PostGE2025 Kuzimwa kwa Internet kipindi cha Uchaguzi ni ukiukwaji wa haki za Binadamu na imesababisha hasara kubwa

PostGE2025 Kuzimwa kwa Internet kipindi cha Uchaguzi ni ukiukwaji wa haki za Binadamu na imesababisha hasara kubwa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Nyie si mnatuambiaga siku zote Serikali haina hasara..

Hii hasara uliyoitaja hapa umeipata wapi?..
Na hasara kama hii huwezi kukuta waandishi wa habari wa Tanzania au vyombo vya habari waliifanyia uchambuzi wao wako busy kucheza na script za Msigwa na kutuma ndege tupu kusafiri maelfu ya miles kufuata timu ya mpira.
 
Umeandika pumba nyingi maswali yangu ninayokuuliza hujibu.

Hii itakua reply yangu ya mwisho kwako.

Tazama hapa jinsi vyombo vya dola vilivyokabiliana na wafuasi wa Trump pale Capitol, ingekua ndio hizi akili za Muliro na Mafwele siku hiyo wangedocument maelfu ya vifo.


View: https://youtu.be/jWJVMoe7OY0?si=69gMmXgQci_wjFF5

Hao waliofanyia fujo hapa Tanzania wangeenda huko huko USA wakafanyie fujo ikiwa walitaka wachome mabasi ya watu, wakate watu vidole halafu eti waachwe tu waendelee kudunda mitaani kisa demokrasia!. Bull shit.

Hakuna haki maishani inayopatikana bila ya wajibu, bila ya kuheshimu haki za wengine. Vijana walifanya ule ujinga bila ya mwongozo wowote. Wakaleta uhuni wakakutana na mapolisi waliouishi uhuni kabla hata mama zao hao vijana hawajawazaa.

Vijana imebidi wajifunze kwa namna ngumu kwamba wapo wakubwa kuliko wao ambao wanawaongoza maishani mwao.
 
Wanabodi

Kitendo cha Tanzania kuzima internet kwa siku 5 mfululizo toka siku ya uchaguzi mkuu, kimepelekea Tanzania kubalaswa kimataifa, kuwa uzimaji huo wa internet sio tuu ni ukiukwaji wa haki za binadamu, bali pia umesababisha hasara kubwa za ma bilioni ya pesa.

My Take,
Natoa wito kwa serikali yetu,tuko kwenye zama za kidigiti,the world of information power, zamani kupata information ilikuwa hisani,lakini sasa information ni haki,the right to information, baada ya nchi yetu kupitisha sheria ya haki ya kupata habari,kitendo cha kuzima internet,ni ukiukwaji mkubwa wa haki habari kwa Watanzania,nchi yetu tuna bahati tuna wanasheria wazalendo wa uzalendo ukondoo,serikali inafanya madudu,haishitakiwi,kwa kukiuka haki za binaadamu na kusababishia watu hasara, tunakwenda kwenye mtangamano wa nchi za Africa Mashariki,ambao una free labor migration,wanasheria wasio makondoo,kutoka nchi zozote za EAC wanaruhusiwa ku practice, tukiendelea kufanya ujinga kama huu,serikali itanyooshwa kwa kushitakiwa na kulipishwa mabilioni ya fidia!

Na kwa vile tunazuiwa kutumia VPN,hata serikali,msiendelee kutumia mitandao inayohitaji VPN!

Jambo baya kama hili naomba lisijirudie,mimi kwa upande wangu situmii VPN, natumia Samsung S.25 ultra,connectivity yake ni direct to satellite.

Paskali.
Leo tarehe 29 October, 2026 ni kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kilichotokea October 29, 2025. Mimi naiadhimisha siku hii kwa kutafakari kwa kuyatembelea mabandiko yangu, ya post October 29, 2025.

Ila Watanzania tuendelee kupeana pole, kwa kilichotokea, mwaka mmoja ni kipindi kirefu, kuna badhi ya wenzetu wame heal kutokana na muda mrefu kupita, katika kumbukizi ya kilichotokea, tukumbuke kwa kiasi, tusije kujikuta tunapitiliza na kufumua makovu, na kutonesha tena kile kidonda na kuleta machungu upya, tujifunze kusamehe hata bila kuombwa msamaha, ili maisha yaendelee.

Mungu Ibariki Tanzania.

Mzee Pasco.
 
Back
Top Bottom