Maisha yana changamoto nyingi; itokeapo mtu anakuwa na mahusiano mengi, kwa mazingira ya kawaida gharama pia uongezeka, na kupelekea mtu kuwa wa kutoa ahadi tu kuliko kutekeleza.
Nachoweza kushauri; jaribu kumsahahu huyo uliyezaa naye na pambana na maisha yako, ingawa watoto wakikua bado watamuitaji baba yao.
Kuhusu kukumbushia, hii inategemea na wewe una mahusiano gani kwa sasa; kama uko kwenye mahusiano hakuna shida, ila kama hauna ni vizuri pia kukumbushia kwa ajili ya afya ya mwili na akili, huku mkijadili maendeleo ya watoto wenu.