Akotia
JF-Expert Member
- Dec 16, 2016
- 528
- 1,241
🤣🤣🤣 Utakuja kujua vitu vingi havina formulaHakuna kitu kisicho na formula.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣🤣🤣 Utakuja kujua vitu vingi havina formulaHakuna kitu kisicho na formula.
katika kitu naona nilifanya mistake ni kutozaa mapema.
ningezaa nikiwa na 23 mpaka 30 nafunga nna watoto wa3 halafu nalea sasa ningekua nazeeka nikiwa tayari wanangu wana Fyucha yao ambayo naiona, namimi najizeekea nikiwa na amani rohoni.
Kwa msoto niliopitia huwa natamani niwaone wanangu wakifanikiwa kabla sijafa, kadri ninavyochelewa umri unaenda na maisha skuizi kuuoboa 50 tu changamoto unakuta unamuacha mtoto ana 15 dunia ya leo unakufa na majuto
Faida ya kuzaa mapema ni kuwa na uwezo wa kuwahudumia watoto kwa nafasi. Una miaka 55, tayari watoto wanajitegemea, unapanga jinsi utakavyoufaidu uzee wako.
ukiwa na majukumu akili inafunguka mapema sana mkuu.Ukiwa na miaka 23 utawezaje Kulea Watoto wenye future nzuri ilhali wewe mwenyewe hujajimudu?
ukiwa na majukumu akili inafunguka mapema sana mkuu.
Pia mpaka umri wa mtoto kujitambua na mimi akili iemzidi kukomaa
sasa chance iliyobaki ni nizae nikiwa na 30 na muelekeo pia sina
katika kitu naona nilifanya mistake ni kutozaa mapema.
ningezaa nikiwa na 23 mpaka 30 nafunga nna watoto wa3 halafu nalea sasa ningekua nazeeka nikiwa tayari wanangu wana Fyucha yao ambayo naiona, namimi najizeekea nikiwa na amani rohoni.
Kwa msoto niliopitia huwa natamani niwaone wanangu wakifanikiwa kabla sijafa, kadri ninavyochelewa umri unaenda na maisha skuizi kuuoboa 50 tu changamoto unakuta unamuacha mtoto ana 15 dunia ya leo unakufa na majuto
Alikiwepo haswaa ila mimi niliona bado, nilipoamua sasa ndo hamna baba sahihiUsijilaumu sana. Pia mtu sahihi wa kuzaa nae alikuwepo wakati una umri huo?
Maana mtoto humzai peke yako
Alikiwepo haswaa ila mimi niliona bado, nilipoamua sasa ndo hamna baba sahihi
ukiwa na majukumu akili inafunguka mapema sana mkuu.
Pia mpaka umri wa mtoto kujitambua na mimi akili iemzidi kukomaa
sasa chance iliyobaki ni nizae nikiwa na 30 na muelekeo pia sina
Usijipe stress utakufa wala hautoujua kama ilikuwepo duniani hayo ndo maisha yako usiwe na wasi.Alikiwepo haswaa ila mimi niliona bado, nilipoamua sasa ndo hamna baba sahihi
kwa mtaji huu mkuu aah muda utapotea sanaHapo sawa. Yameshapita. Jitahidi usizidi kupoteza muda ukikutana mtu sahihi.
Miaka inakimbia kama upepo vile
Hiki ndio kipengele kinatufanya tusizae, yani wasiotaka majukumu ni wengi sana, hata ukisema msaidiane hawatakiNi wachache wenye uwezo huo.
Wengi WA vijana wa siku hizi hawataki majukumu, na endapo majukumu yatazidi huyakimbia. Au kuwatupia Watu wengine majukumu Yao.
Wapo wanaume wengi wamewatelekeza wake na watoto wao.
Wapo Wadada maelfu elfu wametelekeza Watoto wao Kwa Bibi zao Huko vijijini
kabisaa... japo hamna kitu kinaboa kama ukiwa tayari kufanya jambo halafu jambo halipoUsijipe stress utakufa wala hautoujua kama ilikuwepo duniani hayo ndo maisha yako usiwe na wasi.
Wazee kibao wanaishi mpaka miaka 80 kikubwa kuomba Mungu ...
FactMkuu kwani kupata mtoto ni lazim??
Kwa maelezo yako, inaonesha ni lazima mtu awe n mtoto.
Kama jchumi wako hauruhusu kwanini ulete kiumbe duniani, ili ukinyanyase?
Yaani haujajipanga, akili huna, pesa huna na umejion una miaka 40, basi unazaa eti usife bila mtoto, huo ni upumbavu huyo mwanao akulelee nani??
kwa mtaji huu mkuu aah muda utapotea sana
maana hamna muelekeo wowote
Hiki ndio kipengele kinatufanya tusizae, yani wasiotaka majukumu ni wengi sana, hata ukisema msaidiane hawataki
kabisaa... japo hamna kitu kinaboa kama ukiwa tayari kufanya jambo halafu jambo halipo
HII haina ukweli!Ukichelewa sana watoto wako watakuja kukuita babu badala ya baba.
Dah!!! Aseeee umesema kilichopo kabisa kwa sasa wala hakuna uongo ndani yake ni ukweli mtupu...Ila acha tupambane meza zitapinduka tu.. kivyovyote mafanikio yatafikia.Umesema kweli Kabisa.
Sisi wazazi wa kiafrika wengi wetu tunazaa mapema sio Kwa lengo la kukuza Watoto vyema ili wajiandae Kwa Maisha Yao, hapana, bali tunazaa mapema ili tuwahi Kupata matunda ya kuzaa.
Unakuta Mzee anamiaka 55 lakini anamsumbua kijana wake wa miaka 28 ATI amtumie Pesa vinginevyo atamlaani.
Alafu huyo kijana kazi yenyewe anayoifanya utabaki mdomo wazi
Yaaan acha tu. Hadi wewe ambaye haupo kwenye maisha hayo unaona huruma lakn wenyewe ahaaaa hata habari hawana. Ki ukweli tunahitaji ukombozi wa kifikraHapo lazima kuna mmoja lazima alambe mchanga. Hasa huyo muolewaji
Yaaan acha tu. Hadi wewe ambaye haupo kwenye maisha hayo unaona huruma lakn wenyewe ahaaaa hata habari hawana. Ki ukweli tunahitaji ukombozi wa kifikra
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mtoto mwenye akili kuwa saidia wazazi wake ni lazima kulingana na kipato chake usipo mpa mzazi wako utampa nani hela yako?KUZAA MAPEMA SIO KUPATA MSAADA/SULUHU ZA UZEENI
Anaandika Robert Heriel,
Kionambali.
"Nazaa mapema ili nipate wakunisaidia uzeeni"
Hapo ataanza kupiga hesabu, "nikifikisha miaka 35 mtoto atakuwa na miaka 10, nikifikisha 45, mtoto wangu atakuwa na 20, hapo nguvu zitakuwa zinaanza kuyoyoma, lakini nitakuwa sinatabu na mtu. Nikifikisha 55, mtoto wangu kashakuwa dume la mbegu au jike la Simba. Hapo sitakosa miambili miambili"
Atameza mate, kisha atasema, kuzaa mapema Raha"
Nani kasema Ulimwengu huu kuna MTU yupo kwaajili yako? Ni Nani huyo?
Taikon Baada ya kufanya chunguzi zangu, ambazo kwa muda huu nazitolea hesabu, nimekaa na Bibi na Babu zangu wenye idadi ya kutosha na umri wa kutosha. Nimejifunza mengi Kutoka kwao, wamenipa uzoefu na mausia Yao. Na kila utakaponiona naandika ujue ni sehemu ndogo ya kile nilichokipata Kutoka kwao kisha kukifanyia uchunguzi wangu binafsi Kwa sababu zakuambiwa unachanganya na zakwako.
Hata hivi leo, haya niyasemayo Mimi Taikon, yasiwe sheria kwako Bali yapokee kisha ukayafanyie uchunguzi wako binafsi.
Kuzaa mapema kuna faida zake na hasara zake, hata hivyo hasara ni nyingi kuliko faida hasa Kwa Zama hizi za ubeberu. Faida kubwa ya kuzaa mapema ni kuyawahi majukumu mapema ya kuandaa kizazi chako, sasa unaweza kuwa unaandaa kizazi tegemezi na Maskini au unaweza kuandaa kizazi kinachojitegemea na chenye utajiri.
Lakini kuzaa mapema maana yake ni nini?
Kuzaa mapema ni kitendo cha kuyawahi majukumu ya Uzazi na ulezi Kabla ya maandalizi au yakujipanga.
Hii itahusisha;
I) suala la umri,
Ii) Hali ya uchumi, na
iii) Utayari.
Kwenye umri kutahusisha mambo ya Akili, hisia, maumbile, Roho n.k. Mtu anaweza akazaa mtoto Wakati Akili yake haijakomaa, au hisia zake bado zinamambo ya kitoto. Hali hii inaweza kuhatarisha malezi na makuzi ha mtoto atakayezaliwa.
Hali ya uchumi, itahusisha uwezo wa kujisimamia, kujitegemea na kutegemewa. Kabla ya kiumbe chochote hakijabeba mimba ni lazima factor ya kujimudu, kujitegemea na kutegemewa na kile kiumbe atakachokileta izingatiwe. Iwe ni ndege, wanyama au Samaki. Haiwezekani kiumbe kibebe mimba Kabla ya kujitegemea.
Kwa upande wa binadamu, ni lazima mtu aweze kujitegemea na awe na uwezo wa kujilisha, kujisimamia na uwezo wa kulisha na kusimamia familia atakayoianzisha.
Wazazi hutoa mafunzo Kwa Watoto wao, mafunzo ya kujidhibiti kitabia hasa zile tabia zenye nguvu lakini zenye matokeo hasi ndani ya jamii, mafunzo ya kufanya kazi na kuzalisha Mali, mafunzo ya kujilinda na maadui iwe wanyama, magonjwa au maadui Watu. Mafunzo ya kukabiliana na nyakati ngumu. Mafunzo ya uongozi na utawala ndani ya nyumba. Mtoto akishahitimu basi atakuwa tayari kuanzisha na kuleta Watoto Duniani.
Ukomavu kiumri wa Kiakili, kihisia na kimwili ukiaunganisha na kujitegemea kiuchumi na kujisimamia ndio italeta Nia na Utayari wa kuanzisha Familia.
Nia au Utayari wowote wa MTU kutaka kuzaa mtoto na kuanzisha familia Kabla ya ukomavu wa Kiakili, kihisia na kimaumbile, Kabla ya kuweza kujitegemea kiuchumi na kuweza kujisimamia na kutegemewa itachukulia kama Tamaa Mbaya ya kushindwa kujidhibiti kitabia.
Hauwezi ukazaa Mtoto alafu ukampeleka kwa Bibi au mjomba au Ndugu au MTU yeyote Wakati wewe ungali hai. Hiyo ni dalili ya ubinafsi na upunguani, au kukosa maadili na kuharakia mambo Kwa pupa.
Haijalishi Sisi Watoto wengi tumelelewa na kukulia Kwa Bibi au Ndugu Wakati wazazi wetu wapo hai, lakini ukweli thabiti wenye Dawa ya kuiponya jamii lazima usemwe. Huwezi ukazaa mapema ukategemea matokeo mazuri uzeeni. Zaidi Sana upo kwenye nafasi nzuri ya Kupata matokeo mabaya Zaidi.
Sababu pekee ya mtoto kulelewa na Ndugu au jamaa au Bibi(Mama yako) ni wewe Kupatwa na Mauti au Kufungwa Jela, hakuna zaidi ya hapo.
Kuzaa mapema ni ubinafsi wa kiwango cha juu ambao utaleta matokeo ambayo wengi yamewaumiza mioyo Yao. Mtoto wako atahitaji nafasi yako kama mzazi kwake, atahitaji Kupata upendo na malezi Kutoka Kwako.
Na kamwe hutoweza kuutoa Upendo na malezi Kwa mtoto uliyemzaa mapema na hiyo haitakuwa msaada na SULUHU njema nyakati za uzee wako.
Kutokomaa Kiakili, kimaumbile na kihisia inaweza kukufanya uonekane ulifanya uamuzi wa haraka/mapema kuzaa na hii itakufanya usijali Watoto hao.
Kuzaa mapema lazima kufanyike ndani ya familia ya Watu Wawili yaani Mwanamke na Mwanaume waliokatika nafasi Sawa zenye Utayari wa Kupata Watoto. Hii itafanya kila mmoja ndani ya familia kuona thamani ya mtoto ndani ya Familia. Kila kitu kitafanyika kwaajili ya kukuza Watoto kwaajili ya maandalizi Yao ya Maisha. Na sio kuwaandaa Watoto kwaajili ya Maisha yenu ya uzeeni.
Kuzaa mapema au Kwa haraka huchangia ndoa nyingi za siku hizi kuvunjika, Kwa sababu mmoja wa wanandoa anaweza kuwa alifanha uamuzi wa mapema na haraka Kabla ya Wakati wake kufika. Uteketeke wa Akili na hisia za mwanandoa mmoja kama haujakomaa kamwe hawezi kujali thamani ya kile walichokileta Duniani.
Haki za malezi ya Baba na mtoto hawatajali. Wao Watafikiri zaidi kuhusu matunzo ya chakula na mavazi na mambo mengine na hii itaonyesha wazi kabisa Watu hao walifanya uamuzi wa mapema katika kuwapata Watoto hao.
Ni muhimu, kuzaa ukiwa tayari umekomaa kiumri, upo vizuri kiuchumi yaani unaweza kujihudumia na kuwahudumia wanafamilia yako(MKE na watoto) na kuwa na Nia na utayari (huu utakuja automatically ukishakuwa na Sifa mbili za juu). Hii itakupa matokeo mazuri sio wewe tuu Bali Watoto wako, jamii yako na Ulimwengu Kwa ujumla.
Taikon Acha nipumzike.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Wewe akili zako ndogo tangu lini mzee akaonekana kijana mfano mwanaume mwenye miaka 60 akawa ni mtanashati watu watasema ni masafi lakini mzee kijana watasema umri wake bado mdogo tatizo uchafu tuHiyo ni misemo tuu ya Watu wenye Akili ndogo.
Kuzaa mapema hakukufanyi usiitwe Babu.
Wapo wazee lakini Kwa namna walivyoyaishi Maisha Yao wanaafya njema na wanaonekana Vijana alafu kuna Watu wanamiaka 45 tuu lakini wanaonekana wazee.
Mtoto wako uliyemuandaa kuwa Bora hawezi kukuona Babu ikiwa umemuwekea mazingira wezeshi.
Lakini mtoto wako hata ungekuwa kijana Sana lakini kama hukumuwekea mazingira rafiki atakuona Mzee wake ni mjinga, msalaba, na mzigo WA misumari.