Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Ule msafara wa waasi wa Wagner kuelekea Moscow kweli ulitisha japoj wengi wetu tunaofuatilia vyema vita hivi tulijuwa hautofika mwisho wa safari.Namna ambavyo ungezimwa ndio tulitofautiana,ni kwa kupigana au kwa njia ipi.
Ukraine na NATO walishangilia sana na kuanza kuongeza petroli kwenye moto kupitia propaganda kwa kuzusha ya ziada.Marekani kupitia Pentagon ilisema wao walikuwa wakifuatilia kwa makini mwenendo mzima wa majibizano ya Prigozhin na makamanda wa Urusi.
Hata hivyo kuzimwa kwa uasi ule umeonesha kwa mara nyengine jinsi gani Putin alivyo mwamba kwenye vita hivi na imeongeza nguvu na moyo wa mapigano kwa jeshi la Urusi. Kwa upande mwengine umeongeza hofu kwa Zelensky na washirika wake wa NATO.
Hata kama kungekuwa na uasi uliofanikiwa basi usingepaswa kuongozwa na Prigozhin mtu ambaye kichwani ni mkavu sana katika historia na hana hekima katika matamshi yake.