Kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa?

Huu uzi burudani sana, kuna tujibu tuzuri mnoo 😂😂
 
Faida moja ya kuzaliania Kwa viumbe mbalimbali unapata kitu kinaitwa balance of nature faida ya pili unapata kutambua vyanzo vya maisha ya viumbe mbalimbali mfano binadamu,Simba,nyoka
 
Subiri uzee utapata majibu mpaka ya ziada
 
Unataka kuwa mpweke mwenye mawazo na depression maisha yako yote na kukosa hata mtu wa kukupeleka hospitali siku ukiumwa, kukusaidia ukipata shida yoyote na kukufariji alafu mwisho wake ujifie ndani peke yako na uje kuzikwa na serikali siku ukifa na usahulike ndani ya saa 24? basi usizae mkuu.

Na nina uhakika umefikiria na kuandika haya sababu huna mtoto wala mke na upweke ndio umekufikisha hapa.
Ila mtu mwenye familia hawezi kukaa kufikiria haya bali muda wote atakuwa anacheka na watoto na wajukuu zake na kusahau kabisa kwanini yupo duniani au awe anapamba na umasikini na maisha ili watoto wale.
Imagine hapo bado una nguvu je ukiwa na miaka 70?

Kingine ni kwamba huwezi kumkuta tajiri anafikiria dhumuni la maisha bali utakuta yupo busy masaa 24 anafikiria jinsi ya kuendesha company na kudominate soko. vacations plans na mke na watoto wake, jumamosi kuna movie inatoka waende mlimani city pamoja na amesahau kununua tickets. yaani yuko busy na muda hautoshi.
lla masikini tu ndio utakuta ana mawazo kama haya sababu ya shida na kukosa cha kufanya wala kitu cha msingi cha kufanya. hivyo pambana na umasikni sasa hivi kizazi chako kisiwe kama wewe.

Watu ndio chanzo cha furaha ya kweli na hakuna watu wengine watakaokupa furaha na kukufariji zaidi ya familia yako.
Basi usizae mkuu lakini ukizeeka ndio utaona umuhimu wa kuzaa na kuwa na familia na hapo ndio utajua faida yake.
 
Huwezi kuja na sababu kutoka kwenye vitabu vya uongo kama Biblia na Quran kwenye mada fikirishi.. Hivyo vitabu ni kusimulia watoto kabla ya kulala
 
Maisha haya yana biashara kichaa nyingi sana
1. Unakula, unashiba, unasikia njaa, unakula tena.... biashara kichaa
2. Unatafuta pesa kwa nguvu, unatumia zinaisha, unaanza kutafuta tena, unatumia.....biashara kichaa nk
 
Yani maisha niyaishi mimi alafu nisitake faida niipatayo katika maisha? Sasa si angekuja huyo Mungu kuishi akaachana na mimi 🤔
 
Mkuu mwili wa binadamu una rubi, almasi, tanzanite, uranium?
Hiyo nishati hutokana na nini Chifu?

Au wadhani madini ni dhahabu, chuma yatokayo ardhini pekee bila kujua hata mwilini mwako umejawa na madini [emoji848][emoji38]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…