelewa kuzaa, ila wengi wenu naona mmekomalia kwenye umri hamgusii uchumi na afya ya akili.

Mtu anaweza kua na 30 yrs lakini akili ya kitoto, kujisimamia yeye tu hawezi huyo anaachwa akue kwanza. Akizaa akiwa na akili hizo atatafsiriwa kama kazaa mapema.
Miaka 30 ni mtu mzima bhana kama bado yuko na akili za kitoto basi ni punguwani
 
Wazazi wa kiafrika wana vituko sana...yaan ni anazaa kwa ajili ya kupata faida Fulani mbeleni kutoka kwa mtoto mweeh,[emoji848]
Nyiyi ndio mbakana wazazi wenu hata usipo mpa sehemu ya kipato chako utawapa wengine si bora umpe mzazi wako alie kufia ukiwa tumboni mwake?na kumkojolea na kumyea mzazi ni mzazi tu hata mjitoa akili kujifananisha na hayawani(mzungu)
 
KUZAA MAPEMA SIO KUPATA MSAADA/SULUHU ZA UZEENI

Anaandika Robert Heriel,
Kionambali.

"Nazaa mapema ili nipate wakunisaidia uzeeni"
Hapo ataanza kupiga hesabu, "nikifikisha miaka 35 mtoto atakuwa na miaka 10, nikifikisha 45, mtoto wangu atakuwa na 20, hapo nguvu zitakuwa zinaanza kuyoyoma, lakini nitakuwa sinatabu na mtu. Nikifikisha 55, mtoto wangu kashakuwa dume la mbegu au jike la Simba. Hapo sitakosa miambili miambili"
Atameza mate, kisha atasema, kuzaa mapema Raha"

Nani kasema Ulimwengu huu kuna MTU yupo kwaajili yako? Ni Nani huyo?

Taikon Baada ya kufanya chunguzi zangu, ambazo kwa muda huu nazitolea hesabu, nimekaa na Bibi na Babu zangu wenye idadi ya kutosha na umri wa kutosha. Nimejifunza mengi Kutoka kwao, wamenipa uzoefu na mausia Yao. Na kila utakaponiona naandika ujue ni sehemu ndogo ya kile nilichokipata Kutoka kwao kisha kukifanyia uchunguzi wangu binafsi Kwa sababu zakuambiwa unachanganya na zakwako.
Hata hivi leo, haya niyasemayo Mimi Taikon, yasiwe sheria kwako Bali yapokee kisha ukayafanyie uchunguzi wako binafsi.

Kuzaa mapema kuna faida zake na hasara zake, hata hivyo hasara ni nyingi kuliko faida hasa Kwa Zama hizi za ubeberu. Faida kubwa ya kuzaa mapema ni kuyawahi majukumu mapema ya kuandaa kizazi chako, sasa unaweza kuwa unaandaa kizazi tegemezi na Maskini au unaweza kuandaa kizazi kinachojitegemea na chenye utajiri.

Lakini kuzaa mapema maana yake ni nini?
Kuzaa mapema ni kitendo cha kuyawahi majukumu ya Uzazi na ulezi Kabla ya maandalizi au yakujipanga.
Hii itahusisha;

I) suala la umri,
Ii) Hali ya uchumi, na
iii) Utayari.

Kwenye umri kutahusisha mambo ya Akili, hisia, maumbile, Roho n.k. Mtu anaweza akazaa mtoto Wakati Akili yake haijakomaa, au hisia zake bado zinamambo ya kitoto. Hali hii inaweza kuhatarisha malezi na makuzi ha mtoto atakayezaliwa.

Hali ya uchumi, itahusisha uwezo wa kujisimamia, kujitegemea na kutegemewa. Kabla ya kiumbe chochote hakijabeba mimba ni lazima factor ya kujimudu, kujitegemea na kutegemewa na kile kiumbe atakachokileta izingatiwe. Iwe ni ndege, wanyama au Samaki. Haiwezekani kiumbe kibebe mimba Kabla ya kujitegemea.
Kwa upande wa binadamu, ni lazima mtu aweze kujitegemea na awe na uwezo wa kujilisha, kujisimamia na uwezo wa kulisha na kusimamia familia atakayoianzisha.

Wazazi hutoa mafunzo Kwa Watoto wao, mafunzo ya kujidhibiti kitabia hasa zile tabia zenye nguvu lakini zenye matokeo hasi ndani ya jamii, mafunzo ya kufanya kazi na kuzalisha Mali, mafunzo ya kujilinda na maadui iwe wanyama, magonjwa au maadui Watu. Mafunzo ya kukabiliana na nyakati ngumu. Mafunzo ya uongozi na utawala ndani ya nyumba. Mtoto akishahitimu basi atakuwa tayari kuanzisha na kuleta Watoto Duniani.

Ukomavu kiumri wa Kiakili, kihisia na kimwili ukiaunganisha na kujitegemea kiuchumi na kujisimamia ndio italeta Nia na Utayari wa kuanzisha Familia.

Nia au Utayari wowote wa MTU kutaka kuzaa mtoto na kuanzisha familia Kabla ya ukomavu wa Kiakili, kihisia na kimaumbile, Kabla ya kuweza kujitegemea kiuchumi na kuweza kujisimamia na kutegemewa itachukulia kama Tamaa Mbaya ya kushindwa kujidhibiti kitabia.

Hauwezi ukazaa Mtoto alafu ukampeleka kwa Bibi au mjomba au Ndugu au MTU yeyote Wakati wewe ungali hai. Hiyo ni dalili ya ubinafsi na upunguani, au kukosa maadili na kuharakia mambo Kwa pupa.

Haijalishi Sisi Watoto wengi tumelelewa na kukulia Kwa Bibi au Ndugu Wakati wazazi wetu wapo hai, lakini ukweli thabiti wenye Dawa ya kuiponya jamii lazima usemwe. Huwezi ukazaa mapema ukategemea matokeo mazuri uzeeni. Zaidi Sana upo kwenye nafasi nzuri ya Kupata matokeo mabaya Zaidi.

Sababu pekee ya mtoto kulelewa na Ndugu au jamaa au Bibi(Mama yako) ni wewe Kupatwa na Mauti au Kufungwa Jela, hakuna zaidi ya hapo.

Kuzaa mapema ni ubinafsi wa kiwango cha juu ambao utaleta matokeo ambayo wengi yamewaumiza mioyo Yao. Mtoto wako atahitaji nafasi yako kama mzazi kwake, atahitaji Kupata upendo na malezi Kutoka Kwako.
Na kamwe hutoweza kuutoa Upendo na malezi Kwa mtoto uliyemzaa mapema na hiyo haitakuwa msaada na SULUHU njema nyakati za uzee wako.

Kutokomaa Kiakili, kimaumbile na kihisia inaweza kukufanya uonekane ulifanya uamuzi wa haraka/mapema kuzaa na hii itakufanya usijali Watoto hao.

Kuzaa mapema lazima kufanyike ndani ya familia ya Watu Wawili yaani Mwanamke na Mwanaume waliokatika nafasi Sawa zenye Utayari wa Kupata Watoto. Hii itafanya kila mmoja ndani ya familia kuona thamani ya mtoto ndani ya Familia. Kila kitu kitafanyika kwaajili ya kukuza Watoto kwaajili ya maandalizi Yao ya Maisha. Na sio kuwaandaa Watoto kwaajili ya Maisha yenu ya uzeeni.

Kuzaa mapema au Kwa haraka huchangia ndoa nyingi za siku hizi kuvunjika, Kwa sababu mmoja wa wanandoa anaweza kuwa alifanha uamuzi wa mapema na haraka Kabla ya Wakati wake kufika. Uteketeke wa Akili na hisia za mwanandoa mmoja kama haujakomaa kamwe hawezi kujali thamani ya kile walichokileta Duniani.

Haki za malezi ya Baba na mtoto hawatajali. Wao Watafikiri zaidi kuhusu matunzo ya chakula na mavazi na mambo mengine na hii itaonyesha wazi kabisa Watu hao walifanya uamuzi wa mapema katika kuwapata Watoto hao.

Ni muhimu, kuzaa ukiwa tayari umekomaa kiumri, upo vizuri kiuchumi yaani unaweza kujihudumia na kuwahudumia wanafamilia yako(MKE na watoto) na kuwa na Nia na utayari (huu utakuja automatically ukishakuwa na Sifa mbili za juu). Hii itakupa matokeo mazuri sio wewe tuu Bali Watoto wako, jamii yako na Ulimwengu Kwa ujumla.

Taikon Acha nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kuzaa mtoto na kumpeleka kwa Bibi kwetu ni Sunna.. Tena nafosiwa kabisà.

Sababu mosi- Kama ulivyoainisha hata nipate mtoto nikiwa na miaka above 30 bado sijakomaa kila nyanja katika kumlea huyo mtoto. Lazima alelewe na Bibi yake (mama yangu Mimi /nyanya Ake kama yupo .

Pili nia na madhumuni ni kumkuza kiutamaduni ,kifalsafa na kintazamo Namna ambavyo nimekuwa Mimi , maana nitakuwa busy kupambana nikiwa sina muda WA kumlea ...


Ngachoka
 
Sio issue za msaada tu, ama suluhu uzeeni bali huathiri hadi issue za Population Growth. Now days increase in population is a big threat to nature.

Because, you have to understand this people consume vast amount of food, water, energy and area for shelter. That creates environmental catastrophe by pollute and add some waste materials in the environment.

We must understand an Exponential Population Growth and it's consequences.
Post modernism inakusumbua
 
Sijakataa suala la mtu kuitwa babu, hilo lipo tu kiuhalisia kulingana na wakati.

Pointi yangu kwako ni moja tu, unaposisitiza watu wachelewe kuzaa [japo hujasema wachelewe mpaka kufikia miaka mingapi] unajiweka kwenye mtego wa majukumu ya kulea wakati ambapo umri na nguvu vitakuwa vimekutupa mkono.

Lakini pia, muonekano wako kwa wanao utakuwa haufanani na ule wa baba kwa wanae, huu ndio uhalisia, bila kujali kama una uwezo wa kuwalea au vinginevyo, na sio hii story uliyotupigia hapa.
Huo muonekano una impact gani as long as una uwezo wa kuwalea? Kwani wewe unaishi kwa kutegemea wengine watakuchukuliaje au unaishi maisha yako?
 
Wewe hueleweki na hiki ulichoandika, umeandika kwa mafungu ndio maana kinapoteza maana.

Mfano unaposema mtu azae kwa wakati, huo wakati ni upi? atakapofanikiwa kiuchumi? lini? kwamba aendelee kusubiri tu mpaka siku isiyojulikana afanikiwe kiuchumi ndio awe na familia? huku ndiko kunasababisha baba aje kuitwa babu na watoto wake wa kuwazaa mwenyewe, hope mmenielewa na wenzio wenye mtazamo kama wako.
Wakati mwingine unamuona mtu haeleweki kwa sababu wewe ndiye umeshindwa kumuelewa.
 
Swala la kuzaa muda gani haliwezi kuwa na majibu ya kueleweka. Vyote ni probability tu. Unaweza kuzaa mapema ili watoto wakufae baadae na isiwe hivyo. Na inaweza hata kutokea mtoto umemsomesha na yupo vizuri ila asikufae kwa lolote au hata akafa kabisa.

Mimi naona mtu azae pale anapokua tayari malezi ya mtoto, haijalishi ni kuwahu au kuchelewa. Unapozaa lengo kubwa liwe kuleta kizazi kitakachokua n mafanikio dunia. Hapo ujipanhe kumwelekeza na kumuwezesha huyu mtoto kufikia kilr tunaita mafanikio. Zaa na kulea vizuri ukiwa hutegemei return kutoka kwa mtoto, kwani hayo nimatokeo tu
 
Kuzaa mapema kuna faida sana kuliko kuchelewa.ukijipanga vizuri ni bora uzae mapema.sio unastaafu au ni mfanyabiashara una 55 bado unasomesha hicho ni kitanzi bwana mdogo.mimi ni mhanga wa kuchelewa kuzaa hapa nilipo najuta sana.sio kwamba sitapata msaada lakini hata baada ya kustaafu natakiwa mafao yangu yatumike kuwasomesha wanangu.
Kaka kila mtu na akili yake kwenye hii unia. Ninawaonq waajiriwa wengi sana hasa wa serikali wakishapata ajira tu priority ni kuoa na kuanza familia. Nafikiri wana mawazo kama haya. Ila watu wanowaza kufanya shughuli zao na kuwekeza huoa nakuzaa nbaada ya muda sana.

Aliyeajiriwa huwaza kama wewe uwazavyo kwamba niwahi niwasomeshe hawa watoto kabla sijastaafu. Ni sahihi, ila fikiria vipi ukifa leo watoto wako watasoma?

Aliyejiajiri huwaza kuwekeza zaidi, akisha kuwa sawa kwa kiwango akitakacho ndio huanzisha familia. Yeye huwaza kuwa hata siku akifa na mtoto akwa na miaka 5, mtoto anaweza kusoma na kuishi vizuri kwa miradi atakayoiacha. Ndio maana huwa wanapambana sana kuweka misingi mizuri ya miradi yao.

Pole kaka utashinda tu. Ila fikiria zaidi kuwawekea miradi hao vijana. Maana maisha ya leo elimu pekee haitodho kumfanya mtoto asikutegemee.
 
Back
Top Bottom