Nape"Bichwa kubwa" amekuwa mara kadhaa akijinasibu mbele ya vyombo vya ndani na nje kuwa awamu ya sita inazingatia uhuru wa vyombo vya habari sio kama awamu ya tano,ambapo si kweli.
Jana TEC(Baraza la Maaskofu Katoliki Tz) limetoa waraka wake juu ya Mkataba wa hovyo wa Bandari, kama ilivyo ada na hii sio mara ya kwanza kufanya hivyo,ilitoa Waraka kipindi cha mwenda zake na awamu zote imefanya hivyo kama sehemu ya jukumu lake la kulinda rasilimali za nchi,mdau wa maendeleo nk
Jana chombo pekee kilichoripoti waraka huo ni JF kwenye mitandao yao yote wamefanya hivyo.Heko kwa JF muishi sana.Hakuna ITV,CLOUDS,WASAFI,EFM nk
Millard Ayo alipost lakini alifuta punde baada ya kupokea simu toka mamlaka za juu "Bichwa kubwa".
Sasa ni hivi asomaye na afahamu kuwa Waraka huo wa Maaskofu utasomwa kwenye misa zote hapo kesho 20/08/2023 mbele ya waumini wao juu ya mkataba wa kimangungo wa serikali ya Samia na "Emirate of Dubai"
Serikali ya Samia acheni kibri wananchi hatuutaki huo mkataba wa kimangungo mnafosi kuwapa "Emirate of Dubai" wamewapa nini?
Lolote utakalofanya juu ya bandari zetu hauna baraka la Maaskofu(Watanzania) usiseme hukuambiwa,Sikio la kufa halisikii dawa.
Roma Locusta,Causa Finita.(Rome has spoken,the cause is closed!)
View attachment 2722558=
View attachment 2722560